Nilikua naongea na jamaa fulani wa Arusha kwa simu, kwenye background nikawa namsikia jamaa wa Chuga analalamika kwa lafudhi ya ya Kiarusha akisema ;" Aisee chalii, mazeri amezingua aisee, kutuletea mambo ya futiboli huku chuga sisi hizo mambo gani aisee", mwenzake akawa kama anamuuliza ;"Kiaje Joo, si juzi ulikua unasema Godi ampe mazeri malaifu tele vile mambo sasa yanaanza kusomeka?", jamaa akaendelea "ni kweli chalii yangu, ila haya mafutiboli sisi hatuna mizuka nayo, yeye angeendelea kutujengea maukumbi kama AICC, na kutuletea mafestivo watu tujiachie mzuka mwingi, watu na mevesi yetu, hatujapata tu platifomu".
Nikajikuta nacheka sana, na nikaukumbuku huu uzi wako.
Kwa kweli ujenzi wa viwanja ulistahili sana Mbeya, Mwanza pia na Mtwara.
Mbeya watu wana mizuka sana ya soka, watu wakishavuna mahindi watoto wanahamia kucheza soka mashambani. Kule watu wanapenda soka, wana dream soka ila ndiyo hivyo, wenye nchi yao wanaamua wampe nani.
Labda mama ameona kwa kuwa Mbeya wamewapa nafasi ya Spika wa bunge na teuzi za majaji kadhaa nasi uwanja aupeleke kwingine ambako hawajapatapo.