Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta" Ukweli huu hapa

Mkuu tunaomba maono yako juu ya yajayo hasa kuhusu huyu Mwamba Mbowe na kesi yake pamoja na mustakabali wa Katiba mpya Tanzania na uongozi wa Bi. Hangaya kwa ujumla.
Hiyo kesi ni ya ku buy time tu ili katiba mpya isipatikane mapema kabla ya muda haujafika!!kesi itafutwa na katiba itapatikana ndipo MWAMBA ATAKUWA WAZIRI MKUU WA TANGANYIKA!!KUMBUKA KATIBA MPYA ITAKUA YA SERIKALI TATU AMBAYO ITAKUA NA MAWAZIRI WAKUU WAWILI NA RAISI MMOJA WA MUUNGANO WA TZ!!!!
 
Mkuu Mbowe ni kiungo kikuu cha chama,,,na hana muda wa kuwa rais kwan anawaamini wale wote watakaoteuliwa na chama,,,na hilo watz wanalifahamu,,,,mbowe atabaki kama mgombea ubunge na baadaye kuja kuteuliwa kuwa waziri mkuu kutokujali ni kiongozi gani atakayechaguliwa ,,haijalishi atatoka ccm cdm au cuf ila jua atakuwa waziri mkuu wa nchi hii najua hutaweza niamini kwa haraka lakini utajua baada ya katiba mpya ikitoka..
Ni kweli mama ataleta katiba na Mbowe atakua Waziri mkuu!!
 
Ungeomba maono kwa ujumla. Anaweza akakupa hayo ya Mbowe negatively then ukaanza kumtusi. Just thinking aloud

Mkuu,Kwanza nilichoomba hapo ni 'maono' yake na sio 'maoni' kuna utofauti hapo.

Pili,matokeo ya huko mbele sio kosa lake wala matakwa yake ni kitu kitakachotokea ambacho sisi pengine hatukijui bado ila kuna wenye karama wanaweza jua.
Ndio maana hata maono aliyosema kwenye Uzi huu kuna watu walimpinga na wapo waliochukia lakini bado haikubadili uhalisia sababu ndicho kilichokuwa kitokee

Kwahio sina sababu ya kumtukana yeyote kwa sababu ya maoni au maono yake.

Tatu,ukisoma vizuri nimeomba maono ya Kesi,Katiba mpya na Uongozi wa Hangaya kwa Ujumla.
 
Kwa nini nimeamua kusema hivi? Kuna mambo matano (5) makuu yananilazimisha kusema kuwa:
"Tanzania itatawaliwa kidikteta"
Ni vigumu sana kwa mtu asiyeona mbali kunielewa kirahisi na pia ni rahisi sana kwa anayependa demokrasia kunibeza na kuniona kama naota.

1. Kwanza kuna uwezekano mkubwa Rais ajaye ataingia madarakani kwa utata nikimaanisha kutakuwa na mizengwe katika utoaji wa matokeo kwani hali halisi inajionesha wazi kuwa kuna mvutano mkubwa wa vyama viwili na hakuna kinachokubali kuwa kimeshindwa ki-haki.Endapo mgombea wa chama tawala akashinda basi chama kikuu cha upinzani kitatumia nguvu ya umma ili kupata sapoti wakati aliyejiona kashinda kwa haki atakimbilia ikulu na kushawishi dola kulinda ushindi wake kadri wawezavyo.Tukumbuke yaliyozikumba nchi za :LIBYA, IVORY COAST, LIBERIA, NIGERIA, ZIMBABWE, KENYA, VISIWA VYA COMORO, MISRI na TUNISIA.

2. Pili ni ahadi atakazozitoa hususani zile za kushughulikia "MAFISADI". Ili kupambana na aliyekuzidi kifedha lazima uchukue fedha zake kwa nguvu hivyo atataifisha mali za waliosemekana ni wahujumu uchumi au mafisadi. Akiwa yupo kwenye hali hiyo lazima watamwinda hivyo itamgharimu kuwa dikteta katika kupambana na mafisadi ikiwa ni pamoja na kunyonga baadhi yao ili kuweka fundisho. Pia atajikuta analipa kisasi cha mateso yote yaliyompata katika harakati za kuingia ikulu.

3.Suala zima la maendeleo haliendani na kuwapa watu uhuru wa kukaa mijini na kuendeleza masuala kama ya kupiga debe, kutembeza vitu mijini, kuuza na kula madawa ya kulevya, polisi wa barabarani kupokea rushwa, maafisa wa TRA kusamehe kodi na kutoa vibali kwa njia za panya, viongozi wa serikali kutumia ofisi zao kama kampuni zao! Yote haya yatasababisha rais ajaye awe dikteta na mkatili kwa wazembe wote wanaokwamisha matarajio yake, ikiwa ni pamoja na kuwafurutisha vijana wote mijini na kuwafukuza kazi wazembe wote.

