Kubadili dini kisa mahusiano ni usaliti wa imani au ni Upendo?

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Wakuu,
naombeni ,msaada wa ushauri,

Hivi ni sahihi kubadili dini kisa mahusiano? nimekua nikipitia wakati mgumu wa kufanya maaumuzi binafsi ya kubadili dini na kufuata imani ya mwenza wangu ninaempenda, tumeshindwa kufikia muafaka wa ndoa maana yeye hawezi kubadili dini ni mwanaume na kwa upande wangu ni nipo tayari kubadili ila vikwazo ni familia na marafiki, naambiwa bora tufunge ndoa ila kila mtu abaki kwenye imani yake maana hatujui hatima ya maisha yawezekana ndoa yetu isidumu na mimi inakua nishabadili dini

Naomba ushauri
  1. Nibadili dini
  2. Tufunge ndoa ila kila abaki na imani yake
  3. Tuvunje mahusiano
 
Inategemea na mtazamo wako ndg kuhusu dini na imani kama kwako dini ni kuonekana unahudhuria kweny msikitn/church au kuitwa tu we dini fulani fresh badili. Ila kama ni vinginevyo wala usingeuliza maan huwez fuata dini bila kujua misngi na imani ya hiyo dini.
 
Hizi dini za kuletewa zinafanya waafrica waache kutumia akili sawasawa.

Unakuta umepata mtu sahihi kabisa ila ndugu wanaleta ujinga wao wa dini.

📌Binti maisha ni yako,hao wazazi na ndugu zako enzi zao walikuwa wanatoroshana hakuna kufunga ndoa na maisha ni yao yalikuwa biyee bin bulbul, wewe ukiendelea kuwasikiliza utaangukia pua.Tumia akili kama jamaa anaeleweka na umeona kabisa anafaa kufanya nae maisha songa mbele.Hakuna binadamu anayejua hatima yake.Hao ndugu zako waache kukupanda kichwani.

📌Maisha ni GAME OF CHANCE(BAHATI) na bahati haiji mara mbili.Usichezee bahati.

Utamkataa huyo bwanamdogo utatafuta wa dini yako na bado ndoa haitakalika.Songa mbele hayo ni maisha yako na wewe ndo dereva.

Na hata wakikutenga.Pigana ujijenge kiuchumi utaona wanajirudi.Pesa ndio heshima hapa duniani.
 
Kubadili kwasababu ya mapenzi utajuta siku hayo mapenzi yakiisha
 
nakazia
 
Back
Top Bottom