Kubali ukatae lugha ni tatizo kwa elimu yetu

KILLERS KISS GUY

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2013
Posts
718
Reaction score
258
katika tafti yangu ndogo nimegundua lugha ya kigeni katika elimu yetu ni mwiba katika maendeleo ya elimu yetu, kwani ili mwanafunzi aelewe kinachofundishwa mwalimu hana budi kunyanganya kiswahili, mfano mpaka mwanfunzi aelewe swali linataka nini lazima alijue kwa kiswahili ndo atajibu
 
Snake cut cry....yaaani nyooka kata kuli AAA
 
katika tafti yangu ndogo nimegundua lugha ya kigeni katika elimu yetu ni mwiba katika maendeleo ya elimu yetu, kwani ili mwanafunzi aelewe kinachofundishwa mwalimu hana budi kunyanganya kiswahili, mfano mpaka mwanfunzi aelewe swali linataka nini lazima alijue kwa kiswahili ndo atajibu
kama kweli umefanya tafiti leta data ambazo zinaonyesha wanafunzi wamefaulu sana somo la kiswahili kuliko masomo mengine yanayofundishwa kwa lugha ya kigeni, yaani prove kuwa always wanafunzi wanafaulu kiswahili kuliko english,biology,physics,math,history etc ndo ntakuelewa.
 
Hebu angalia matikea ya darasa la saba.form4 na form 6 kiswahili performance yake ikoje. Lugha ya kusomea sio hii unayoongelea. Masomo yote itabidi yatafsiriwe kwa kishwahili. Fikiria geography.history.physics.chemistry.mathematics. Nakwambia kiswahili hakijitoshelezi kwa masomo mengi. Utaishia kutamka nwno la kiingereza kwa kiswahili. Hesabu za kiswahili. Calculus.numerical analysis.intergrate.differentiate.exponential function. Itakuwa ngumu kuliko ilivyo. Hebu nikuulize;Pole anaambiwa mtu ali aliyefiwa. Aliyeumia. Aliyechoka. Kwa kiingereza je?
Kwa kweli angalia kamusi ya kiswahili uone kama inajitosheleza. Sio. Inahitaji misamiati kibao tena ya kutunga sasa na haikuwepo kabisaaa.
Kama hujui lugha usidhani kiswahili kitakuokoa. Cha shule kigumuuu.
 
bold: tofautisha kati ya lugha ya kufundishia na lugha kama somo mkuu! Tanzania tunatumia kiingereza kama lugha ya kufundishia ktk elimu ya sekondari na vyuo lakini liafundishwa kama somo primary (kuanzia std III na kuendelea) hadi sekondari na baadhi ya vyuo.

kiingereza kama lugha ya kufundishia sekondari na vyuo ni tatizo kubwa kwa walimu na wanafunzi. mwalimu hajui kwa dhati anachokiongea na mwanafunzi haelewi anachokiongea mwalimu.

Walimu wa masomo ya english,biology,physics,math,history etc hulazimika kutumia kiswahili kwa 90% darasani wakijitetea kuwa wanafunzi hawaelewi kiingereza halafu notice wanawandikia kwa kiingereza wakati sababu kubwa ya kutumia kiswahili ni kuwa walimu wengi kiingereza kinawagonga.

hata baadhi ya walimu wa kiingereza hufundisha kiingereza kwa kiswahili. ukitaka data zaidi (endapo data za mleta mada hutaridhika nazo) nitakuandikia zingine.

Je, lini wanafunzi hawa wanaofunzwa kwa kutumia lugha ya kiswahili watakuwa tayari kuwaelewa walimu wao kwa lugha ya kiingereza ili walimu hao waache kutumia kiswahili darasani huko sekondari na vyuo?

Tanzania tunang'ang'ania kutumia Kiingereza kama lugha ya kufindishia kwa sababu ya ukoloni mamboleo. sababu zingine zote hazina mashiko

wanasiasa uchwara wamefanikiwa kuwaaminisha watanzania kuwa kiingereza ndio lugha inayotoa maarifa badala ya kufikiria kutoa maarifa kwa kutumia lugha inayoeleweka kwa mwalimu na mwanafunzi (kiswahili) ili lugha ya kiingereza ifundishwe kama somo na walimu waliobobea ktk kiingereza ili tuache kupeana vichomi vya lugha na maarifa.
 
