Kubadilisha dini ndani ya ndoa

Mwenzi wako wa Maisha akibadilisha dini utachukua hatua gani?

  • Utaendelea nae/Divorce

    Votes: 1 4.8%
  • Utatengana nae/Separation

    Votes: 4 19.0%
  • Utaendelea nae

    Votes: 16 76.2%

  • Total voters
    21
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.

October

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2009
Posts
2,145
Reaction score
93
Nimekua najiuliza swali moja ambalo sina jibu lake naomba maoni yenu.
Uko na mwenzi wako wa ndoa na mnaishi vizuri kama wanandoa na japo mnakua na Ups na Downs za hapa na pale ingawa siyo serious sana. Ghafla mwenzi wako akapata mtizamo mpya wa kiimani akabadilisha dini yake. Sizungumzii kubadilisha dhehebu kama kutoka Katoliki kwenda Lutheran au kutoka Sunni kwenda Shia nazungumzia complete change mfano kutoka Uisilamu kwenda Ukristo and viceversa, au kutoka Ukristo/Uisilamu kwenda Hinduism and viceversa.

Na umejaribi kila njia za porini, za mijini za kifamilia na kidiplomasia kumshauri arudi kwenye dini yenu ya awali na akakataa kabisa, na wewe una msimamo thabiti katika dini yako hutaki kubadilisha.

Je utafanya nini? Please Vote


NB Option ya kwanza kwenye Poll ingetakiwa kuwa - Utaachana nae/Dovorce
 
Kama ni mimi imenitokea nitakaa naye chini anieleze kwanza kwa nini ameamua kuchukua uamuzi huo kwa maana kila jambo lina sababu yake, baada ya hapo ndiyo nitafikiria nini cha kufanya.
 
Mhhhh hii ni ngumu ile mbaya

kuna jamaa alikuwa na mke mcheshi,wanatoka out kila weekend

but ikatokea mke akaokoka yaani,
ilikuwa kama amekuwa mtu mwingine kabisa.
Hataki kwenda out,hataki mume anywe pombe,nyimbo ni za dini tu.yaani.
 
Hili ni tatizo kubwa sana.Linaweza kupelekea kuvunjika kwa ndoa na Sheria ya Tz LMA 1971 inasema wazi.
Binafsi siwezi kujua nitafanya nini.Akiokoka itakua poa sana na sitamwacha.
 
hili ni tatizo kubwa sana.linaweza kupelekea kuvunjika kwa ndoa na sheria ya tz lma 1971 inasema wazi.
Binafsi siwezi kujua nitafanya nini.akiokoka itakua poa sana na sitamwacha.

we unasema tu usisikie.
Bora aokoke bila kukusumbua
wengine wanaokoka na kuwaambia wenzi wao
waaache maisha ya dhambi,inakuwa ukisikiliza redio ni dhambi
ukitazama tv ni dhambi,wao redio za dini tu na tv za dini.
Wengine wanaambiwa kama mumeo hajaokoka achana nae.bwana
atakuletea mume wa kwako.
 


Hii ni ngumu mno! lakini kama amebadilika kiasi cha kuwa mtu mwingine kabisa kitabia na kuathiri hata ndoa iliyopo basi hapa ni vizuri tu kubwaga manyanga na kuanza moja katika jukwaa hili la ndoa. Vinginevyo ndoa hiyo haitakuwa na raha na maelewano yoyote yale.
 
