Kuanzia leo, biashara ya bar imeniogopesha

Kuanzia leo, biashara ya bar imeniogopesha

Usiogope mkuu, hakuna biashara inalipa kama pombe duniani, sema Jacaranda mwenyewe kafa (if am not mistaken), mbona kona bar, barakuda, yenu, mawenzi, pazi, hongera (kwa uchache) zipo hadi leo na zinafanya vizuri tu, sema usimamizi tu ndo muhimu na wanywaji wa Kinondoni huwa wanafuata upepo wapi iko mpya ndo wanajazana.

YENU Bar ipo saiti nzuri sana kupoteza wateja ni ngumu mno,ila bar ina wateja kuanzia Asubuhi
 
Singida hasa warangi, wengi wao ni warembo sana, harafu huwa hawakatai mtu kirahisi, na ukiwaangalia wamejariwa.Ndio maana watu wengi waliokuwa wanafungua ma bar wanakwenda huko kondoa ana somba anakuja ana wapangia na gheto, kweli mwanzoni wanaume wale wakwale utawapata kweli!!hadi utaongeza viti, ila baadaye huduma itaanza kushuka kila leo kwani jukumu lao kubwa wanalisahau na ku base kwenye maslahi yao binafsi na mwisho wa siku ni kuanza kuondoka na kutafuta sehemu nyingine watakayoonekana wapya ili soko liwe zuri
 
ukitaka kupata wateja wengi na mauzo kuwa mengi weka wanawake wazuri wenye mvuto huu ndo ugonjwa wa walevi utawakamata wengi sana siyo bar nzuri unaweka wanawake wana sura mbaya mpaka ukiagiza bia unaogopa kumwangalia uso au kukaa naye mezani
 
Duu! Ivi wanawake wao wanafaidi nini? Make hao wanawake wazuri itakua kwa ajili ya wanaume,
Mbinguni kuna bikra 72 kwa ajili ya wanaume.



BTW, mwanzisha mada hajatuambia alienda tarehe zipi apo awali, assume alienda mwisho wa mwezi mara ya kwanza, afu akaenda jana, lazma tofauti iwepo.
unauhakika hao mabikra 72 watakuwepo huko? na ni 72 kwa pamoja au kwa kila mwanaume? na kama wapo unadhani watatoa?
 
kumbukeni lakini,mwenye baa ya jacaranda ameshafariki kitambo,pengine inaweza kuwa sababu ya baa yake kuyumba,maana mtu mara nyingi anakimudu alichokiasisi mwenyewe
 
Biashara ya bar huwa nzuri na endelevu kama una jiko zuri. Kuna bar ipo Boko inaitwa Fyatanga bar ni ya kawaida sana kwa maana ya mazingira na wahudumu wake lakini kuna nyama choma ya mbuzi ya ukweli haswa,ukienda pale weekends utakosa hata pakupark gari. Ni jiko ndilo linawajaza wateja pale na beer zinanyweka haswa.
 
Biashara ya bar huwa nzuri na endelevu kama una jiko zuri. Kuna bar ipo Boko inaitwa Fyatanga bar ni ya kawaida sana kwa maana ya mazingira na wahudumu wake lakini kuna nyama choma ya mbuzi ya ukweli haswa,ukienda pale weekends utakosa hata pakupark gari. Ni jiko ndilo linawajaza wateja pale na beer zinanyweka haswa.


Aione babu Asprin na mkewe Kongosho
 
Last edited by a moderator:
Mapi

Ok,huko kwingine sio wazuri?
 
Last edited by a moderator:
Hapo nashangaa hata mimi mwenye jacaranda alikufa kwa ajali ya gari wakati anarudi nyumbani usiku pale daraja la kawe na mwenye uhuru pk nay hivyo hivyo kafia palepale usiku kwa ajalli hiyohiyo..jacaranda inaendeshwa na mkewe ila uhuru walikua share ndugu watatu.Jacaranda ilifungwa kwa muda wakati wa msiba ila uhuru haikufungwa hata kwa lisaa limoja wakati mmoja wa wamiliki alipokufa.
 
koma kabisaa, wahudumu wenye mazowea ya faster ndiyo mwanzo wa kujitongozesha na kupiga mizinga. mhudumu anatakiwa awe mchangamfu lakini asiwe na mazowea yasiyo na msingi, binafsi nikiingia bar huwa napendelea kuhudumiwa na mhudumu wa kiume.

Alaa kumbe kwa ufupi biashara hii ni ya Wazinzi na wachafu wa tabia?
Kwanini usinywe bia nyumbani.

nitake radhi mkuu, mimi situmii kilaji!

Ahaa kumbe, karibu hapa Kwamtogore tujenge Taifa kwa Chibuku bariidi
 
Fungua baa, weka mademu warembo...na wanaojali wateja

Hiyo baa kama imekufa haina wateja, fungua kanisa pale pale, weeeee wateja (wahumini) watajaa mpaka utukufu wa bwana utashuka!!!
 
Maasai kuna nyapu za kumwaga ndo maana hapakauki wateja
 
Management wadau. Wabongo tunamazoea ya kuogopa kuajiri watu wenye uwezo kue desha biashara. Unakuta manager ni la saba hana ubunifu hata wa kumanage wenzake unategemea nini? Kunajirani yangu hapa kaishia kufunga alikuwa amemwajiri kijana mshamba analeta ubabe tu kuvimba kicha kuitwa manager sasa biashara imekufa na kijana kibarua kimeota nyasi. Hamjiulizi kfc ipo bongo mnadhani mmiliki anakaa hapo?
 
Biasharaa ya bar ni huduma ya uhakika, jiko la maana, wahudumu wa bashasha na kujua aina ya wateja unaotakaa.
Otherwise ni biashara yahitaji sana kukuna kichwa na kutokubweteka asilanii.
Vp rose garden dar badoo inabambaaaa??

Ipo ICU
 
Back
Top Bottom