Kubadili akaunti ya malipo ya mshahara kutoka NMB kwenda CRDB

Kubadili akaunti ya malipo ya mshahara kutoka NMB kwenda CRDB

Madihani

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2015
Posts
6,154
Reaction score
7,083
Habari wana Jamii,

Naomba kupata ushuhuda kwa waliobadili akaunti za kupitishia mshahara.

1. Je, haiwezi kupelekea kukosa mshahara?
2. Je, mhusika ni HR tu au kuna ngazi nyingine ya kwenye zoezi tajwa?

Kwa upande wangu naona NMB wana shida kwenye mifumo yao, kuna mwezi benki zingine mshahara uliingia ijumaa ila sisi wa NMB tukapata jumanne ya wiki inayofuata.

Jana wadau wa CRDB na benki zingine mshahara umeingia ila sisi wa NMB hatujui nini kinaendelea.

Tatizo hili ni la muda mrefu na kwa upande wangu naona bora kubadili akaunti.

Faida za kuhamia CRDB ni nyingi ila sitazitaja hapa.

Wale ambao vichwa vyao haviko sawa soma kisha pita kimya kimya kuliko kuandika yanayotoka kwenye kichwa kibovu.
 
Nasubiri jibu ili leo leo nifanye utaratibu.
 
Rahisi kabisa, nenda tawi la CRDB jirani watakupa maelekezo
 
Mchakato wake ni rahisi sana,utapata mshahara vizuri tu changamoto huwa inakuja mwishoni kwenye mafao ya kustaafu.

Upande wangu sababu zako hazina mashiko kwani wao wakipata ijumaa wewe jumanne shida iko wapi?

Au riba ya 13% imekuvutia wamekupa sharti la kuhamishia mshahara kwao?
 
Una uhakika nategemea mshahara pekee, wewe ni kati ya wajinga walioambiwa wapite kimya kimya.
Acha kutegemea mshahara pekee bro


 
Andika barua ya kuomba kubadilisha account kwenda kwa mkurugenzi rasirimali watu.
 
Andika barua inayo enda kwa HR inakuwa ushamaliza
 
Unaandika barua kwa mwajiri wako tu mchezo unaisha.

Kama uko kwa mwajiri mdogo andika barua iadress kwa mwajiri mkubwa kupitia kwa huyo mwajiri mdogo.

Yahusu: KUBADILISHA ACCOUNT YA MALIPO YA MSHAHARA.

Mimi joni mwajiriwa katika ofisi yako kama fundi rangi naomba mshahara wangu ulipwe kupitia account namba 11118888444 crdb badala ya account namba 2222000 ya nmb niliyokuwa nikipokelea mshahara.

Asante.
 
Mchakato wake ni rahisi sana,utapata mshahara vizuri tu changamoto huwa inakuja mwishoni kwenye mafao ya kustaafu.
Upande wangu sababu zako hazina mashiko kwani wao wakipata ijumaa wewe jumanne shida iko wapi?
Au riba ya 13% imekuvutia wamekupa sharti la kuhamishia mshahara kwao?
kWENYE KUSTAAFU HAKUNA SHIDA PIA. Mimi nilihama NMB nikaelekeza mshahara wangu upitie CRDB ambako nilikuwa na akaunti pia. Mafao yangu niliyapata bila shida yoyote! na pensheni ya kila mwezi inaingia bila shida yoyote!
 
Back
Top Bottom