Kama aki badilisha dini na akawa moderetae.....meaning halazimisi imani yake mpya kwako na watoto basi labda taratibu unaweza kukubali hali hiyo mpya kwenye ndoa yako. Ila sasa kazi ninayo ona mimi ni kwamba majority ya watu wanaoa mtu wa dini yao kwa makusudi...yani kuwa dini moja ni moa ya vitu mtu alivyo kua ana vitafuta katika mwenza. Sasa ukisha ondoa kigezo ambacho kwa mwenza wake kilikua muhimu basi ina kua kazi kweli.
 
kweli ni ngumu sana katika maisha ya ndoa

kama ulikuwa mtu wa kutoka mwenzi anagoma ndo mambo yanayoletea mtu anajikuta katika mahusiano mengine ,na kusababisha mtafaruku na mvurugano katika ndoa
 
Suala kama hilo nadhani ingekuwa busara kama angekaa chini nawe kabla ya kubadili na akupe sababu maalumu za yeye kubadili dini. Then mtadiscuss any implication ya uamuzi wake huo katika ndoa yenu na maisha yenu kwa ujumla na impact yake kwa watoto wenu. Then kama hakuna negative impact yoyote basi abadili tu na nitaendelea naye kwani naona uamuzi wake hautaniharibia plab ya maisha yangu wala ya watoto wangu

By the way suala la dini si la mtu binafsi?
 
By the way suala la dini si la mtu binafsi?

Mkiwa kwenye ndoa linakoma kuwa suala binafsi! Fikiria umefunga ndoa ya kikristo (ya mke mmoja, hakuna kuachana!) halafu mumeo anabadili dini na kuwa muislamu (ambapo ndoa ya wake hadi wanne ruksa, talaka pia ruksa!).
 
Mkiwa kwenye ndoa linakoma kuwa suala binafsi! Fikiria umefunga ndoa ya kikristo (ya mke mmoja, hakuna kuachana!) halafu mumeo anabadili dini na kuwa muislamu (ambapo ndoa ya wake hadi wanne ruksa, talaka pia ruksa!).

Aksante kwa kunikumbushia hilo, nadhani nilipitiwa katika nyanja hii.
Kweli hapa pagumu but kama nilivyosema ni suala la kujadiliana kwoanza kabla ya kuamua anachotaka kuamua.
 
Ishu ni kwamba kama maamuzi yake hayatakua na negative effects katika ndoa yenu acha abadili...mbona kuna ndoa nyigi tu za watu dini tofauti ziko imara! ila mh inataka moyo kwani kama mlikua mnatumia "kiti moto" gafla mwenzio anaanza kukutaza usilete home hapo hapata kalika!!
 
Mkuu wanaambiwa na nani waachane na wenzi wao baadaya kuokoka?

baba 'mchungaji'...Msindima, huwezi amini hawa wachungaji wanavokuwa na nguvu za ajabu dhidi ya 'kondoo wao' kiasi kila wanalosema linaonekana limetoka juu!πŸ˜•
 
baba 'mchungaji'...Msindima, huwezi amini hawa wachungaji wanavokuwa na nguvu za ajabu dhidi ya 'kondoo wao' kiasi kila wanalosema linaonekana limetoka juu!πŸ˜•
Kwa kweli imani ni kitu cha ajabu kabisa sasa najiuliza hao wanamama wanapoambiwa wawaache waume zao huwa wanakuwa wamefanywaje maana wapo wanaotekeleza kabisa!!
 
mwanaume akiamua kubadilisha dini hakuna mwanamke anayeweza ku-counterfeit,NANI ANABISHA?
 
mwanaume akiamua kubadilisha dini hakuna mwanamke anayeweza ku-counterfeit,NANI ANABISHA?
........... Usigeneralize wanawake wengine wamekomaa! hebu mfanyie hayo nyamayao uone labda kama kubadili kwako dini hakutaathiri ndoa yenu
 
Kwa kweli imani ni kitu cha ajabu kabisa sasa najiuliza hao wanamama wanapoambiwa wawaache waume zao huwa wanakuwa wamefanywaje maana wapo wanaotekeleza kabisa!!

MJ1, mi hata sitakagi kujua..ila jamani vitu kama hivi mtu akitafuta kanyumba kadogo mtamlaumu?
 
Kufuatana na sheria ya Ndoa ukibadili dini kinyume na ile uliyokuwa nayo wakati wa kufunga ndoa ni ushahidi tosha kuwa ndoa imevunjika beyond repair.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…