Kuanzisha biashara ni jambo gumu sana kuliko kutafuta ajira

Kuanzisha biashara ni jambo gumu sana kuliko kutafuta ajira

political Engineer 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
295
Reaction score
792
Ni muda wa miezi kadhaa, sasa niko na mtaji mkononi wa zaidi ya 40m nimejitahidi kutafuta biashara ya kufanya nimegonga mwamba.

Nimetafuta frame ili nianze biashara ya uwakala wa pesa, Bank Wakala na Mitandao ya simu. Nimekumbana na Kodi kubwa ya frame lakini pia location ya frame Kwa biashara husika haziendani kabisa, nimewaza kuuza nafaka Nako NILIFANYA analysis naona kama mtaji unaenda kudidimia huko, Nikawaza kilimo nikakumbuka kilishanizamisha mwaka juzi, Nikawaza nifungue duka la jumla nikawaza nani akae pale na faida yake huwa ni kidogo sana hii biashara, nikiangalia wanaofanya hawaendelei.

Nimejaribu kutoa mtaji kidogo nikampeleka mtu anunue mahindi Sumbawanga lakini wapi siku hizi mahindi hamna kule, Serikali imeingia hadi wilayani kukusanya mahindi.

Mpaka sasa naona mtaji kila siku unazidi kupungua, kila baada ya week naona milioni inaondoka hata sijui nafanyia Nini.

Kimsingi kwa Afrika hasa TZ kutunzia hela unaangalia si mchezo zinaisha bila kujua ulichofanya.

Na hii ikiisha sijui nitakuwa mtoto wa nani, juzi nilienda bank wakaniambia imebaki 33m.

Hapa sielewi kabisa.
 
Ni muda wa miezi kadhaa,sasa Niko na mtaji mkononi wa zaidi ya 40m nimejitahidi kutafuta biashara ya kufanya nimegonga mwamba.

Nimetafuta frame ili nianze biashara ya uwakala wa pesa ,Bank Wakala,na Mitandao ya simu. Nimekumbana na Kodi k

Hapa sielewi kabisa.
Njoo nayo nitafute pm.itakulipa
 
Huo mtaji mbona ni mkubwa sana mkuu, nikushauri kitu, nunua mashine ya kusaga na kukoboa nafaka tumia madalali kupata mahindi na mpunga kutoka mashambani baada ya kukoboa na kusaga pakia kwenye viroba vya kuanzia kilo 5, 10, 25 na 50, kisha sambaza kwenye maduka na masoko au masoko mtaji wako unatosha sana, huku nina uhakika huwezi kuzama kwa sababu chakula ni hitaji muhimu la kila siku.
 
Njoo Dar uwekeze kwenye biashara ya kuuza Fanicha za ndani kama makabati bedi sofa vitanda utaifanya biashara hii mtandaoni mtaji wa m 5 tu unatosha amini hautakuwa unakosa 600+ kwa mwezi wateja wanapatika fb na Insta na Whatsapp sio lazma kuwa na frame barabaran kazi Yako ni kupost bidhaa tu

NB: Lazma uwe unalipia pages kwenye fb na insta ili upate wateja kiurahisi
 
Huo mtaji mbona ni mkubwa sana mkuu,, nikushauri kitu,, nunua mashine ya kusaga na kukoboa nafaka tumia madalali kupata mahindi na mpunga kutoka mashambani baada ya kukoboa na kusaga pakia kwenye viroba vya kuanzia kilo 5,10, 25 na 50, kisha sambaza kwenye maduka na masoko au masoko mtaji wako unatosha sana,, huku nina uhakika huwezi kuzama kwa sababu chakula ni hitaji muhimu la kila siku,,
Hili ni wazo zuri, nifanye mkoani au Dar maana Mimi nipo Dar ila mikoa yote nimefika napafahamu
 
Back
Top Bottom