Kubadili akaunti ya malipo ya mshahara kutoka NMB kwenda CRDB

Kubadili akaunti ya malipo ya mshahara kutoka NMB kwenda CRDB

Mkuu hamia tu CRDB. Huku hakuna foleni nyakati za mishahara. Mimi nilihamia CRDB mwaka jana nikitokea NMB. HR wako ndiyo anamaliza Kila kitu.
 
Baki NMB bank ya masikin CRDB ni bank ya wafanya biashara utakuja kulia nakwambia na hiyo 13% haipo hivyo amini nakwambia nmb kwako ni bank nzuri kwa muda mfupi tu nimeona una akili ndogo kama chaja ya pini ndogo sababu ulizosema ni upuzi mtupu
 
Nenda CRDB fungua akaunti,

Ukishapata namba ya akaunti ndio uandike barua kwa HR wako kuwa unaomba kuhamisha mshahara na ile namba ya akaunti ya CRDB unai mention.. ukisha hakikisha wameanza kukuwekea mshahara CRDB unarudi NMB kuomba kufunga akaunti. Hata kama unahama bank ni vizuri ukaomba kufunga akaunti officially usiache tu ukatoa pesa ukasepa sio uungwanq.

Kuhusu wenzio wa CRDB kuwahi kupokea inaonekana taasisi unayofanya kazi wanbank CRDB ndio maana wao wanapata chapchap (ni internal transfers)...kwenda bank nyengine inakuwa mpk wapitishe kwa EFT
 
kWENYE KUSTAAFU HAKUNA SHIDA PIA. Mimi nilihama NMB nikaelekeza mshahara wangu upitie CRDB ambako nilikuwa na akaunti pia. Mafao yangu niliyapata bila shida yoyote! na pensheni ya kila mwezi inaingia bila shida yoyote!
Huku mitandoni yatakikana tuwe na adabu ya hali juu vinginevyo utaharibikiwa kabisaa, imagine mkuu mbingunikwetu hadi keshastaafu wakaati wengine ndio kwanza tunasubiri ule msemo "life beginning at forty"
 
Back
Top Bottom