Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Ukikaa na watu wanaoamini uchawi na kupiga stori za uchawi huwa Kuna mambo ya kushangaza Sana.
1. Mmoja anasimulia eti Kuna mzee alikamatwa na radi ameiweka kwenye mfuko wa salfeti. polisi kumuuliza akasema huwa anaiuza.
2.Mwingine anasema eti radi ikipiga sehemu huwa inataga yai . Basi wataalamu huwa wanachukua hayo mayai na kuyaangua kutoa radi. Anasema kijijini kwao radi ilikuwa inaua Sana wanafunzi hivyo Kuna mzungu alikuja kufunga antenna juu ya shule ili kukamata mayai.
3. Mwingine anasema vile vi narrow bee fly Kuna mtu walimkamata amejaza gunia!, anavisambaza kusumbua watu.
4.Mmoja alikuwa na gono. Anasema alivyoenda kwa mganga mganga akamwambia ametembea na mwanamke mwenye nyoka hivyo huyo nyoka kamuingia.
5. Nasikia Kuna sherehe ukialikwa Yale maji mliyonawia wanayakusanya na kwenda kuchukua nyota zenu.