Kubadilishiwa matokeo ya mtihani - UDSM

Kubadilishiwa matokeo ya mtihani - UDSM

su li

Member
Joined
Mar 21, 2019
Posts
7
Reaction score
3
Jana natokea zangu chuo niko kwenye daladala ya Tegeta pembeni kuna mtoto mkali akapigiwa simu kwa maelezo niliyosikia kwa upande mmoja ni kuwa huyu binti alifanya mtihani wa Supplementary matokeo yametoka hakufanya vizuri.

Kwahiyo akashauriwa akate rufaa mtihani usahishwe upya baada ya matokeo yakitoka mchezo utachezwa.

Majibu yakitoka baada ya rufaa matokeo yatabadilishwa kwenye ku-upload hayo matokeo kwenye system ya chuo na binti ataonekana amefaulu hata kama matokeo yamekuja vipi.

Tahadhari kwa wahusika. Kuweni makini kuna msomi wa kutengeneza anaandaliwa hapa.
 
Mkuu uko dunia gani?? Hayo mambo mbona yapo sana tu??
 
su li, Hii kwa mfumo wa mitihani na matokeo wa UDSM ulivyo ni ngumu kutokea. Kama matokeo hayatabadilishwa na rufaa yake, ni ngumu mtu mwingine yoyote kuyabadilisha.
 
Hao wanaokuongoza sasa hivi ndiyo hawakufanya hayo siyo?? Naona unajitoa ufahamu mkuu!!
haya mambo yanatakiwa yapigwe vita maana hawa ndio wanakuja kuwa viongozi wa kuongoza taifa
 
Am walking away, trouble trouble in our education system am walking away
 
[emoji23][emoji23][emoji23]

Msomi wa kutengenezwa
 
Back
Top Bottom