Hebu angalia matikea ya darasa la saba.form4 na form 6 kiswahili performance yake ikoje. Lugha ya kusomea sio hii unayoongelea. Masomo yote itabidi yatafsiriwe kwa kishwahili. Fikiria geography.history.physics.chemistry.mathematics. Nakwambia kiswahili hakijitoshelezi kwa masomo mengi. Utaishia kutamka nwno la kiingereza kwa kiswahili. Hesabu za kiswahili. Calculus.numerical analysis.intergrate.differentiate.exponential function. Itakuwa ngumu kuliko ilivyo. Hebu nikuulize;Pole anaambiwa mtu ali aliyefiwa. Aliyeumia. Aliyechoka. Kwa kiingereza je?
Kwa kweli angalia kamusi ya kiswahili uone kama inajitosheleza. Sio. Inahitaji misamiati kibao tena ya kutunga sasa na haikuwepo kabisaaa.
Kama hujui lugha usidhani kiswahili kitakuokoa. Cha shule kigumuuu.

kufeli kwa wanafunzi kunasababishwa na mambo mengi (naamini bado unayakumbuka). hata Uingereza, ambako Kiingereza ndo lugha mama yao (kwa walio wengi) hufeli masomo yao pia

bold: kamusi za hayo masomo tayari zipo. ulizia TUKI pale UDSM. Hata hicho kiingereza tunachokilafukia kilikibadili Kirumi( lugha ya wakoloni wa Waingereza( wadau mtanisaidia kama nimekosea)). wakaeka msamiati wao, wakauingiza kwenye mfumo wa e;imu japo wataalamu walipata upinzani kama huu uliopo leo kwa lugha ya kiswahili

red: lugha hukua( huongeza msamiati) kila siku ndo maana kuna matoleo mbalimbali ya kamusi ktk lugha mbalimbali. angalia kamusi za kiingereza

hakuna lugha duniani inayojisheleza kwa sababu jamii inakumbwa na mabadiliko katika nyanja mbalimbali na hivyo kuhitaji msamiati mpya kila siku kukidhi mahitaji ya mawasiliano.

tuache kutawaliwa kiakili
 
Tatizo la msingi ni historia ndefu ya uwekezaji mdogo ktk elimu. Yanayoonekana ktk lugha ni matokeo au dalili za ugonjwa mkubwa. Tatizo la lugha liko dhahiri hata ktk Kiswahili. Dalili nyingine ni elimu ambayo sasa inalenga kwenye mitihani tu na si kuelimisha. Angalia jinsi serikali inavyohaha na kuanzisha madaraja ya ajabu ya ufaulu. Ukifikiri kwamba tatizo ni Kiingereza, basi hujaenda kwenye chanzo.
 
Umesahau ya marehemu Kanumba kwenye jumba la big brother?
 
hv kuna mtu anafeli kwa kushndwa kuelewa lugha?vp kuhusu wanaoenda kusoma nchi kama china japani ujeruman russia nk ambao hujifunza lugha kwa mwaka 1 tu?
 
Hebu angalia matikea ya darasa la saba.form4 na form 6 kiswahili performance yake ikoje. Lugha ya kusomea sio hii unayoongelea. Masomo yote itabidi yatafsiriwe kwa kishwahili. Fikiria geography.history.physics.chemistry.mathematics. Nakwambia kiswahili hakijitoshelezi kwa masomo mengi. Utaishia kutamka nwno la kiingereza kwa kiswahili. Hesabu za kiswahili. Calculus.numerical analysis.intergrate.differentiate.exponential function. Itakuwa ngumu kuliko ilivyo. Hebu nikuulize;Pole anaambiwa mtu ali aliyefiwa. Aliyeumia. Aliyechoka. Kwa kiingereza je?
Kwa kweli angalia kamusi ya kiswahili uone kama inajitosheleza. Sio. Inahitaji misamiati kibao tena ya kutunga sasa na haikuwepo kabisaaa.
Kama hujui lugha usidhani kiswahili kitakuokoa. Cha shule kigumuuu.

Halafu itakuwaje ukijua kuwa hayo maneno unayodai ni ya Kiingereza mengi yao ni ya Kilatini na Kigiriki?
 
Back
Top Bottom