kanga
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 1,025
- 494
Wadau nipeni maujuzi na utaalamu mwepesi kwa walio weledi katika mambo ya Bima.Nataka kuanzisha kampuni yangu ya Udalali wa Bima. Tayari ninakmapuni lakini haina line ya Bima lakini kwa sasa naona kama kuna Opportunities katika eneo hilo na naweza kucapitalize vya kutosha, ila miye ni mtaalamu wa mambo ya fedha na uchumi siyo Bima.Kwa kutambua nafasi ya jamii forums naombeni msaada katika kukidhi haja yangu ya kuwa na kmapuni ya Bima kwa siku zijazo kwa kuanza na kampuni ya udalali.Msaada kwa wabobezi katika secto hii iwe ni
- Mtaji unaotakiwa
- staff qualification
- maeneo/ location ya biashara
- mahitaji na masharti ya leseni ya Udalali
- na mengineyo yanaendena na biashara hii
- Vijana waliomaliza au kuwa na elimu ya Bima watapewa kipaumbele wakati wa ajira
- Tofauti ya Wakala wa Bima na Dalali wa Bima katika mahitaji ya Usajili.
- Naweza kupata fomu za usajili kwenye mtandao wa Mamlaka ya Bima au ni non- digital?
- natanguliza shukrani kwa elimu nitakayopata toka kwenu.