Kubadili NMB chap chap kuwa Personal Account

Suip

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2010
Posts
1,353
Reaction score
815
Nataka kubadili au ku upgrade akaunti ya NMB chap chap kuwa Akaunti ya kawaida kwani nina project inayohitaji kuwekewa zaidi tsh milioni 20 na Cha chap haiwezi kupokea tsh. zaidi ya milioni 5.
Je itachukua muda gani kubadili,na kadi pia itabadilishwa,kama itabadilishwa itachukua muda gani kupata kadi nyingine?
Nawasilisha
 
Nenda kwenye tawi lolote la NMB Kuna form utapewa ujaze..
Maelekezo mengine utayakuta huko huko..
Wanawapenda sana wateja kama wewe na Hakika watakuhudumia vizuri sana.
 
Nataka kubadili au ku upgrade akaunti ya NMB chap chap kuwa Akaunti ya kawaida kwani nina project inayohitaji kuwekewa zaidi tsh milioni 20 na Cha chap haiwezi kupokea tsh. zaidi ya milioni 5.
Je itachukua muda gani kubadili,na kadi pia itabadilishwa,kama itabadilishwa itachukua muda gani kupata kadi nyingine?
Nawasilisha
Mimi nilienda nikawaambia kuna million 70 zinatakiwa kuingia humo kuna dada karembo we kalichangamkia sana walibadili ndani ya dakika 12 tu..
Masikini ya mungu na deal lenyewe likabuma..
Ila kama miezi 5 baadae zikaingia kama 30 m hivi..
 
Mimi leo nimetoka huko nikawauliza wakasema sasa hivi zinapokea hadi 20 million, au alinidanganya!
 
Sio kweli huwezi kupokea na kutoa zaidi ya tsh milioni 5 nimeenda na kubadilisha, nilipewa fomu ya kubadilisha akauntI inayohitaji picha mbili za passport na nimekamilisha kubadili akaunti toka chap chap kuwa personal.
 
Dah, yule mfanyakazi kumbe na yeye kiazi tu...
 
Back
Top Bottom