Habari wakuu, poleni na majukumu. Siku ya leo nimeingia ajira portal na kukuta mabadiliko fulani nikashindwa kuelewa japo Hii ni mara yangu ya 7 kuomba kazi utumishi.
Kwa wale mliokuwa mkikubaliwa for oral interview, hivi ile sentence huwa inabadilika? Mfano kwenye picha nilizoambatanisha, mwanzo ilikuwa selected for oral interview na leo baada ya kuingia nimekuta shortlisted.
NB: tumekwisha kufanya oral interview ya TRA. Na baada ya kufanya nimekuta neno shortlisted na mwanzo ilikuwa selected for oral interview.
Hapo kuna picha mbili tofauti. Position mbili za mwanzo ni picha ya kwanza ambayo niliona wakati nimefanya written
Na position mbili za mwisho ni muonekano wa baada ya kufanya oral
Mwenye ufahamu na hili tafadhali atujuze. Je ni kawaida kuwa hivyo au ni system tu imecheza kidogo
View attachment 2163132
View attachment 2163133