Kubadilisha dini ndani ya ndoa

Kubadilisha dini ndani ya ndoa

Mwenzi wako wa Maisha akibadilisha dini utachukua hatua gani?

  • Utaendelea nae/Divorce

    Votes: 1 4.8%
  • Utatengana nae/Separation

    Votes: 4 19.0%
  • Utaendelea nae

    Votes: 16 76.2%

  • Total voters
    21
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Kufuatana na sheria ya Ndoa ukibadili dini kinyume na ile uliyokuwa nayo wakati wa kufunga ndoa ni ushahidi tosha kuwa ndoa imevunjika beyond repair.

Mkuu unaweza kutusaidia zaidi ni ibara ipi na kifungu kipi cha sheria ya ndoa kinachosema hivyo?
 
If you are a Christian the only legal grounds for divorce is adultery. Therefore I would continue to dwell with him/her, Since we are together all the time, I would not cease persuading him/her, warning him/her about hell and the everlasting life that s/he has forsaken. I would intercede for him/her in prayers and use all means I can to win him/her back..

1 Corinthians 7.12-13,16 NIV
"If any brother has a wife who is not a believer and she is willing to live with him, he must not divorce her. And if a woman has a husband who is not a believer and he is willing to live with her, she must not divorce him.".... "How do you know, wife, whether you will save your husband? Or, how do you know, husband, whether you will save your wife?

mimi sitakubali, ina maana hapo tayari mmekwishaingia kwenye ufa wa ndoa, maana kupishana kiimani ni mija ya chanzo cha kuvunjika kwa ndoa
 
Huyo si bure kama macho mjomba/shangazi unaenda pigwa kanzu muda si MREFU
Namaanisha wajanja wameshamgeuza na kumshika akili. AMKA
 
baba 'mchungaji'...Msindima, huwezi amini hawa wachungaji wanavokuwa na nguvu za ajabu dhidi ya 'kondoo wao' kiasi kila wanalosema linaonekana limetoka juu!😕

Mkuu sikubaliana na wewe kama kuna mchungaji anaweza kumshauri mtu amwache mwenza wake kama kuna mchungaji wa sampuli hiyo atakua na matatizo ya kumtosha kabisa,mbona wapo wengi tu tumewaona wameokoka na wakaendelea kuishi pamoja? Nakupa mfano wa family friend yeye ndo alianza kuokoka mke wake alikasirika sana maana alijua kwamba hapa sasa hamna cha kwenda muziki wala bar kunywa alichukia sana,na huyo family friend alimvumilia sana na wachungaji walimshauri kuwa awe mvumilivu hata kama mke anamfanyia vituko huko ndani cha muhimu ni kumwombea,na baada ya kama mwaka hivi yule mke nae alikuja naye akaokoka.

Kwa hiyo kaka sikubaliani kabisa na kauli yako kama baba mchungaji anaweza kumshauri kitu kama hicho muumini wake.
 
Mkuu unaweza kutusaidia zaidi ni ibara ipi na kifungu kipi cha sheria ya ndoa kinachosema hivyo?

The Law of Marriage Act:

107. Evidence that marriage has broken down
(1) In deciding whether or not a marriage has broken down, the court
shall have regard to all relevant evidence regarding the conduct
and circumstances of the parties and, in particular–

(a) shall, unless the court for any special reason otherwise directs,
refuse to grant a decree where a petition is founded exclusively
on the petitioner's own wrongdoing; and

(b) shall have regard to the custom of the community to which
the parties belong.

(2) Without prejudice to the generality of subsection (1), the court
may accept any one or more of the following matters as
evidence that a marriage has broken down but proof of any such
matter shall not entitle a party as of right to a decree–

(a) adultery committed by the respondent, particularly when more
than one act of adultery has been committed or when
adulterous association is continued despite protest;

(b) sexual perversion on the part of the respondent;

(c) cruelty, whether mental or physical, inflicted by the respondent
on the petitioner or on the children, if any, of the marriage;

(d) wilful neglect on the part of the respondent;

(e) desertion of the petitioner by the respondent for at least three
years, where the court is satisfied that it is wilful;

(f) voluntary separation or separation by decree of the court, where
it has continued for at least three years;

(g) imprisonment of the respondent for life or for a term of not less
than five years, regard being had both to the length of the
sentence and to the nature of the offence for which it was
imposed;

(h) mental illness of the respondent, where at least two doctors,
one of whom is qualified or experienced in psychiatry, have
certified that they entertain no hope of cure or recovery;

(i) change of religion by the respondent, where both parties
followed the same faith at the time of the marriage and where
according to the laws of that faith a change of religion
dissolves or is a ground for the dissolution of marriage.
 
