Kuanzia mwezi huu, June 2024 mishahara ya watumishi wa umma itakuwa inalipwa Kati ya tarehe 28 - 30

Kuanzia mwezi huu, June 2024 mishahara ya watumishi wa umma itakuwa inalipwa Kati ya tarehe 28 - 30

Kwanza mshukuru Mama yetu mpendwa kwa kukulipa mshahara kila mwezi na kujaza tumbo lako.
We endelea kuisifia CCM na hauna hata check no. Sisi tunalipwa na hiyo serikali yako ya CCM ,lakini tunaipiga virungu bila kuchoka sembuse wewe jobless unaye tegemea buku saba?. Subiri kazi za sensa na kuandikisha wapiga kura.
 
Tuct
Taarifa kutoka TUCTA

Ndugu wafanyakazi napenda kuwataarifu kwamba kuanzia mwezi huu mishahara itakua ikitoka tarehe za mwisho wa mwezi yaani tarehe 28-30. Lengo la kufanya hivyo ni kuondoa gap lililopo kati ya tarehe za mishahara wa sektabinafsi na sekta za Umma. Mwenyekiti wa TUCTA kasema hayo leo wakati akipongeza kuongezeka kwa asilimia ya Kikokotoo kutoka asilimia 33 mpaka 40.
Tucta wanahusika vipi na kupanga tarehe za kulipwa mishahara ya watu?
Hiyo sababu waliyoitoa mbona haina mantiki?
Something is fishing here.
 
Kama hii taarifa ni kweli basi serikali ya mama Abdul inazidiwa, mapato yatakuwa yanapungua huku wazito kwenye serikali yake wakizidi kujineemesha.

Hili tangazo lingetakiwa kutolewa mapema kuwaandaa wafanyakazi kisaikolojia, lakini kuwashtukiza hivi ni dalili hii serikali ya huyu mama imefeli kwa namna nyingi, kuanzia wasaidizi wasiojielewa, wala rushwa, poor coordination..
 
Back
Top Bottom