Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta" Ukweli huu hapa

Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta" Ukweli huu hapa

Kumbe hiyo roadmap ilichorwa tangu 2012, ok! lakini mkae mkijua hiyo Mikakati ovu ya kulinda madaraka itatugharimu wote, kisiasa kijamii na kiuchumi, baada ya miaka 10 nchi itakuwa masikini sana
Mwaka huu "Mkombozi wa Tz amezaliwa" Yote yatakwisha kaka.
swali je,utafika?
 
Niliwahi kusikia kuwa hao watu Deep state huwa wana angalia makosa /madhaifu ya rais aliyepo madarakani kisha wanakuja na majibu muafaka
.Mfn : Jakaya :kipindi chake safari zilikua nyingi mno za nje
Magufuli :kapunguza ama kaacha kabisa
Jakaya : kipindi chake watu wapiga sana hela EPA na kadhalika ,list ya mafisadi,mpk PM pinda akasema wakiguswa nchi itatikisika
Magufuli : yeye anawatia adabu vzr mno
Jakaya: kipindi chake wapinzani waliongea mno tena kwa nguvu zote wote tunakumbuka
Magufuli : yeye kapiga pini kabisa
Jakaya : kipindi chake watumishi walikua wanafanya kazi wajisikiavyo
Magufuli : kaondoa hy dhana

Na Rais Magufuli mpk sasa yuko sahihi kwa maelezo ya mleta Mada maana inaonekana bila kufanya hivi kuna tabia ingejengeka ,ingawa pia kuna madhaifu kadhaa wa kadhaa

Nadhani hata sasa hao Deep state wanatathimini haya yanayofanyika sasa then 2022 kuelekea 2025 waje na jina lingine

Yoyote kwa yoyote mleta Mada alikua deep zaidi
 
Hao "madipu steti" wana akili sana!
Inawezekana huyu hakuwa number one,ila walisoma ramani wakaona hali tete beyond 2015,ikabidi watafute buldoza la kufagia uchafu ili hewa safi irudi halafu yule mlengwa akaja 2020!who knows?!nazungumza hivi sababu ya economic factors.Kama hao madipu steti wapo kweli basi ni lazima wanaliona hili,kwamba hatuwezi kuendelea hivi kiuchumi kwa muda mrefu,tutaua nchi.Sioni matajiri tu wakianguka bali naona waendesha uchumi na matajiri "wabunifu" wakianguka..sijui who is replacing them!Sijui tunaona upande wa utajiri tu au na huu wa muhimu,kwamba "wanaendesha uchumi" nao tunaukumbuka?!tuangalie tusije tukareplace "matajiri" kwa "wenye hela"..wenye hela wamepewa tu wanayo,sio lazima wawe na historia nayo yenye faida kwetu,ila tajiri huanzia kichwani,na hela zake zina historia ya faida kwetu,ukimfuatilia utakuta kajitengeneza kwetu sisi wananchi ,hivyo tuna maslahi nae "sisi tulio wengi"..sio wa kupewa na mtu au kikundi kidogo cha watu..mwenye uelewa kaelewa.i cant simplify my language beyond this point.
 
Je unadhani,hii tendency,ni nzuri
 
do u think this is the right,way of tackelling tning
 
4. Suala zima la ushawishi wa dini, endapo ataegemea dini moja basi atajikuta yupo kwenye wakati mgumu kwani atajikuta amegeuka gafla na kuwa adui wa dini nyingine hivyo kujikuta akichukua maamuzi ya kibabe ili kukabiliana na upinzani kutoka dini fulani. Suala kujiunga na dini ya mashetani au "FREEMASONS" litakuwa jambo la kawaida na watu wengi wenye kupinga serikali watatoweka na wasijulikane wapo wapi
 
Mungu akufumbue macho uone mwanga badala ya giza la udikteta!

tunapigania utawala wa sheria na haki, na ndio tunawataka watanzania wote pamoja na wewe tuelewe!
Tanzania ni ya watanzania wote, si ya hao unaowataja! Amka!
Oyaaa mzimaa
 
Sikubaliani na wewe, baada ya 2015 kutakuwa na katiba mpaya ambayo haitampa raisi madaraka makubwa na kutakuwa na utawala wa sheria, pia kuwawajibisha wavivu siyo udikteta, swala la mashoga raisi hawezi kuwa na maamuzi nalo kwani litakuwa chini ya mahakama ya katiba kuamua, kumbuka wakati huo mahakama zitakuwa huru, tofauti na sasa.

Kuhusu kupola mali za mafisadi huenda hasifanye hivyo, badala yake akawasamehe, akaunda tume ya uwazi na ukweli ambayo itawahoji watakaohisiwa walikuwa mafisadi ili wasaidie kuzuia ufisadi usitokee kirahisi.

Rais ajae atakuwa na kazi ngumu sana, kwani kila idara ya nchi imeoza na hawezi kuwa na nguvu sana kisheria kama alivyo raisi wa sasa.
Nakusalimia
 
adolfhitlernazipropagandaeslebedeutschland.jpg

Kwa nini nimeamua kusema hivi? Kuna mambo matano (5) makuu yananilazimisha kusema kuwa:
"Tanzania itatawaliwa kidikteta"
Ni vigumu sana kwa mtu asiyeona mbali kunielewa kirahisi na pia ni rahisi sana kwa anayependa demokrasia kunibeza na kuniona kama naota.

