Kuanzisha thread JF ujipange

Kuanzisha thread JF ujipange

Kule sasa hivi nimekuwa na magroup mawili, moja linanikubali moja halinikubali.

Sababu ambayo group halinikubali:

Naweza kupost picha za hela tsh au dola basi baadhi roho zinawauma kuona zile pesa maana utakuta kwa wakati huo kuna mtu vyuma vimemkaza sana. Aidha anadaiwa au ana shida japo elfu 10 hajui atoe wapi.

Kundi linalonikubali ni kwamba mimi silazi damu, ukija kichwa kichwa kwenye post yangu, utaondoka ukijiuliza hivi ndo yule ambae namuona mstaarabu? Kumbe umekuja kutafuta sifa ili watu wakuone wa maana lakini nakupa makavu.

Wengine sasa hawa like, wala kukoment maana niliwapiga mabomu ya motor hawatosahau.
Ila pia nina marafiki wengi akina dada nikiweka picha tu lazima like nyingi ziwe za kwao mpaka kuna aliekuwa dem wangu kanichunia sababu:
Kuna wadada watano wanawahi seat sasa kile kitendo kilimkera na kunambia ni madem zangu, nilibaki mdomo wazi.

Kwa ufupi nina changamoto sana njoo ujionee mwenyewe.
Acha mbwembwe, kwani Unatumia jina gani huko fb!
 
Back
Top Bottom