Kuanguka kwa uchumi: Serikali inakosea wapi?

Kupanda kwa Bei maana yake Shillingi imeshuka thamani, hivyo watu kupata hasara katika hela zao.
 
Hili la kuuza mashirika ya umma, alikuja litambua na kusema serikali ilikosea kwa kutoweka watchdog .
 
Ni waziri wa pesa mbovu kuliko wote toka uhuru.
Waziri anaefikiri kukusanya kodi kubwa na tozo ndio kukuza uchumi.
Ukweli wa upandishwaji wa kodi na tozo ndicho kitu kimegeuka shubiri kwa wananchi wa kawaida na wa chini maana wao ndio waathirika wakubwa. Matajiri wafanya biashara ni mawakala tu wa kupora fedha za kodi kutoka kwa wananchi na kuilipa serikali.
Halafu pia awamu ya sita inakopa fedha nyingi sana inayoishia kwenye matumizi ya kawaida ambapo ni pigo kwa ukuaji wa uchumi.
 
Huyo waziri hagusiki. Huenda ndiyo mchawi wa Rais
 

Uchumi upi huo unazorota …?
 
Wewe ni mjinga na hujui hata unachoongea 👇
 
Uchumi hatuwezi kuwa stable Kama tunakopa kwa ajili ya kujenga madarasa na nyumba za walimu ambavyo havizalishi
 
Wavivu lazima walalamike tu ngoja tuone maana waliolalamika kwa magufuli ndio haohao wanalalamika kwa Samia
 
Ushauri wa kipumbavu
 
Ni kweli mimi ni mjinga. Lakini najua taarifa ya WB kwamba serikali imeweza kudhibiti mfumko wa bei ya bidhaa ni uongo.
Kuhusu Tanzani kupata mapato makubwa ya kuuza dhahabu, Tanzanite etc nayo si sahihi. Kwa kuwa serikali inaishia kuambulia royalities na export tax basi
 
Unaposema unashuka bila kuweka data sijui tutakuelewa vipi tuambie wakati wa Magufuli ulikuwa% ngapi na sasa upo % ngapi?
 
Wavivu lazima walalamike tu ngoja tuone maana waliolalamika kwa magufuli ndio haohao wanalalamika kwa Samia
Binadamu hatuwezi kuwa na maono au uwezo sawa. Hili halina ubishi. Na pia silalamiki kwa sababu mimi ni mvivu. Hapana. Nalalamika kwa sababu naiona na kuiishi shida tuipatao sisi masikini. Wanasema mwenye nacho (wewe)hamjui mwenye shida.
 
CCM MBELE KWA MBELE
 
Hapatawahi kutokea Rais kama Mkapa Tanzania,wengi wanawaza kuwafilisi Watanzania hasa hasa aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano kwa kujidanganya kufilisi matajiri waliokuwepo na kujitengenezea matajiri wake kama Makonda,Mnyeti,Gambo na Sabaya.
 
Chanzo cha yote ni chaguzi za 2019 na 2020.
 
Ndio maana nakwambia wewe ni mjinga hakuna unachojua..

Kama huamini taarifa kwani huoni miradi inasonga au Kuna mradi umesimama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…