CCM ndio tumaini la mamilioni ya watanzania.ndio kilichobeba kesho bora ya watanzania
Matumaini ya Nini hasa na nani alipoteza hayo matumaini?
Kimsingi unapozungumza matumaini ni kwamba Kuna Hali ya kukata tamaa katika jambo Fulani na hivyo Kuna mtu au watu wanaonesha kwamba yapo matumaini mbele na usiendelee kukataa tamaa. Kwahiyo watanzania wamekata tamaa katika mambo ya kisiasa kijamii na kiuchumi
Kwa kuzingatia muktadha huo naungana na wewe kwamba watanzania wengi wamekata tamaa na kwa maana hiyo wameamua kususuia na mchawi yupo msibani na anwapa matumaini huku akitumia msiba huo kujinufaisha yeye na familia yake.
Kinachofanyika hivi sasa ni ushahidi bayana kwamba katika swala la demokrasia, utawala Bora na uwajibikaji umekua kiini macho. Uendeshaji wa zoezi la uandikishaji limebainisha namna uhuni wankuandikisha marehemu, watu waliopotea na walio chini ya umri vilivyosababisha watu kukata tamaa, hivyo wanahitaji kupewa matumaini ya kuchagua viongozi kwa uchaguzi huru na WA Haki.
Mauaji na ukamataji wa viongozi wa vyama vya siasa ni bayana ya kujenga hofu kwa watanzania kukata tamaa ya kushiriki kwenye chaguzi. Hii pamoja imewekwa bayana na viongozi waandamizi wa chama Nape Nauye na Yule DC. HAlii hii ya kuwa na matokeo mfukoni nindhahiri inakatisha tamaa kwamba kura haimui matokeo Bali utashi na matakwa ya watu Fulani.
Watu wamekata tamaa kwani kasi ya maendeleo na ujuaji wa uchumi imebaki kwenye Rushwa ya takwimu, (statisticous corruption) lakini uhalisia hakuna. Wahitimu wa vyuo vikuu licha ya kumaliza wakiwa wadaiwa wa serikali hawana matumaini ya kuajiriwa au kujiajiri kwani mazingira ya kujiajiri serikali imeyapa kidogo. Chawa Ndio wanapewa nafasi za uteuzi na wazee waliochoka Ndio wanarudishwa kwenye mfumo. Hali hii ni dhahiri inakatisha tamaa! Nani wa kuleta matumaini!
Kinachofanyika kesho katika serikali za mitaa ni wezi wanaoenda kubadilishana nafasi katika kusimamia mapata yatokanayo na shughuli za walalahoi katika mitaa kwa kile wanachoita ushuru, nyumba za kupanga za Ccm Yani frem, ushuru wa taka na fedha za ulinzi shirikishi, fedha za mihuri na barua za utambulisho pamoja na kusaidiana na watendaji kugawana ardhi na fedha za maendeleo zitokanazo na Kodi za wananchi!
Mpambano mkali unaouona sio kwamba Wana kiu ya kuongoza la hasha ni kugombea fursa hizo za kiuchumi! Hali hii husababisha watu kukata tamaa wanahitaji matumaini!
Ukisema Tanzania inahitaji matumaini, ni kweli Ccm imetawala nchi hii kwa miaka 60 sasa na inawajibika kwa kiasi kikubwa kupoteza matumaini ya watanzania. Ni Ccm Chini ya Magufuli ilisitisha ongezeko la mishahara ya watumishi wa uma, Ajira za watumishi wa umma pamoja na kuongeza makato ya loan board kufikia asilimia 15.
Kwahiyo haiwezi kukwepa aibu ya kuwakatisha tamaa watanzania huku viongozi wake waki topea kwenye ukwasi usiomithilika!
Ni Ccm hii hii inawakatisha tamaa wastaafu kwa kuweka kikokotoo na kuwanyima wastaafu Haki Yao ambayo wameitumikia kwa miaka na kutowelekea angalau riba fedha hizo! Wazee wanakufa wakidai madai hayo huku wabunge wa Ccm wakijiongezea mishahara,posho na kiinua mgongo pindi wanapostaafu! Kwanini wasikate tamaa.
Ni Ccm hii inawalaghai wananchi kwa kujenga majengo yanayoitwa vituo vya afya ambavyo wao wenyewe wanaogopa kwenda kutibiwa huko kutokana na huduma mbovu. Hali kadhalika watu hawana bima ya ya afya kwahiyo uhakika wa matibabu Bado ni kigugumizi kisichoisha kwanini watu wasikate tamaa.
Shule walizojenga yamekua majengo ya kukuzuia watoto wa walipakodi. Huku watoto wao wakisoma shule bora za kisasa na zenye elimu Bora ndani na nje ya nchi. Hawaamininhata shule wanazodai wamejenga wao! Huu ni ujinga na ukatishaji tamaa uliopitiliza. Elimu ni Bure, Bure mana Haina chochote zaidi ya kuzalisha wapiga debe, boda boda na baamedi! Ambao watauza baa zao na kukopeshwa boda boda zao na bajaji zao wanazoagiza Kila siku kwa mwamvuli wa kuwawwzesha wananchi! Kwanini watu wasikate tamaa?
Hakuna sectorial linkaje kati ya kilimo na viwanda! Wakulima hawajui hatma yao na mazao Yao, minyororo WA thamani umebakia kwenye makaratasi! Nchi imekua ya wachuuzi badala ya wazalishaji, dampo la bidhaa kutoka nje na kushindwa kuzalisha bidhdaa zake, huku wakinesha vituko kwenye miradi kama SGR, ATCL na BRT kiasi ya kuwapa wageni mpaka viwanja vya ndege ukiacha bandari!
Watu lazima wakate tamaa na wanahitaji matumaini, matumaini wayapate wapi hakuna pa kuyapata mana mifumo Yote wameshika wezi wa Ccm! Walituimbia umeme ukianza kuzalishwa itashuka bei Ili angalau sekta isiyo rasmi iweze kukua. Matokeo yake ni kupanda maradufu kwa bei ya luku kwa kisingizo Cha Kodi ya jengo na maboresho! Huu ni ujinga huku mnasema tuntaka kuuza nje. Kwanini watu wasikate tamaa.
Mama yenu anapiga jaramba eti nishati safi, na kugawa mitungi ya gas kumbe ni biashara ya watu walioko karibu nae. Hakuna mpango wowote wa kisera kuhakikisha kinakua na Ruzuku kwenye gasi na vifaa vyake Ili watu wengi waweze kuaccess na kuaford hiyo gesi pamoja na umeme Ili kupunguza gharama za maisha! Kila kitu Kiko pale pale, je watu wasikate tamaa?
Punguza uchawa na ishi uhalisia mjinga mmoja wewe ashakum sio matusi