Kuanza biashara ndogo ndogo ukiwa na majukumu ni ngumu mno kutoboa

Kuanza biashara ndogo ndogo ukiwa na majukumu ni ngumu mno kutoboa

"Mnaolalamika hakuna ajira muende mkajiajiri msisubiri kuajiariwa" Hizi si kauli ngeni mjini ila ni kauli ambazo husemwa na watu ambao aidha hawajawahi pitia msoto wa mtaani au wana watu wa kuwapush nyuma yao wakikwama.

Ni kweli, kwa namna moja ama nyingine kujiajiri linaweza kuwa sulihisho la kukosa ajira lakini katika mazingira gani?

Utasikia usiseme huna mtaji ila je, hao walioanza kujiajiri bila mitaji kama kufanya vibarua mpaka wakapata mitaji ni kweli walianza wakiwa wana majukumu? Labda, ila ni ngumu mno maana utakuwa ukilipwa posho makula yote na unakosa hata nauli ya kwenda kibaruani.

Kama tayari una majukumu, mfano familia nk ukakosa kipato leo, pesa kidogo uliyonayo ukaamua kuanzisha biashara uwezekano wa kuipoteza pesa ni mkubwa sana kwani utaishia kuila pesa hiyo badala ya kuendeleza biashara.

Biashara inahitaji pesa uliyoiweka itulie na isitumiwe mpaka biashara ijiendeshe yenyewe, itengeneze faida ila katika hali ya majukumu kusubiri muda biashara itengemae mtu atakula mawe?

Ndio ugumu wa kujiajiri unapoanzia, unajikuta kila siku mtaji unasoma sifuri sababu ukipata 500, una majukumu ya lazima ya sh 400 tayari mtaji umeyumba hapo.

Hili suala la kujiajiri linahitaji mtu ambaye biashara siyo sehemu anayotegea kula humo hapo atatoboa.
Makonda mwnyewe ni bilionea lakini hadi leo huwezi kumwambia ajiajiri akakuelewa
 
Biashara Inahitaji ROHO NGUMU sana , Kutokana na Mifumo ya Biashara za Afrika
 
Ndo maana mie nashangaa mwanaume unaoa halafu shughuli zako za kusua sua au bado hazijakaa vyema huko kwenye ndoa unaenda kumaliza mtaji wote

Naona Tz vijana wengi chini ya miaka 30 wanaoa halafu ukiangalia vipato vyao ni vya kuungaunga kua na familia haiitaji mtu lelemama ndo maana huko kwenye ndoa zenu kelele ni mingi mno

Hakikisha uchumi wako upo sawa unaweza kumudu majukumu ya familia ndo OA wengi kimewalamba
Hapa Duniani hakuna binadamu mwenye 100% Assuarance kuwa ipo siku uchumi wake utakuwa upo sawa na ni ndoto ya kilamtu aoe uchumi wake ukiwa sawa ila uharisia haupo hivyo kabisa unajikuta unanedea miaka 40 uko na nature ileile ya uchumi unakuwa huna budi kuoa tu na kupata mtoto.

Mimi ni eary 30's nashukuru uchumi wangu wa leo sio kama wa jana ila siwezi kusema upo sawa na nikiangalia Strenght and Weakness zangu kwenye aspect ya kiuchumi naweza kufika 40's nikiwa hivihivi so siwezi kufika 40's sijaoa na sina mtoto mzee sina Assuarance ya kuwa na uchumi stable and secured.
 
Umeeleza vyema, majukumu huharibu kabisa mitaji na muendelezo wa biashara.

Jamaa yangu mmoja anamiaka m5 kwenye biashara ya sabuni, anatengeza mwenyewe na kusambaza kwa jumla madukani, ni expert Sasa ila huoni akisogea mbele kwakua anamajukum mengi ya familia yaani BABA, MAMA mpaka wadogo zake wanamtegemea kwa Kila kitu .

Siku akipunguziwa majukumu au akimaliza majukumu hayo baaasi katoboa .
Mkuu, unaweza kunitumia sample ya sabuni zake PM?
 
Back
Top Bottom