Mkuu sikubaliana na wewe kama kuna mchungaji anaweza kumshauri mtu amwache mwenza wake kama kuna mchungaji wa sampuli hiyo atakua na matatizo ya kumtosha kabisa,mbona wapo wengi tu tumewaona wameokoka na wakaendelea kuishi pamoja? Nakupa mfano wa family friend yeye ndo alianza kuokoka mke wake alikasirika sana maana alijua kwamba hapa sasa hamna cha kwenda muziki wala bar kunywa alichukia sana,na huyo family friend alimvumilia sana na wachungaji walimshauri kuwa awe mvumilivu hata kama mke anamfanyia vituko huko ndani cha muhimu ni kumwombea,na baada ya kama mwaka hivi yule mke nae alikuja naye akaokoka.

Kwa hiyo kaka sikubaliani kabisa na kauli yako kama baba mchungaji anaweza kumshauri kitu kama hicho muumini wake.

Msindima usiseme mimi nakupa mfano wa baba yangu mdogo mkewe aliokoka akaambiwa ni lazima ahakikishe mumewe naye kaokoka within three months akishindwa basi amuache. So campaign ikaanza mama akishirikiana na watoto -miezi mitatu ilipokwisha chuki ikatawala kwani baba yangu yule hakuwa ameokoka wala nini na ndio kwanza akazidisha mtungi maji- Mkewe akawa anamrefer kwa majina ya shetani, ibilisi sijui mdhambi ilimradi kero...... kidogo ndoa ivunjike ila baada ya kukalishwa chini ndo kidogo amepunguza siku hizi but alikuwa anaiendea talaka
 
MJ1, kuna mahali nimeeleza kuwa ukiona mchungaji anamshauri hivyo mwenza wa mtu kuwa aachane nae kisa mmoja kaokoka elewa huyo si mchungaji wa kondoo? na atakuwa na agenda zake za siri na pia atakuwa na matatizo ya kumtosha, kwa sababu inapotokea mmoja ameokoka basi wewe ulieokoka unapaswa kuwa mfano kwa mwenzako,sasa inapokuja mama/baba anapandikizwa chuki amchukie mwenzi wake hapo kweli kuna wokovu? maana navyoelewa wokovu unasisitiza AMANI,UPENDO,UVUMILIVU, na mambo mengi sana mema sasa ukuishindwa kuyafanya hayo kuna wokovu hapo?

Unajua unapokua kwenye ndoa sio kila ushauri unaubebea bango,kila ushauri unaopewa unapaswa kuufikiria kwa umakini,na kila anaekushauri sio kwamba anaitakia ndoa yako mema,wapo wengine lengo lao ni kuharibu tu na anapoona umeharibikiwa ndo furaha yao,nashangaa sana pia labda mama/baba anaokoka anashauriwa eti aachana na mwenzi wako nae anakubali tu kirahisi hapo napo kutakuwa na shida tena kubwa sana.
 
Ishu ni kwamba kama maamuzi yake hayatakua na negative effects katika ndoa yenu acha abadili...mbona kuna ndoa nyigi tu za watu dini tofauti ziko imara! ila mh inataka moyo kwani kama mlikua mnatumia "kiti moto" gafla mwenzio anaanza kukutaza usilete home hapo hapata kalika!!
...Unajua kiukweli Kimey effects lazima zitakuwepo na hii itatokana na misimamo mipya ya imani mpya ya huyo mwenza wako. Kama watu waliamua kuoana wakiwa dini tofauti tangu mwanzo ni rahisi sana kwani kila mtu ameshajua level ya imani ya mwenzie kwenye dini yake na anaamini ataimudu...Lakini kwa hili litasumbua tu!!!
 
Mkiwa kwenye ndoa linakoma kuwa suala binafsi! Fikiria umefunga ndoa ya kikristo (ya mke mmoja, hakuna kuachana!) halafu mumeo anabadili dini na kuwa muislamu (ambapo ndoa ya wake hadi wanne ruksa, talaka pia ruksa!).
Jiandae kwa talaka saba kabisaaa!!
 
hapa hakuna tena ndoa bali doa!
Yahitajiaka maelezo ya kina na siubabe juu ya jambo hili.
 
fata dini yako na yeye afate dini yake ila kuwe na common ground!!

Asante kwa comment yako ingawa imenifanya kuwa na maswali mengi zaidi.
Je watoto watafuata dini ya nani? Ni kweli kwamba watoto wanapata influence kubwa sana kutoka kwa mama kwa sababu mama ana muda mwingi zaidi na watoto kuliko Baba, huoni kwamba tayari watoto watakua na muelekeo wa dini ya mama yao? Kama mkeo alikua na ujasiri wa kukukatalia kurejea katika dini yenu ya zamani unadhani ataacha kuwasawishi watoto wafuate dini yake hii mpya?
 
...swali hili linafanana kidogo na lile la kumshawishi mwenzio abadili dini kabla ya kufunga nae ndoa.

Dini ni imani, so long as anazingatia mipaka ya ndoa yenu bora huyo huyo kuliko yule asiyeamini chochote. "Kila dini ina miongozo ya ndoa, lakini si kila ndoa zina miongozo ya dini!"

