Miaka kadhaa majira ya Saa 11.20 alfajiri nipo Ubungo Maziwa nasubiri dereva wa ofisi anipitie ili tuwahi kikao pale Manispaa ya Morogoro (Mji kasoro Bahari).
Nikashangazwa kuona pale kituoni kuna wadada na watoto wadogo kabisa wanasubiri School Bus; ilinisikitisha sana.
Lakini nikakumbuka tatizo hili halijaanza miaka ya karibuni, mimi nikiwa shule pale Bunge; kuna watoto walikuwa wanatoka mbali sana kuja shule, hivyo walikuwa wanaamka mapema sana.
Baada ya kukua nikapata ufahamu zaidi kwamba huu utaratibu sio sahihi.
Baadaye likaja wimbi la hizi shule za English Medium; miaka yetu zilikuwa chache St Mary, Brain Trust, Montfort na nyingine. Na watu walikuwa wanatoka maeneo ya mbali kuja kusoma kwenye hizi shule.
Siku hizi English medium zimekuwa nyingi bila kujali ubora, tuna tatizo la watu wa kupeleka watoto lakini bila kujali muda wa mtoto kuchukuliwa na kurudishwa.
Mimi niliamua kabla sijapata mtoto na nikazungumza na mke wangu kuwa katika mazingira yoyote yale, mtoto wetu ataenda shule jua likiwa limechomoza na wakati wa likizo atabaki nyumbani kufurahia mapumziko.
Changamoto ya kwanza
Binti yangu akafikisha miaka mitatu; muda wa kwenda shule ya awali (nursery); nahisi mke wangu akasahau makubaliano yetu. Jioni moja ananiambia kuwa amechukua admission form ya XXX Nursery School; nishule nzuri na pale tulipokuwa tunaishi watoto wengi walikuwa wanasoma hapo, nikajua haya mambo ya wanawake.
Nikamuuliza, watoto wa huu mtaa huwa wanafuatwa saa ngapi na School bus? Akachukua simu akampigia mama Agnes ambaye mtoto wake alikuwa anaingia middle class kwenye hiyo shule; nikamwambia weka loud speaker na uulize muda.
Simu ikaita na sauti nyororo ya mama Agness ikasikika upande wa pili; swali likaulizwa; Mama Agnes akajibu kuwa muda wa school nus ni saa 12.00 kamili asubuhi.
Nikamgeukia mke wangu nikamwambia mtoto wa miaka 3 ili awe tayari saa 12 asubuhi walau umwamshe saa 5 alfajiri. Kabla hajaongea chochote nikamuuliza wewe unaamka saa ngapi kwenda kazini? Akajibu saa 12.30 asubuhi nusu saa saa ya kujiandaa natoka saa 1.00 asubuhi.
Nikamwambia tafuta shule nyingine ya karibu, kama huwezi nitasimamia zoezi mimi mwenyewe na hakikisha school bus inapita kuanzia saa 1.30 asubuhi.
Akaanza kusifia hiyo shule sijui ina walimu kutoka Kenya na mazingira mazuri; nikamwambia mtoto wa miaka 3 kumpeleka shule ni kwenye kukuza tu uwezo wake wa kuishi na watoto wengine na kucheza; nothing else.
Mwisho tukapata shule ya jirani nzuri kabisa na mtoto akawa anachukuliwa saa 1.40 asubuhi. Anapata muda wa kulala, lakini pia hapotezi muda kwenye school bus.
Changamoto ya pili
Binti akamaliza Baby Class, Middle Class, then Pre-standard; tukafanya graduation na kila mtu akafurahi. Likaja suala la Primary School sasa; hapa napo nikaletewa fomu ya shule ambayo ilikuwa imeongoza kiwilaya lakini pia ilikuwa top ten kwenye matokeo ya darasa la saba.
Hii shule naifahamu vizuri lakini ilikuwa mbali na tunapoishi na kama kawaida kuna binti alikuwa anasoma hapo alikuwa anafuatwa saa 11.30 alfajiri.
Nikamuuliza mke wangu; hivi umesahau tena makubaliano yetu; huyu mtoto hawezi kuamshwa saa 11.00 alfajiri ili aende shule tena shule ya msingi. Mke wangu akanuna kweli kwa sababu pale mtaani watoto kadhaa waliandikishwa kwenye hiyo shule, nikamwambia mimi nafanya mambo yangu mwenyewe sina pressure ya majirani wala marafiki. Habari ikafika ukweni, baba mkwe akanipigia simu na kuniambia kuwa amepata lawama kwamba sitaki kupeleka mtoto kwenye shule nzuri. (Huyu baba mkwe zamani huko alikuwa kwenye hivi vyombo vya usalama na alikuwa na ka-cheo cha kuamrisha watu) kwahiyo alidhani anaweza kuniingia vyoyote tu.
Nikamwambia with all due respect, huyu mtoto ni wa kwangu, wewe ni babu tu, hivyo maamuzi ya mwisho kwa mustakabali wa binti yangu yapo mikononi mwangu; akakata simu na mimi hata sikujali.
Baadaye kidogo napokea simu ya mama yangu; akauliza tatizo ni nini? Nikamwambia hakuna tatizo zaidi ya shinikizo tu kwa mke wangu kutaka mtoto asome shule ya mbali ambayo school bus inafika saa 11.30 alfajiri, akashtuka kisha akasema; basi sawa limalizeni hilo suala kwa amani; nikamwambia kwangu amani sio muhimu ila muhimu ni kutomtesa huyu mtoto.