4. Suala zima la ushawishi wa dini, endapo ataegemea dini moja basi atajikuta yupo kwenye wakati mgumu kwani atajikuta amegeuka gafla na kuwa adui wa dini nyingine hivyo kujikuta akichukua maamuzi ya kibabe ili kukabiliana na upinzani kutoka dini fulani. Suala kujiunga na dini ya mashetani au "FREEMASONS" litakuwa jambo la kawaida na watu wengi wenye kupinga serikali watatoweka na wasijulikane wapo wapi.

5.Ushawishi wa nchi za magharibi; hili nalo ni tatizo ambalo nitafanya nchi isitawalike endapo Rais ajae ataamua kufuata matwakwa ya raia wake kwenye masuala la uwekezaji, ajira, ugawaji wa ardhi, kodi, na utaifishaji wa mali za umma kama viwanda, mashamba makubwa, n.k.na endapo atawageuka wananchi na kusikiliza matakwa ya nchi za magharibi basi atajikuta amepitisha sera ya ndoa za jinsia moja, biashara haramu ya siaha, urutubishaji wa nyuklia. Hali hii itapelekea wanachi waanze kumchukia na atajikuta anatumia nguvu za dola kulazimisha wananchi wakubali sera zake.

Pia kuna mambo mengine kama kuibuka vyama vya siasa vyenye nguvu vinavyotaka kumtoa madarakani kwa nguvu na atajikuta akiwasweka rumande wapinzani wengi ambapo itachafua hali ya hewa ya nchi. Pia utata wa mgawanyiko wa wabunge maana kuna kila dalili vyama viwili vyenye ushindani kugawana sehemu kubwa ya idadi ya wabunge na hivyo kumlazimisha Rais kuwa na wakati mgumu wa kuvunja bunge zaidi ya mara moja kwenye kipindi cha miaka mitano.

Pia suala la ajira litaendelea kutesa nchi na ongezeko la wasomi itakuwa pia tatizo hivyo itamlazimu kutumia sheria kali na za kibabe ili kuendesha utawala wake.

Vyombo mbalimbali vitanyimwa uhuru wa kutoa mawazo yao hii itapelekea vyombo vya habari vya magharibi kumuulika nchi na hivyo hali kuwa mbaya zaidi.

Swali la kujiuliza, Rais ajaye atakuwa nani ?

Ni vigumu kupata jibu la moja kwa moja ingawa watu wengi wanatazamia kuona sura mojawapo kati ya hizi:
- Zito Kabwe,
  • Dr. Willbrod Slaa,
  • Dr. Asha Rose Migiro,
  • Edward Lowassa.
  • Samwel Sitta
  • Prof. Ibrahim Lipumba.
  • Bernad Membe, na
  • John Pombe Magufuli
.

Kwanini Watanzania wengi wanategemea kati ya watu hawa mmoja wapo atakuwa Rais wa Tanzania mwaka 2015?
Jibu kubwa na la msingi ni suala zima la uwajibikaji na kujituma.

Kwanini nasema hivyo?
Ukiangalia sura zote ni watu wachapa kazi, wanajituma na wenye maamuzi magumu kwa masuala nyeti ya nchi. Ingawa kila mmoja ana mapungufu yake lakini ukweli bado unabaki pale pale wanauwezo mkubwa wa kulifikisha taifa pale Watanzania wanapotaka ikiwa watatekeleza majukumu yao ipasavyo.

Bado suala la wapinzani kuungana na kumsimamisha mgombea mmoja litakuwa ni ndoto. Kwanza utofauti wa sera na mawazo yao vinakinzana. Pia kuna suala zima la itikadi ya chama na mitazamo. Wapinzani wamejifunza mengi kutoka kwa jirani zao Kenya. Hivyo hawapo tayari kuungana na kuanza kung'ang'aniana madaraka ni bora kila mmoja ashiriki kwa nguvu zake na ashinde kwa nguvu zake.
MAGAMBA MATATU
Mkuu, njoo utueleze pale Bi Kubwa anapeleka nchi kwa sasa!
 
Ulitabiri sahihi.Mwenda zake alipoteza,aliteka,aaliua alifunga. Ili kulinda utawala wake. He 2025,ANATAKIWA aweje. Type nondo.
 
Nabii Bado Yupo Hai, Tafadhali Tunangoja Unajimu Wako
Bila Shaka Yoyote Unakokotoa Awamu Hii Ya Sita Nyota Ikoje
 
Kwa hii list ulioweka...
Wa mwisho ndio mshindi na ndo wa Kwanza kuondoka! Cc mshana jr
 
Niliamua kuwa kimya,,,ila soon nitawapa ukweli wa kitakachojili baada ya uchaguzi wa 2025,,ila kuna shida kubwa sana ipo kwa uongozi uliopo baada ya kifo cha mhusika

Kakaaaaaa,,nipoooooo
Naona mama ameanza kuhujumiwa na wateuzi wa Mwendazake!!Tatizo mama katangaza mapema kuwa atagombea 2025 na kuzua taharuki kwa wale wanaoutaka u namba moja!!!Nadhani matatizo ya uongozi wake yatatokana na yeye kutangaza nia mapema hapo 2025! Bado ni mbali tuombe uzima kabisa!kuna mengi yatajiri!!!
 
Back
Top Bottom