Kuanzia leo, biashara ya bar imeniogopesha

kuchangumu

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2014
Posts
724
Reaction score
290
Habari wakuu!

Leo nimepita maeneo ya Kinondoni kuna kitu kimenishangaza sana,miezi kama sita iliyopita nilikunywa bar moja inaitwa Jacaranda bar pembeni yake ipo bar nyingine inaitwa uhuru peak hizi bar zilikuwa habari ya mjini lakini leo jacaranda nimefika kupata kinywaji imekufa kabisa.

Uhuru peak bado wapo vizuri lakini sio kama last time nilipokunywa hapo ipo tofauti last time nyomi ilikuwa ya kufa mtu....nimejaribu kuuliza nikaambiwa kuna bar zingine zimefunguliwa maeneo hayo ambazo ni MK bar na Masai club.

Kitu nilichojifunza walevi hawana sehemu ya kudumu hata ungewapa huduma ya hali ya juu kwa kiasi gani, hususani wateja wa pombe maana ki ukweli bar hizi zilikuwa na huduma nzuri kabla.

ANGALIZO:

Wana JF tukitaka kuwekeza kwenye biashara ya pombe tuwe makini maana nimeona sio biashara inayoweza kudumu kwa miaka mingi na sababu ki ukweli sijazijuwa kikamilifu labda wataalamu wa biashara ya bia waliopo hapa jamvini watuuzie uzoefu kwa faida ya wote wenye nia ya kufanya biashara hii siku za usoni.

Kibiashara zaidi nawasilisha.
 
Fungua baa, weka mademu warembo...na wanaojali wateja
Ndugu hata ukifanya hivyo haitoshi, sema itasaidia i survive kwa muda mrefu kidogo, tatizo lililopo kwa wateja hata ukiwa na walembo kiasi gani, wateja wengi wanakuwa ni kwa ajiri ya ngono tu, wakishawamaliza wote wanaona hakuna jipya, na kama jirani yako patafunguliwa bar iwe na wahudumu wakali hao hao wateja wako watakimbilia kule!!

Cha muhimu ni kuwa na wahudumu walio makini na kazi na wanaojua nini wanafanya, mfano mzuri kwa dar kwenye bar za kisuma utakuta wahudumu wengi ni majimama tena watu wazima ila wateja ni nyomi, tatizo la hao unao waita wakali hawajitumi wao wako kibiashara zaidi hata akiwa na bwana yake mteja mwingine ukiingia hana muda na wewe!!! waulizie wale waliokuwa wanakimbizana kufuata wahudumu Singida waliishia wapi?
 
Fungua baa, weka mademu warembo...na wanaojali wateja

Mkuu nilipokunywa uhuru peak kulikuwa na wahudumu visu sana hata leo nilipopitia nimepata bia kadhaa lakini still wahudumu sio wabaya mimi nimewaona warembo tu na ni wachangamfu pia.
 
Kwa nini kutoka Singida?
 

Kabisa wizard! Kuweka wahudumu warembo baa ni mwanzo wa kuififisha. Wengi wa hao wanageuka kuwa makwini. Huduma hutolewa kwa dharau na ndweo. Kitu cha muhimu biashara ya baa ni wahudumu wanaojituma; na mazingira safi.
 
Ukianzisha bar kwanza ujue unataka wateja wa aina gani. Ukiamua unataka wateja kama wa Rambo ya manzese wawekee menu yao na utadumu nao. Hawa ni wateja kama wa kimboka Buguruni. Unaweza uka target kama wateja middle class kama Rombo Green View na ukadumu nao. on the other hand kama huna target group maalum kama corner bar tegemea kufunga bar ikifunguliwa nyingine jirani. Cha msingi kwa wengi wa Dar. concentrate kwenye jiko na wahudumu waliojazia jazia na wacheshi kisha punguza mziki. Hata mimi utanipata.
 
Hili swali la msingi, na kuna ukweli wengi wanaofungua bar huwa wanaenda singida au manyara kufuata manyara sijui kwa nini......

Wanawake wa Singida wa rahisi kunawa na hawana NO kwa walevi
 
Hili swali la msingi, na kuna ukweli wengi wanaofungua bar huwa wanaenda singida au manyara kufuata manyara sijui kwa nini......

Warembo wa kule hata kama ni mlugaluga huwa wanamwonekano mzuri tofauti na wa huku kwetu akija mjini mpaka apigwe vipodozi kwanza
 

Ndio sababu kubwa ya kwanini bar nyingi zinakufa kutokana na ukweli kwamba kuna wanywaji wengine huwa wapo wapo tu na ni wengi kweli ambao mara nyingi huangalia wapi panavuma na ndio wanakwenda hivyo uki-deal na hawa utapata shida. Kuna wengine wao tayari wana maeneo yao wameshavumbua hata kama utapiga mabanzi unawakuta wanapiga kilaji tena cha kutosha kabisa kushinda hata hao wengine wanaokimbilia kwenye bar inayovuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…