Endelea nae mpaka kifo kitapowatenganisha.
Huo ni mtizamo wangu tu.
 
Asante kwa comment yako ingawa imenifanya kuwa na maswali mengi zaidi.
Je watoto watafuata dini ya nani? Ni kweli kwamba watoto wanapata influence kubwa sana kutoka kwa mama kwa sababu mama ana muda mwingi zaidi na watoto kuliko Baba, huoni kwamba tayari watoto watakua na muelekeo wa dini ya mama yao? Kama mkeo alikua na ujasiri wa kukukatalia kurejea katika dini yenu ya zamani unadhani ataacha kuwasawishi watoto wafuate dini yake hii mpya?

'...bendera fata upepo'

...ni makosa kuwalazimisha watoto wafuate dini ya mama, au baba ati kwakuwa wewe 'umezaliwa' katika dini hiyo. Dini ni kuisoma, kuielewa, kuiamini, na kuyazingatia mafundisho yake.

Wape elimu ya dini unayoamini wewe mzazi, pia wakuone nawe unafuata maadili ya dini yako kiukweli. Wakivutiwa, heri yako...

Dini ni Imani, huwezi mlazimisha mtu aamini unachoamini wewe, atakudanganya tu!
 
mkishaingia ndani ya ndoa mimi inakuwa sisi na hapo suala lolote ni la wote, mi nafikiri ipo sababu na inaweza kuwa ya msingi iliyomfanya abadili dini, ila kama kubadili kwake dini kumeathili mahusiano ya kifamilia kama vile kubadili kabisa mfumo na utaratibu wenu wa maisha hapo ndoa inaweza kuwa karaha kwasababu ulimpenda na kumuoa akiwa mtu wa aina fulani na ni mfumo wake wa maisha pia ulimpendea, sasa kama kabadili mueleze athari za usoni kwa huo uamuzi wake kisha msikie anasemaje.
 
akiwa mtoto anatakiwa kulelewa katika imani ambayo mzazi anaiona ni sahihi hadi hapo atakapo pata ufahamu na kuamua ni imani ipi aifuate
 
fata dini yako na yeye afate dini yake ila kuwe na common ground!!

hicho kitu akiwezekani, kwani kama ulioa kanisani, na mkeo sasa akawa mwislamu basi hapo hakuna ndoa kwani kwa kiislamu hiyo ndoa ya kikristo ni batili
hii issue ni ngumu sana na mwisho wake ni divorce tu
 
Kama huyo ni mwanamke au ni mwanamume na wote mlikuwa waislm lakini huyu mwanamke au mwanaume akaamua kuuacha Uislam na kwenda kuwa Mkristo. kwa mujibu wa Imani, misingi, Sharia n.k za dini ya KIISLAM tangu siku aliyoamua kuwa Mkristo huyo siyo Mke au Mumeo tena. Ni sawa na kumuita Mkeo Mama au kumuita Mumeo Baba. Ukijaribu tu kumuita Mkeo Mama basi hiyo ni TWARAKA unatakiwa umuache mara moja kwani umemfananisha na Mamayo na huwezi kumuoa mamayo. au ukumuita Mumeo BABA basi inatakiwa akuache mara moja wka sababu huwezi kumfanya Babayo kuwa Mumeo. Hii ni kwa mujibu wa Dini ya Kiislam na halihitaji MJADARA hapa wa Kimagharibi ambapo Mwanaume na Mwanaume wanaoana na Mwanamke na Mwanamke wanaoana. Ukiwakataza eti HAKI ZA BINADAMU. Mungu tuseme hajuwi haki za Binadamu eti, kwa sababu angekuwa hajuwi basi angeumba wote kuwa WANAWAKE au wote kuwa WANAUME. Hebu ona hata Mbwa au Nyani n.k hawapandani wanaume na wanaume.

FUNGUENI AKILI ZETU
 
Asante kwa comment yako ingawa imenifanya kuwa na maswali mengi zaidi.
Je watoto watafuata dini ya nani? Ni kweli kwamba watoto wanapata influence kubwa sana kutoka kwa mama kwa sababu mama ana muda mwingi zaidi na watoto kuliko Baba, huoni kwamba tayari watoto watakua na muelekeo wa dini ya mama yao? Kama mkeo alikua na ujasiri wa kukukatalia kurejea katika dini yenu ya zamani unadhani ataacha kuwasawishi watoto wafuate dini yake hii mpya?

Pamoja na kwamba sababu pekee inayoruhusiwa kuachana katika ndoa ni uasherati, Nadhani hili la kubadilisha dini nalo ni gumu sana sana hasa ukizingatia kuwa hizi dini ni tofauti mno.

Kwa ujumla ni kwamba hata kama mtaendelea kuishi pamoja lakini ladha ya maisha ndio itakua imekwisha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom