Kuanza biashara ndogo ndogo ukiwa na majukumu ni ngumu mno kutoboa

Kuanza biashara ndogo ndogo ukiwa na majukumu ni ngumu mno kutoboa

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
"Mnaolalamika hakuna ajira muende mkajiajiri msisubiri kuajiariwa" Hizi si kauli ngeni mjini ila ni kauli ambazo husemwa na watu ambao aidha hawajawahi pitia msoto wa mtaani au wana watu wa kuwapush nyuma yao wakikwama.

Ni kweli, kwa namna moja ama nyingine kujiajiri linaweza kuwa sulihisho la kukosa ajira lakini katika mazingira gani?

Utasikia usiseme huna mtaji ila je, hao walioanza kujiajiri bila mitaji kama kufanya vibarua mpaka wakapata mitaji ni kweli walianza wakiwa wana majukumu? Labda, ila ni ngumu mno maana utakuwa ukilipwa posho makula yote na unakosa hata nauli ya kwenda kibaruani.

Kama tayari una majukumu, mfano familia nk ukakosa kipato leo, pesa kidogo uliyonayo ukaamua kuanzisha biashara uwezekano wa kuipoteza pesa ni mkubwa sana kwani utaishia kuila pesa hiyo badala ya kuendeleza biashara.

Biashara inahitaji pesa uliyoiweka itulie na isitumiwe mpaka biashara ijiendeshe yenyewe, itengeneze faida ila katika hali ya majukumu kusubiri muda biashara itengemae mtu atakula mawe?

Ndio ugumu wa kujiajiri unapoanzia, unajikuta kila siku mtaji unasoma sifuri sababu ukipata 500, una majukumu ya lazima ya sh 400 tayari mtaji umeyumba hapo.

Hili suala la kujiajiri linahitaji mtu ambaye biashara siyo sehemu anayotegea kula humo hapo atatoboa.
 
Ndo maana mie nashangaa mwanaume unaoa halafu shughuli zako za kusua sua au bado hazijakaa vyema huko kwenye ndoa unaenda kumaliza mtaji wote

Naona Tz vijana wengi chini ya miaka 30 wanaoa halafu ukiangalia vipato vyao ni vya kuungaunga kua na familia haiitaji mtu lelemama ndo maana huko kwenye ndoa zenu kelele ni mingi mno

Hakikisha uchumi wako upo sawa unaweza kumudu majukumu ya familia ndo OA wengi kimewalamba
 
Umeeleza vyema, majukumu huharibu kabisa mitaji na muendelezo wa biashara.

Jamaa yangu mmoja anamiaka m5 kwenye biashara ya sabuni, anatengeza mwenyewe na kusambaza kwa jumla madukani, ni expert Sasa ila huoni akisogea mbele kwakua anamajukum mengi ya familia yaani BABA, MAMA mpaka wadogo zake wanamtegemea kwa Kila kitu .

Siku akipunguziwa majukumu au akimaliza majukumu hayo baaasi katoboa .
 
Ndo maana mie nashangaa mwanaume unaoa halafu shughuli zako za kusua sua au bado hazijakaa vyema huko kwenye ndoa unaenda kumaliza mtaji wote

Naona Tz vijana wengi chini ya miaka 30 wanaoa halafu ukiangalia vipato vyao ni vya kuungaunga kua na familia haiitaji mtu lelemama ndo maana huko kwenye ndoa zenu kelele ni mingi mno

Hakikisha uchumi wako upo sawa unaweza kumudu majukumu ya familia ndo OA wengi kimewalamba
Ukioa mwanamke mchakarikaji na mna elewana vizuri mnatoka kirahisi sana
 
Mfano mauzo ni 20,000 kwa siku, labda faida kwenye hayo mauzo ni 3000; Badala aagize mchicha wa 500 apike ale, ataagiza maini kilo ya 14,000 ili kufurahisha mwili. Hapo lazima biashara ife.​
Ukiwa na familia utafuga , utalima mchicha , utaokota mayai bandani , ukiwa na familia ni rahisi sana kutoboa kimaisha , najipima binafsi kipindi nikiwa na mke na sasa🤔
 
Wengi wetu hatuna financial education hata ya msingi Tu, ili utoboe kuna maamuzi magumu Sana inabidi uyachukue, nidhamu ya fedha ni Jambo la msingi Sana hasa ukiwa Huna majukumu makubwa na hata ukiwa nayo pia, sasa ukiwa na familia halafu ndo unaanza biashara na unategemea biashara Kwa Kila kitu basi mtaishi kawa wachawi ww na familia yako, usipokuwa makini unafunga biashara, unapotaka kuingia kwenye biashara rasmi lazima uwe na back up plan, hakikisha Una pesa ya pango ya mwaka mzima (ofisini na nyumbani), hakikisha mazingira ya chakula umeyaweka vizuri, hakikisha Una pesa ya dharura angalau miezi sita na cha mwisho hakikisha Una sehemu salama ya kupeleka familia pindi Tu mambo yakiwa vibaya.
 
Msg sent usikimbilie kuoa wakati mambo yako hujayaweka Sawa hakuna Baraka zinazokuja Bure eti ukishaoa hio ni zana mfu na tunafeli sana kwenye hili jambo
 
Naona Tz vijana wengi chini ya miaka 30 wanaoa halafu ukiangalia vipato vyao ni vya kuungaunga kua na familia haiitaji mtu lelemama ndo maana huko kwenye ndoa zenu kelele ni mingi mno

Hakikisha uchumi wako upo sawa unaweza kumudu majukumu ya familia ndo OA wengi kimewalamba
Ni mwendo wa kuchapiwa tu hakuna namna
 
Ukiwa na familia utafuga , utalima mchicha , utaokota mayai bandani , ukiwa na familia ni rahisi sana kutoboa kimaisha , najipima binafsi kipindi nikiwa na mke na sasa🤔
Hio kufuga na kulima kuna Itaji mtaji hayo mambo unayaanza kabla hujaoa ukishaoa yanakuwa magumu
 
Wengi wetu hatuna financial education hata ya msingi Tu, ili utoboe kuna maamuzi magumu Sana inabidi uyachukue, nidhamu ya fedha ni Jambo la msingi Sana hasa ukiwa Huna majukumu makubwa na hata ukiwa nayo pia, sasa ukiwa na familia halafu ndo unaanza biashara na unategemea biashara Kwa Kila kitu basi mtaishi kawa wachawi ww na familia yako, usipokuwa makini unafunga biashara, unapotaka kuingia kwenye biashara rasmi lazima uwe na back up plan, hakikisha Una pesa ya pango ya mwaka mzima (ofisini na nyumbani), hakikisha mazingira ya chakula umeyaweka vizuri, hakikisha Una pesa ya dharura angalau miezi sita na cha mwisho hakikisha Una sehemu salama ya kupeleka familia pindi Tu mambo yakiwa vibaya.
Cha mwisho hujasema ikotokea umechapiwa baada ya kuishiwa vibunda usitangaze na usinune chukulia km ndio hali ya maisha waliokuzidi wamekuzidi tu hakuna namna
 
Kwenye haya maisha ukitafuta visingizio ni lazima uvipate ,maisha ni kuchagua upambane kubadilisha hali yako ama ukae ukilalamika
 
Back
Top Bottom