Kubali au kataa lakini page ya Mange Kimambi ya instagram ndio talk of the town kwa sasa

Kubali au kataa lakini page ya Mange Kimambi ya instagram ndio talk of the town kwa sasa

Umejitahidi kutoa maneno ya kunyongonyesha but all in all insta INA fursa nyingi na almost kila icon,star,super star na matajiri Wapo huko so kama utaitumia vzr sion hyo girlish
 
C alisema wema anarudi ccm. Tunasubr utabr wake. Mm alinipa block kwa kumwambia ukweli. Akiongea uongo anasimamia uongo huo chuo. Hassan ngoma kafukuzwa clouds, Mara diamond hayupo vevo, nyumba ya south c yake, tiffah c wake, ukimwambia ukwel unakula block. Yeye na le mutuz wanataka uwasapot hata ujinga
Tayari Sepenga jana ame "fly back to CCM" Mkuu.
 
Naamini sote Tumeanza Mwezi Wa December wenye shamrashamshara za kipekee, nikiwa bado niko Arusha nikimalizia kazi, nimeona nirudi tena kwenu kwa salamu za December.

Kwanza nataka CHADEMA na Afisa Habari wenu mnayemheshimu Mange Kimambi mtambue kuwa watoto 1,300 wa Kibiti mnaotangaza kuwa wamepotea na kutaka kuwaaminisha Watanzania kuwa wamekufa sio kweli, Kamanda Simon Sirro anasema alitajiwa idadi hiyo kuwa ni ya watoto watoro wa shule (Absentees).

Na kwa kuwa Afisa Habari wenu anayetumiwa na Wazungu kuivuruga Tanzania na nyie kwa Unyumbu wenu mnamtukuza hajui tatizo la utoro Tanzania basi mmedandia hoja na kuanza kushutumu kuwa wameuawa na Serikali imenyamazisha vyombo vya habari visiripoti .

CHADEMA mchukueni Mange Kimambi wenu mpelekeni wilaya zote za Tanzania akajionee tatizo la utoro.

Mwambie Afisa Habari wenu anayefanya kazi kutokea Marekani kuwa kuna wilaya za Tanzania utoro umefikia hadi wanafunzi 7,000 .

Mwambieni wanaoripotiwa kuwa watoro wengine wamehama shule bila kutoa taarifa shuleni ama mamlaka za Serikali.

Mwambie wengine wanaolewa na kutoroka shule, mwambieni wengine wanaacha kusoma na kwenda kwenye uzalishaji mali na familia .

Na hii sio mara ya kwanza, ilikuwa inaokotwa miili ufukwe wa bahari Dar es Salaam. Afisa Habari wa CHADEMA Mange Kimambi akaanza kutangaza wananchi wanaua, na Viongozi wakuu wa CHADEMA wakadandia lakini mpaka leo hawajaonesha ni ndugu wa nani waliuawa kwa idadi ile.

Nataka kuwatahadharisha Watanzania dhidi ya uchochezi unaofanywa na Mange Kimambi.

Wazungu ni wataalamu sana wa kutengeneza akina Mange Kimambi ili waivuruge nchi. Wanatumia mitandao ya kijamii hivi hivi na wanashabikiwa na wananchi.

Tunayoyaona leo Libya yalianza hivi, Wazungu waliwatumia akina Mange Kimambi wakagombanisha watu na Serikali, wakawatengeneza vijana ili wamuue Ghadafi na walifanikiwa wakamuua Ghadafi.

Leo Libya imevurugika, haikaliki na wananchi wa Libya wamekuwa watumwa wanauzwa kama bidhaa. Wanadhalilishwa, na wanauawa kama kuku, Libya neema haipo tena. Libya imekuwa jehanamu .

Ni hayahaya yalifanyika Syria leo Syria ni balaa. Ni hayahaya yalifanyika Iraq. Yanayotokea Iraq wote tunayaona.


Najua Watanzania wanaakili timamu na wanauwezo wa kutambua upuuzi wa CHADEMA na Mange Kimambi wao ambaye baada ya Watanzania kuwaadhibu kwenye kura za udiwani juzi amejaribu kuhamasisha watu waanze kupambana na Serikali eti wameibiwa kura lakini amekwama.

Mimi naomba Watanzania tukiangalie Chama cha CHADEMA . Tuwaangalie viongozi wake, tuwapime wanaitakia nini nchi hii. Hivi chama Serious kinaweza kufika mahali kinamtukuza mgonjwa wa akili kama Mange Kimambi? Yaani Mwenyekiti Freeman Mbowe anamtaja kabisa kwenye hotuba yake na kumshukuru Mange Kimambi? Anayoyaposti Mange Kimambi yanafaa kwenye nchi ya wastaarabu kama Tanzania? Halafu ndio hawa wanataka wapewe nchi.

Tuonane Machame this Xmass .

Ngariba Mkuu
Arusha, Tanzania
01/12/2017

Kwa hiyo kwa vile huko yametokea hayo inamaana kama serikali inafanya madudu yasisemwe? Kama wapinzani wanashambuliwa na silaha za kivita Asiseme? Kama nchi inaendeshwa kidikteta asiseme? kama Kuna double standards kwenye maamuzi ya Mkulu Asiseme? kama watu wanakosa uhuru wa kuikosoa serikali Asiseme? Uhuru wa kuandamana kulingana na katiba ukipingwa Asiseme? kisa tu tuogope yasijekutokea kama ya wenzetu, c'mon man. Waliopigania uhuru walitaka wananchi tuwe na uhuru wa kuendesha mambo yetu kwa kufata Katiba ambayo sisi wenyewe tutaitunga na kuifata lakini kama sheria inavunjwa na watu ambao tumewapa mamlaka ya kusimama kwa nini Akae kimya kama anauwezo wa kuongea kwa niaba ya wengi. Muacheni afanye yale yanayomfaa kwa niaba ya nchi yake na wananchi wanyonge, muache atumie uhuru wake wa kujieleza, kuhoji nk kulingana na katiba inavyoruhusu na kulingana na haki za binaadamu.
 
Kama ndivyo basi ni habari njema hizi.
 
ddcc21d8b75531745493e941d93a2958.jpg
 
One who writes for fools is always sure of a large audience.
 
Kama ndo hii sababu imemtoa atarudi tena maana nakumbuka pia aliwahi kufungiwa akajitetea huko instagram! mh ila bora wamempumzisha tu maana anapilika mno kwake hakuna jema kila mara anakosoa tu.
ddcc21d8b75531745493e941d93a2958.jpg
 
Back
Top Bottom