Kubadilisha dini ndani ya ndoa

Kubadilisha dini ndani ya ndoa

Mwenzi wako wa Maisha akibadilisha dini utachukua hatua gani?

  • Utaendelea nae/Divorce

    Votes: 1 4.8%
  • Utatengana nae/Separation

    Votes: 4 19.0%
  • Utaendelea nae

    Votes: 16 76.2%

  • Total voters
    21
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
solution ya kikristo kwa suala hili ni kuwa "kama mtu ana mke asiyeamini na anakubali kuishi naye, asimuache"

hakuna ruhusa ya kumwacha kwa sababu ya kubadili dini, bali kuishi naye maisha matakatifu ya ndoa. ila akikataa kuishi nawe kwa ajili ya din yake mpya, una ruhusa kumuacha.

malezi ya watoto katika hali kama hii yatafuata dini ya baba (ama dini waliyozoea kama baba hana dini) hadi watakapokuwa na umri wa kuamua wenyewe wafuate imani gani
 
Bottom line ni "A woman has no religion until she gets married".
 
Ni pale wife wake alipobadili dini na kua Budha ndio naye alipojua na kuamini kua kila mtu asilia ni Budha na basi naye akajiunga huko. Dini ni imani pia ni nguvu itayofanya ndoa na jamii kwa ujumla kua pamoja, kulewana na kuwa na nguvu. Ni jambo la msingi wanandoa kua na dini moja hivyo maelewano kufuata dini gani kati ya wanandoa ni muhimu. Nitakua na uamuzi gani ikitokea kwangu, siwezi kujua itakuwaje kabla ya mawasiliano na mwanandoa mwenza, kuna uwezekano mkubwa ntaamini mafundisho ya Dini mpya na kujiunga huko.
 
Hapo uafrika wetu ndo matatizo yake yalipokalia,hivi kwa nini tunapenda kushabikia hizi dini kuliko waliozileta? Ndo kusema ulimbukeni au twamjua sana mungu.hebu fikiria mwana jf mwenzangu,kabla wakoloni hawajafika afrika tulikuwa tunaishi vp? Jamani hao ni wajanja tu kwanza wao wanatucheka mpaka leo,acheni hizo dini za kifisadi(deci nk)rudini kwa mababu zetu tulipotoka siyo lazima uitwe ahmed sayyd au joseph john ndo ukamilike,tusidanganyike na vijizawadi vya tende,magari,divai nk,kumbukeni tulipotoka enzi za mababu zetu kabla ya hawa mafisadi hawajaja.
Tumefikia kuvunja uchumba sugu eti hadi mmoja wetu afuate dini ya mwenza wake,hivi nani ana uhakika na anakokwenda????shuuuuuuuuuuut
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom