kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Unapobadilisha mtaala kutoka ule wa kujua tu na kuajiliwa kwenda ule wa kujua na vitendo zaidi na kujiajili kunahitaji uwekezaji mkubwa sana ambao ni ghali sana. Unapobadilisha mtaala maana yake utahitaji seti mpya ya walimu waliohitimu kwenye mitaala ya aina hiyo hiyohiyo au ya aina hiyo ambao Sasa hivi hawapo. Walimu waliopo hata wenye PhD na maprofesa hawawezi kujiajili wenyewe na hawana skills za kutosha za hands on.
Vyuo vikuu vyetu vingi hasa vile vya kibinafsi na vya mashirika ya kidini vinaongozwa na walimu wazee sana ambao wametokana na mitaala Ile ya zamani ya kufundishana zaidi madarani na mitihani migumu ya kwenye makaratasi, hawana uwezo wa kubuni Wala kupokea mbinu na mawazo mapya. Tunahitaji aina mpya ya madarasa, katakana na sehemu za kutoa elimu kwa vitendo, maana hata wale ambao wako makazini hawezi kuwafundisha ujuzi sahihi kwa wanafunzi watakaohitaji ujuzi na uzoefu wao kwakuwa na wao hawajui kwakuwa hawawezi.
Mitaala mipya ni nani ataifundisha? Tunahitaji uwekezaji mkubwa sana kabla ya kuingia hasara ya kuandika mitaala mipya. Wakati mwingine hatuhitaji kuandika mitaala mipya bali tunahitaji kwenda kuomba, kupewa na kutumia mitaala ya watu wengine kama vile wachina, wahindi, wakorea, wajapan au wakenya kwenye fani ambazo tunaona kuwa wao wako vizuri, nakuongeza TU machache ambayo tunahisi yahatuhusu sisi TU na utamaduni wetu.