Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,237
- 1,744
Zab 145:14 SUV
[14] BWANA huwategemeza wote waangukao, Huwainua wote walioinama chini.
Moja ya sifa nzuri aliyonayo Mungu ni huruma aliyonayo kwa watu wake, wale watu wanaofika wakati wanavunjika moyo kutokana na mambo mbalimbali wanayokutakana nayo katika maisha yao, Yeye huwainua tena.
Mtu anaweza kuanguka dhambini, kutokana na maisha mabaya aliyoishi wakati yupo kwenye dhambi, watu wanaweza kumtenga, ila Mungu yupo tayari kumwosha na akawa safi tena.
Watu wanaopitia katika hali ya unyanyasaji mbaya, wakafika wakati wakajikinai wenyewe, Mungu anaweza kuwaondoa katika hali hizo na akawapa faraja ya kweli, sio hivyo tu, anaweza kurejesha hadhi yao iliyopotea katika maisha yao.
Tunapopitia katika maisha fulani ya machukizo, tunapaswa kuelewa Mungu wetu ni mwenye rehema nyingi na upendo wa kweli, tukirejea kwake atatuganga upya.
Tunaweza kuanguka vibaya katika uchumi, ikiwa jicho letu litamtazama Mungu, tukaendelea kufanya kazi kwa bidii tukimwamini yeye, anaweza kutuinua tena tukarudi kwa viwango vikubwa katika uchumi wetu.
Tunaweza kukutana na mambo mabaya katika ndoa zetu, mume na mke wakatawanyika, Mungu anaweza kuzirejesha upya ndoa hizi.
Kikubwa tunachopaswa kuelewa na kukizingatia katika maisha yetu, tunapaswa kutemtegemea Mungu nyakati zote, hata zile nyakati za majaribu. Maana Yeye anaweza kutuinua tena pale tuliporudi chini.
Ikiwa ulifika mahali umekata tamaa kabisa kutokana na matatizo magumu, huzuni nyingi, kumbuka Mungu hajakuacha, anaweza kukusaidia na kukuinua tena.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana