Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta" Ukweli huu hapa

Haka ka uzi ukute kana somwa sana na malaika chochote kikiombwa huku kitatokea .kujaribu c ujinga .
Aisee wadau mpk 2040 ntakua niko vizuri mpk team ya ligi kuu ntakua namilik
 
Kwenye hiyo orodha ukimtoa Bernard &Lowassa waliobaki wote Enzi hizo walikua vyema Sana!!
Sijui nini kimewabadirisha!
 
Magufuli aliwasikiliza wananchi, na wananchi walimkubali, cha ajabu ilibidi apore uchaguzi ili aendelee kukaa madarakani! Sasa kama unakubalika unanajisi uchaguzi ili iweje.
Hakuna siku mmewahi imebiwa kura zaidi ya kulalamikia tume kisha mnashiriki tena uchaguzi kwa tume ile ile.
 
Huyu mkuu alikua mbele ya mda sana , Mungu amwongezee neema
 
Huujui udikteta kaa kimya kula bata uwezavyo.kama umeiona awamu ya tano ndio ya kidikteta rudi shule kasome uelewe vzr then njoo utuandikie tena, CCM ndio hii bado inatuongoza.
 
Hakuna siku mmewahi imebiwa kura zaidi ya kulalamikia tume kisha mnashiriki tena uchaguzi kwa tume ile ile.
Kuibiwa kura sio jambo linalohitaji ww ukiri, hilo liko wazi. Hao wanaondelea kushiriki hizo chaguzi za kishenzi hiyo ni haki yao. Lakini hakuna mtu anayejitambua ataendelea kushiriki hizi chaguzi za kihayawani kwa mazingira haya. Kama huamini subiri uone idadi ya wapiga kura itakavyoshuka.

Ni aidha machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi ili tupate mabadiliko ya kweli, na hapo ndio box la kura litaheshimiwa.
 
Na kubaliana na wewe kuwa wapiga kura wanaweza kushuka lakini sio kwa sababu ya upinzani bali sababu zipo nyingi.
 
Na kubaliana na wewe kuwa wapiga kura wanaweza kushuka lakini sio kwa sababu ya upinzani bali sababu zipo nyingi.
Nusu ya hao ni wapiga kura wa upinzani. Kuanzia uchaguzi wa 2010 na 2015 walipanda sana, na wengi walikuwa wa upinzani. Alipoingia Magufuli akataka kulazimisha kila mtu aikubali ccm, tokea pale wapiga kura hasa wa upinzani wakapuuza uchaguzi.

Kwa bahati mbaya hata ccm haina wapiga kura wengi, bali wapiga kura wengi huhamasika na uwepo wa wapinzani. Alichokifanya Magufuli cha kunajisi chaguzi waziwazi, kumechangia sana wapiga kura wanaojitambua kupuuza kushiriki chaguzi zetu. Ni kweli kuna sababu nyingine, lakini sababu hasa ni ushenzi uliofanyika chini ya utawala wa Magufuli, na watu hawatarejea tena, hadi kufanyike mabadiliko ya kweli ya tume ya uchaguzi, na kupatikana katiba mpya. Ufahamu kizazi kimebadilika hiki. Sioni mabadiliko ya kweli bila machafuko ama mapinduzi ya kijeshi.
 
Umeandika mambo mengi sijaona ukimtaja Lowasa na hiyo ndiyo tabia yenu ninyi wafia vyama haijalishi mpo chama gani, muwe unaheshimu mchango wa watu. Uchaguzi wa 2015 ni dhahiri ulikuwa ni wa watu wawili wenye ushawishi na wala haukuwa na ushindani wa kivyama. JMP alivutia wapiga kura kutokana na record yake ya utendaji, Lowasa alivutia wapiga kura kutokana na umaarufu wake so usileta fact za uongo humu kuwa Chadema au ccm ilivutia wapiga kura. Wapiga kura wanavutiwa na aina ya wagombea na sio vyama vya siasa japo navyo vina nafasi yake kiasi fulani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…