political Engineer 2
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 295
- 792
Ni muda wa miezi kadhaa, sasa niko na mtaji mkononi wa zaidi ya 40m nimejitahidi kutafuta biashara ya kufanya nimegonga mwamba.
Nimetafuta frame ili nianze biashara ya uwakala wa pesa, Bank Wakala na Mitandao ya simu. Nimekumbana na Kodi kubwa ya frame lakini pia location ya frame Kwa biashara husika haziendani kabisa, nimewaza kuuza nafaka Nako NILIFANYA analysis naona kama mtaji unaenda kudidimia huko, Nikawaza kilimo nikakumbuka kilishanizamisha mwaka juzi, Nikawaza nifungue duka la jumla nikawaza nani akae pale na faida yake huwa ni kidogo sana hii biashara, nikiangalia wanaofanya hawaendelei.
Nimejaribu kutoa mtaji kidogo nikampeleka mtu anunue mahindi Sumbawanga lakini wapi siku hizi mahindi hamna kule, Serikali imeingia hadi wilayani kukusanya mahindi.
Mpaka sasa naona mtaji kila siku unazidi kupungua, kila baada ya week naona milioni inaondoka hata sijui nafanyia Nini.
Kimsingi kwa Afrika hasa TZ kutunzia hela unaangalia si mchezo zinaisha bila kujua ulichofanya.
Na hii ikiisha sijui nitakuwa mtoto wa nani, juzi nilienda bank wakaniambia imebaki 33m.
Hapa sielewi kabisa.