Kwa sisi wa pikipiki hata hatupati shida kuelewa maana waya wa speedometer cable unachomekwa kwenye tairi linavyozunguka na wenyewe ndio unavyozunguka.
So mzunguko wa tairi linaathiri spidi inayosomwa moja kwa moja.
Ukitaka kuelewa basi tumieni hata mfano wa baiskeli za gia. Unaweza kuweka gia fulani laini sana hadi ukakanyaga kwa spidi kubwa lakini mwendo wa baskeli ukawa ni mdogo tu.
Ukichunguza unakuta ule upana halisi wa gia ya nyuma umekuzwa saaana. So mizunguko mingi haitafsiriki tena kuendana na spidi ya chombo kwenye tairi.
Hence: Ukubwa wa maduara yanayozunguka unaathiri mwendokasi wa spidi inayoonekana chombo kujongea mbele.