Kubananga: lugha ya Kiswahili, lawama ziende BAKITA

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,478
Reaction score
3,659
Ukweli ni kwamba kumekuwa na uharibifu mkubwa sana wa lugha ya kiswahili miaka ya karibuni. Tatizo hili lipo haswa kwa kizazi hiki kinachoitwa cha 2000 aka Gen Z. Imefika wakati hadi hawa vijana/watoto wanapoandika jambo au kuongea na wakafanya hivyo kwa usahihi ndio unashangaa. Sio unashangaa kwa kukosa bali unashangaa kwa kuwa sahihi. Mfano wa maneno haya ni kama;
1. aya - haya
2. hii nyimbo - huu wimbo
3. baazi - baadhi
4. naniliu - nahihii
5. una shangaa - unashangaa
6. lamani - ramani
7. dharula - dharura
8. mala - mara
9. mambo ambayo yaliyofanyika - mambo yaliyofanyika/mambo ambayo yalifanyika
10. mungu - Mungu

Yapo mengine mengi sana kiasi kwamba inaleta kichefuchefu. Tatizo hili linaanzia huko shuleni na hasa elimu ya msingi. Kwenye somo la kiswahili lipo somo la imla ambapo mwalimu husoma na mwanafunzi huandika kile kilichotamkwa na kwa usahihi.

Sasa yupo mtaalam mmoja kutokana na utafiti wake anasema ni kutokana na watu kutokuwa na tamaduni ya usomaji vitabu. Yaweza kuwa ni sababu kweli ila sio ya msingi. Msingi upo shuleni.

Sasa kutokana na hili tatizo kuwa ni la muda mrefu, hili baraza la kiswahili linaonekana lipolipo tu. Wao kazi ni kutohoa misamoiati mipya kuendana na mahitaji ya sasa na wamesahau kuwa kiswahili kinapaswa kutamkwa na kuandikwa kwa ufasaha kwanza.

BAKITA mna mchango kwenye uharibifu wa lugha adhimu ya kiswahili. Sasa mjiwekee malengo yafuatayo;
1. Kuainisha aina ya maneno ambayo yanakosewa sana na watumiaji.
2. Kuwakutanisha walimu wa shule za msingi Tanzania na kuwaeleza ukubwa wa tatizo.
3. Kuwapa walimu hao kozi ya ufasaha wa kiswahili.
4. Kuwakutanisha watu wenye ushawishi (influencers) hasa wa mitandaoni na kuhakikisha mnawapa elimu ya ufasaha wa lugha hii.
5. Kwenda kwenye vyombo vya habari na kutangaza mkakati wenu wa kuamsha ufasaha wa lugha ya kiswahili.

Mengine mnaweza kuongeza. Mkakati/malengo haya yawe ya mwaka mmoja, inatosha na baada ya miaka mitatu mnarudi kufanya tahmini. Tunahitaji kugongomea kiufasaha hii lugha kwenye akili na mioyo ya watanzania.

Usahihi:
Moderators Fang Maxence Melo Mhariri Boqin na wengine, naona kuna Mod karekebisha kichwa cha habari na bado kakosea. Isomeke, Kubananga lugha ya Kiswahili, lawama ziende BAKITA

Sio kama mlivyoweka hapo maana nami nitaonekana walewale
 
Apo namba 4 nafikiri kuna ufafanuzi zaidi unahitajika mkuu🤔
Na wewe sio apo, hi hapo
Haya, ufafanuzi ni kwamba, hawa jamaa huwa wana wafuasi wengi. Wanachoandika na kuongea kinasomwa na kusikilizwa na wengi. Wengi wao pia hawajui ufasaha wa lugha hii, hivyo wakielimishwa watakuwa mabalozi wazuri
 
Nafikiri kwenye namba 4 kuna kitu wana maanisha kama kupunguza ukali wa maneno na sio makosa ya kisarufi.
 
Ukweli ni kwamba kumekuwa na uharibifu mkubwa sana wa lugha ya kiswahili miaka ya karibuni. Tatizo hili lipo haswa kwa kizazi hiki kinachoitwa cha 2000 aka Gen Z. Imefika wakati hadi hawa vijana/watoto wanapoandika jambo au kuongea na wakafanya hivyo kwa usahihi ndio unashangaa. Sio unashangaa kwa kukosa bali unashangaa kwa kuwa sahihi. Mfano wa maneno haya ni kama;
1. aya - haya
2. hii nyimbo - huu wimbo
3. baazi - baadhi
4. naniliu - nahihii
5. una shangaa - unashangaa
6. lamani - ramani
7. dharula - dharura
8. mala - mara
9. mambo ambayo yaliyofanyika - mambo yaliyofanyika/mambo ambayo yalifanyika
10. mungu - Mungu

Yapo mengine mengi sana kiasi kwamba inaleta kichefuchefu. Tatizo hili linaanzia huko shuleni na hasa elimu ya msingi. Kwenye somo la kiswahili lipo somo la imla ambapo mwalimu husoma na mwanafunzi huandika kile kilichotamkwa na kwa usahihi.

Sasa yupo mtaalam mmoja kutokana na utafiti wake anasema ni kutokana na watu kutokuwa na tamaduni ya usomaji vitabu. Yaweza kuwa ni sababu kweli ila sio ya msingi. Msingi upo shuleni.

Sasa kutokana na hili tatizo kuwa ni la muda mrefu, hili baraza la kiswahili linaonekana lipolipo tu. Wao kazi ni kutohoa misamoiati mipya kuendana na mahitaji ya sasa na wamesahau kuwa kiswahili kinapaswa kutamkwa na kuandikwa kwa ufasaha kwanza.

BAKITA mna mchango kwenye uharibifu wa lugha adhimu ya kiswahili. Sasa mjiwekee malengo yafuatayo;
1. Kuainisha aina ya maneno ambayo yanakosewa sana na watumiaji.
2. Kuwakutanisha walimu wa shule za msingi Tanzania na kuwaeleza ukubwa wa tatizo.
3. Kuwapa walimu hao kozi ya ufasaha wa kiswahili.
4. Kuwakutanisha watu wenye ushawishi (influencers) hasa wa mitandaoni na kuhakikisha mnawapa elimu ya ufasaha wa lugha hii.
5. Kwenda kwenye vyombo vya habari na kutangaza mkakati wenu wa kuamsha ufasaha wa lugha ya kiswahili.

Mengine mnaweza kuongeza. Mkakati/malengo haya yawe ya mwaka mmoja, inatosha na baada ya miaka mitatu mnarudi kufanya tahmini. Tunahitaji kugongomea kiufasaha hii lugha kwenye akili na mioyo ya watanzania.
Mkuu, hivi kubananga ndiyo kuyatimba?
 
Back
Top Bottom