Kuanzisha biashara ni jambo gumu sana kuliko kutafuta ajira

Nunua ardhi pima halafu uza kama viwanja Mfano hapo Dodoma,mji unatanuka sana.
Nina kiwanja sehemu huko kigamboni nimetafuta wateja mwaka wa tano huu sipati yaani Ardhi inahitaji uwe na hela usiyoitegemea ili uzamishe uko isahau utauza siku pakichangamka. Lakini hizi za kwetu tunazotegemea tuzalishe ili tupanuke haraka maisha yaendelee si mchezo
 
Bro biashara isikie tunaongea hapa tu lakini kuimplement ni kitunkingine, unataka ufungue duka unaangalia mwenye duka jirani anashinda anapiga miahayo na anatafuta mikopo
Kabisa nakuelewa mkuu. Kabla hujapata pesa confidence inakuwa juu na mipango kibao. Lakini ukija kuipata sasa, Woga unaingia na yale uliyokuwa ukiwaza awali unaona hayana maana . Unaanza kuwaza upya lakini taratibu ile hela unazidi kuimega kwa mambo ambayo hata hukuyatarajia
 
KIchwa chako ndicho kigumu. Uwekezaji hauhutaji mashauriano mengi. Unapaswa uamue na utekeleze hauwezi kuanzisja biashara leo na kupata ubilionea leo. Ni mchakato. Finally nipe hata 5M kwa hzo afu mwakan muda kama huu nakulipa zote hela zako na faida ya 1M jumla iwe 6M
 
Shida JF Ina vijana wametoka shule wanafikiri wao wakipata 5m wanatajirika kumbe ukiwakabidhi ukarudi mnaanza kulaumiana.
Hii mkuu umesema kweli! Mdogo wangu alikuwa na duka la simu sehemu moja nzuri kabisa huko Dar. Akamweka mtoto wa sister ndio kwanza ametoka chuo, kwamba awe anasimamia maana yeye alihamishwa kikazi. Alipokuwapo faida alikuwa hakosi laki 1 kwa siku. Sasa alivyoondoka tu dogo akazuzuka maana walikubaliana kwamba awe anamtumia laki 5 kila wiki mpaka thamani ya mtaji itakapokamilika ili duka liwe la kwake huyo mpwa! Kwani alifika wapi? Visababu vikawa vingi mara nimeibiwa hela Kariakoo nilifuata mzigo mara wezi wamevunja duka! Shenzi kabisa! Mwisho wa siku dogo akauza vifaa vyote na yeye akarudishwa kijijini na degree yake! Hawajielewi!
 
33ml get rich quick!!

Anyway mkuu unaplan za walau kutengeneza faida ya Tzs ngapi kwa kila mwezi!?
 
Ni kigumu ndiyo ila kimepata 40m Cha kwako kiraisi kinataka kipewe 5M na kichwa kigumu. Mjini pagumu sana mkuu
 
Ni marufuku kufanya biashara na ndugu, ni kutafutiana tu lawama bure mkuu
 
Unapatikana wapi Boss?

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…