Kuanza Upya si Ujinga

Kuanza Upya si Ujinga

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Nakumbuka niliwahi kuwa na kaduka kule barabara za namba Tanga mjinišŸ¤£šŸ¤¦ā€ā™€ļø Mwanzoni kalinipa heshima kidogo angalau pesa ya mboga nyumbani haikukosekana, angalau kipindi mambo ya mishahara yanasumbua basi kifaida kikawa kinakidhi mahitaji.

Likaja wazo la ushauri mbalimbali la kuikopea biashara ili ikue, Benki zetu hazina hiyana nyie kukupa Ile mikopo yao, huku na huku Corona ikaja, nani akanunue nguo avae aache kusevu pesa kwa ajili ya chakula, biashara ikabuma, pesa ya pango ikagoma, malipo ya TRA hayapo, ushuru hulipi, posho ya msaidizi hakuna, bills zote hazilipiki na bado una rejesho Benki.

Huu mwaka wala haukuondoka hivyo, likatokea sekeseke nikaikosa ajira nikajionea wala isiwe shida kuwa tu na Jina mjini kwamba namiliki duka lisilonipa chochote, nikaamua kubeba virago vyangu na kurudisha mlango wa watu. Sikuishia hapo tu, baada ya mambo kuwa magumu zaidi ilibidi nijiambie kwa dhati kabisa kwamba kuanza moja si ujinga, nikashuka chini nikatafakari, nikakubali matokeo ya mabadiliko ya Maisha na nikakubali fedheha zote, kejeli, masimango na vicheko ili tu nijitafute nijipate.

Hadi sasa bado najitafuta, na ninakutia moyo usijichoke, endelea kujitafuta na ikibidi kuanza moja Anza tu maana kupotea njia ndio kujua njia
 
Kabla ya COVID-19 kuna biashara nilikua nafanya iliniendea vizuri hadi nikasema nataka kuacha Utumishi wa umma.

Ya nini kupoteza muda 8 hours kwa siku hafu mwisho wa mwezi nalipwa hela inayoingia ndani wiki kwenye biashara yangu.

Aisee, Mungu fundi. Yaliyotokea, hadi leo sijawahi amini. Na mimi pia ilibidi tu nirudishe fremu ya watu, ingawa nilijitahidi kupambana ila nimerudisha mwaka huu mwezi wa 5. Nani anaweza kodi ya mwaka kwa biashara hizi.
 
Nakumbuka niliwahi kuwa na kaduka kule barabara za namba Tanga mjinišŸ¤£šŸ¤¦ā€ā™€ļø Mwanzoni kalinipa heshima kidogo angalau pesa ya mboga nyumbani haikukosekana, angalau kipindi mambo ya mishahara yanasumbua basi kifaida kikawa kinakidhi mahitaji...
Mkuu bado upo Tanga.

Vip biashara ipoje hapo sasa?

Mtaji kiasi gani kwakijana anaejitafuta unaweza kumfaa?
 
Oooh i ll be in Tanga, waja leo waondoka leo, makorora, kwa njeka, duga, mabovu, sahare, ngamiani, mabanda ya papa, bombo, raskazone, Tanga beach resort, nyumbani hotel, majani mapana, kwa michi, nguvu mali.....

šŸ˜…šŸ˜…šŸ˜… anyway Tanga nimepamiss sana.
šŸ˜…šŸ˜…Karibu sana
 
Kweli.

Niliharibu mahali nikataka niachane na jambo lile, baadae nikatiwa moyo kuwa anza upya. Nashukuru kuanza upya kulinirudisha kwenye mstari nikajua nilikosea wapi.

Hata sasa hivi nimekosea tena na nataka kuanza upya, naamini itawezekana.
 
Same to me

Mwezi Aprili mwaka huu nilifukuzwa kazi baada ya kupishana kauli na boss.

Imagine nafukuzwa kazi nikiwa na mwanamke ndani na mtoto anakaribia miaka miwili.

Mwezi May mwanzoni nikatia 500k kwenye biashara flan ila nayo ikafa ht mwezi May haujaisha.

Kuna muda mpaka nikatamani kurudi home ila mwanamke wangu alikuwa akinitia moyo na kunifariji hakuna kurudi nyumbani, kaa hapa hapa tutakunywa hata maji.

Sasa hv mwanamke wangu ndie anayeniweka mjini pamoja na hiyo pesa yake kdg anayoipata ila kwa shida shida tunajitahidi kutoboa nayo.
 
Back
Top Bottom