Hizi dini za kuletewa zinafanya waafrica waache kutumia akili sawasawa.
Unakuta umepata mtu sahihi kabisa ila ndugu wanaleta ujinga wao wa dini.
๐Binti maisha ni yako,hao wazazi na ndugu zako enzi zao walikuwa wanatoroshana hakuna kufunga ndoa na maisha ni yao yalikuwa biyee bin bulbul, wewe ukiendelea kuwasikiliza utaangukia pua.Tumia akili kama jamaa anaeleweka na umeona kabisa anafaa kufanya nae maisha songa mbele.Hakuna binadamu anayejua hatima yake.Hao ndugu zako waache kukupanda kichwani.
๐Maisha ni GAME OF CHANCE(BAHATI) na bahati haiji mara mbili.Usichezee bahati.
Utamkataa huyo bwanamdogo utatafuta wa dini yako na bado ndoa haitakalika.Songa mbele hayo ni maisha yako na wewe ndo dereva.
Na hata wakikutenga.Pigana ujijenge kiuchumi utaona wanajirudi.Pesa ndio heshima hapa duniani.