1. Kwanza kuna uwezekano mkubwa Rais ajaye ataingia madarakani kwa utata nikimaanisha kutakuwa na mizengwe katika utoaji wa matokeo kwani hali halisi inajionesha wazi kuwa kuna mvutano mkubwa wa vyama viwili na hakuna kinachokubali kuwa kimeshindwa ki-haki.Endapo mgombea wa chama tawala akashinda basi chama kikuu cha upinzani kitatumia nguvu ya umma ili kupata sapoti wakati aliyejiona kashinda kwa haki atakimbilia ikulu na kushawishi dola kulinda ushindi wake kadri wawezavyo.Tukumbuke yaliyozikumba nchi za :LIBYA, IVORY COAST, LIBERIA, NIGERIA, ZIMBABWE, KENYA, VISIWA VYA COMORO, MISRI na TUNISIA.

2. Pili ni ahadi atakazozitoa hususani zile za kushughulikia "MAFISADI". Ili kupambana na aliyekuzidi kifedha lazima uchukue fedha zake kwa nguvu hivyo atataifisha mali za waliosemekana ni wahujumu uchumi au mafisadi. Akiwa yupo kwenye hali hiyo lazima watamwinda hivyo itamgharimu kuwa dikteta katika kupambana na mafisadi ikiwa ni pamoja na kunyonga baadhi yao ili kuweka fundisho. Pia atajikuta analipa kisasi cha mateso yote yaliyompata katika harakati za kuingia ikulu.

3.Suala zima la maendeleo haliendani na kuwapa watu uhuru wa kukaa mijini na kuendeleza masuala kama ya kupiga debe, kutembeza vitu mijini, kuuza na kula madawa ya kulevya, polisi wa barabarani kupokea rushwa, maafisa wa TRA kusamehe kodi na kutoa vibali kwa njia za panya, viongozi wa serikali kutumia ofisi zao kama kampuni zao! Yote haya yatasababisha rais ajaye awe dikteta na mkatili kwa wazembe wote wanaokwamisha matarajio yake, ikiwa ni pamoja na kuwafurutisha vijana wote mijini na kuwafukuza kazi wazembe wote.

4. Suala zima la ushawishi wa dini, endapo ataegemea dini moja basi atajikuta yupo kwenye wakati mgumu kwani atajikuta amegeuka gafla na kuwa adui wa dini nyingine hivyo kujikuta akichukua maamuzi ya kibabe ili kukabiliana na upinzani kutoka dini fulani. Suala kujiunga na dini ya mashetani au "FREEMASONS" litakuwa jambo la kawaida na watu wengi wenye kupinga serikali watatoweka na wasijulikane wapo wapi.

5.Ushawishi wa nchi za magharibi; hili nalo ni tatizo ambalo nitafanya nchi isitawalike endapo Rais ajae ataamua kufuata matwakwa ya raia wake kwenye masuala la uwekezaji, ajira, ugawaji wa ardhi, kodi, na utaifishaji wa mali za umma kama viwanda, mashamba makubwa, n.k.na endapo atawageuka wananchi na kusikiliza matakwa ya nchi za magharibi basi atajikuta amepitisha sera ya ndoa za jinsia moja, biashara haramu ya siaha, urutubishaji wa nyuklia. Hali hii itapelekea wanachi waanze kumchukia na atajikuta anatumia nguvu za dola kulazimisha wananchi wakubali sera zake.

Pia kuna mambo mengine kama kuibuka vyama vya siasa vyenye nguvu vinavyotaka kumtoa madarakani kwa nguvu na atajikuta akiwasweka rumande wapinzani wengi ambapo itachafua hali ya hewa ya nchi. Pia utata wa mgawanyiko wa wabunge maana kuna kila dalili vyama viwili vyenye ushindani kugawana sehemu kubwa ya idadi ya wabunge na hivyo kumlazimisha Rais kuwa na wakati mgumu wa kuvunja bunge zaidi ya mara moja kwenye kipindi cha miaka mitano.

Pia suala la ajira litaendelea kutesa nchi na ongezeko la wasomi itakuwa pia tatizo hivyo itamlazimu kutumia sheria kali na za kibabe ili kuendesha utawala wake.

Vyombo mbalimbali vitanyimwa uhuru wa kutoa mawazo yao hii itapelekea vyombo vya habari vya magharibi kumuulika nchi na hivyo hali kuwa mbaya zaidi.

Swali la kujiuliza, Rais ajaye atakuwa nani ?

Ni vigumu kupata jibu la moja kwa moja ingawa watu wengi wanatazamia kuona sura mojawapo kati ya hizi:
- Zito Kabwe,
- Dr. Willbrod Slaa,
- Dr. Asha Rose Migiro,
- Edward Lowassa.
- Samwel Sitta
- Prof. Ibrahim Lipumba.
- Bernad Membe, na
- John Pombe Magufuli
.

Kwanini Watanzania wengi wanategemea kati ya watu hawa mmoja wapo atakuwa Rais wa Tanzania mwaka 2015?
Jibu kubwa na la msingi ni suala zima la uwajibikaji na kujituma.

Kwanini nasema hivyo?
Ukiangalia sura zote ni watu wachapa kazi, wanajituma na wenye maamuzi magumu kwa masuala nyeti ya nchi. Ingawa kila mmoja ana mapungufu yake lakini ukweli bado unabaki pale pale wanauwezo mkubwa wa kulifikisha taifa pale Watanzania wanapotaka ikiwa watatekeleza majukumu yao ipasavyo.

Bado suala la wapinzani kuungana na kumsimamisha mgombea mmoja litakuwa ni ndoto. Kwanza utofauti wa sera na mawazo yao vinakinzana. Pia kuna suala zima la itikadi ya chama na mitazamo. Wapinzani wamejifunza mengi kutoka kwa jirani zao Kenya. Hivyo hawapo tayari kuungana na kuanza kung'ang'aniana madaraka ni bora kila mmoja ashiriki kwa nguvu zake na ashinde kwa nguvu zake.

hii ilikuwepo au huwa kuna namna wanaedit kalenda??? nina wasiwasi sana
 
Back
Top Bottom