Nikafanya michakato nikachukua fomu shule nyingine ambayo ilishika nafasi ya 4 kiwilaya lakini ilikuwa jirani kiasi na school bus inapita saa 1.30 asubuhi.
Binti akaanza Primary school huku akipata muda wa kupumzika na kulala vya kutosha. Na maendeleo yake yakawa mazuri kabisa.
Changamoto ya Tatu
Alipomaliza darasa la tatu; akapewa ripoti nak ama kawaida akapewa karatasi ya mchanganuo wa ada.
Kwenye karatasi nikaone kitu kimeandikwa ‘’Remidial’’ na tunalipia kiasi Fulani cha fedha. Nikakumbuka nikiwa kidato cha nne pia term ya pili shuleni kwetu kulikuwa na Remidial ila ilikuwa saa moja kila siku mnabaki kusoma.
Nikamvutia waya Mkurugenzi wa shule kuuliza; hii remidial itakuwa ya muda gani; mkurugenzi kwa confidence kabisa akasema wakati wanafunzi wengine wanatoka saa 8.30mchana wanafunzi wa darasa la nne na la saba wao watakaa mpaka saa 11.00 jioni; nikaguna kisha nikauliza mtihani wa darasa la nne nao ni wa kuweka wanafunzi mpaka saa 11.00 kila siku? Akajibu kuwa huo ndio utaratibu wao.
Nikamwambia mtoto wangu atakuwa anatoka saa 8.30 kama kawaida, hatokuja Remedial ila hiyo pesa ya remedial nitalipa. Akaniambia vipi maendeleo ya mtoto? Nikamwambia, saa 2.00 asubuhi mpaka saa 8.30mchana ni muda unaotosha kabisa mtoto kufundishwa kwa ufanisi na akafaulu mtihani wa darasa la nne; akacheka na tukaishia hapo.
Wakati huu wazazi watano tulikataa huu ujinga wa Remedial, hapa nikapata wenzangu walikuwa wanafikiri sawasawa.
Nikampa Habari mke wangu akasema maamuzi ni yako maana huwa unaamua tu.
Kweli mwanangu alikuwa anatoka shule saa 8.30 mchana kwaa mwaka wote akiwa darasa la tatu; ukaja mtihani wa Mock wilaya, akawa nafasi ya tatu shuleni huku akiwa na wastani wa A hata wale Watoto wengine wanne pia walikuwa na wastani wa A wakiwa top ten; Nikasema asante Mungu.
Mtihani wa Taifa, akawa nafasi ya pili shuleni kwao, akiwa na wastani wa A tena na wale wengine mmoja alikuwa namba moja na wote walikuwa kwenye Top Ten. Hapa nikatoa sadaka ya shukrani na kumpatia mtoto zawadi.
Nilipenda kwa sababu ulikuwa ujumbe wa walimu na baadhi ya wazazi kuwa hawa Watoto tunawatesa bila sababu.
Hawa Watoto kwa umri wao wanahitaji muda wa kuwa huru na kucheza.
Changamoto ya Nne
Alipofika darasa la saba, nikapewa taarifa kuwa wanafunzi wa darasa la saba wanatakiwa kufika shule saa 12.50 asubuhi, hivyo school bus itakuwa inapita saa 12.00 kamili; nikaona hawa watu bado hawajanielewa.
Bahati nzuri au mbaya wale wabishi wenzangu wawili walihama Dar hivyo wanafunzi nao wakahama. Nikabaki mimi na wenzangu watatu, mmoja akazidiwa nguvu akaona sio kesi mtoto kuwa shule saa moja; mimi na yule mwingine tukawaambia walimu na wazazi kwenye kikao kuwa Watoto wetu watapitiwa na school bus muda wa kawaida na masomo kwao yataanza saa 2.00 asubuhi.
Hapa sasa mambo yakawa mengi, ikabidi mpaka nipitie miongozo ya elimu ya msingi na utaratibu wake; nikashinda kesi lakini bado mke wangu alikuwa hanielewi; nikamwambia mtoto anafanya vizuri hatuna haja ya kumchosha.
Darasa la saba likaisha nab ado akafaulu viziuri kabisa akiwa na ufaulu wa alama A kwa masomo yote.
Tukafunga ukurasa wa elimu ya awali na msingi.
Miaka kadhaa mke wangu akakiri kuwa nilikuwa sahihi; hii nilitumia kwa mtoto wangu wa pili na Maisha yanaenda vizuri.
Nikukubushe juzi hapa Waziri wa Elimu Professa Mkenda, amesema waziwazi kama unapeleka mtoto shule ya kulipia na mtoto anatakiwa kusoma muda wa ziada, au kwenda shule wakati wa likizo basi wewe kama mzazi hufikiri sawasawa(yaani kifupi hauna akili)
Niwatakie siku njema; wapeni Watoto nafasi ya kufurahia utoto wao. Elimu ya shule ya msingi sio ngumu kiasi hicho cha kuwanyima fursa za kucheza na kufurahi.
Soma pia

- Wizara ya Elimu inaruhusuje watoto wanateswa hivi ili shule zionekane inafanya vizuri kimatokeo
- KERO - Hivi ni sahihi Wanafunzi wa shule ya msingi kwenda shule saa 12 asubuhi mpaka 12 jioni?
- KERO - Waziri Wizara ya Elimu, Ustawi wa Jamii, Wizara ya Maendeleo Wanawake na Watoto, Katibu Mkuu, Necta, Nacte, Tie. OKOENI HAWA WATOTO TUTAWAPOTEZA