min -me
JF-Expert Member
- Jul 20, 2022
- 23,322
- 64,738
Nikirogwa na ephen , italeta maana sahihi?inategemea umerogwa na nani!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nikirogwa na ephen , italeta maana sahihi?inategemea umerogwa na nani!
😂😂😂inategemea umerogwa na nani!
Hilo neno huwenda lipo sahihi?🤔Huwenda ni kweli mkuu, ila kumbuka lugha yetu adhimu ya kiswahili ni lugha pana kwa hiyo siwezi nikafahamu kila neno. Naomba kueleweshwa maana yake🙏
muulize yeye kama anapenda kuroga! nawewe jiulize!Nikirogwa na ephen , italeta maana sahihi?
Mkuu,
Maana yake huwa ni ni ni mkuu🙏Hilo neno huwenda lipo sahihi?🤔
maneno hayo hayana ufanano. Kuyatimba ni lugha ya mtaani, japo neno "timba" ni neno sahihiHuwenda ni kweli mkuu, ila kumbuka lugha yetu adhimu ya kiswahili ni lugha pana kwa hiyo siwezi nikafahamu kila neno. Naomba kueleweshwa maana yake🙏
Capitalise a language.Huwenda ni kweli mkuu, ila kumbuka lugha yetu adhimu ya kiswahili ni lugha pana kwa hiyo siwezi nikafahamu kila neno. Naomba kueleweshwa maana yake🙏
Sio akuje ni aje. Akuje ni Kiswahili haribifu cha wakenya.Ndo lugha yetu hii tutafanyaje, nasubiri muanzisha uzi akuje anikosoe 😂😂😂
Kweli kabisa. Mtu unakuta ana hoja ila makosa ya kisarufi yanamwondolea thamaniMkuu,
Kwa jinsi ambavyo watu wanaichabanga lugha vibaya, nikiona maneno yenye ukakasi napita zangu mbio. Kifupi kuna kizazi kimekuja hapa kati kimeharibu sana lugha. Apa, apana, akuna, ujambo, dharula, kufuri, hii nyimbo...tena hii ndio kabisa unakuta wimbo mmoja jamaa wapo busy "hii nyimbo"...napata ukakasi napita zangu
#7 ipo sahihi, ila wewe mwalimu ndiye uliyekosea.Ukweli ni kwamba kumekuwa na uharibifu mkubwa sana wa lugha ya kiswahili miaka ya karibuni. Tatizo hili lipo haswa kwa kizazi hiki kinachoitwa cha 2000 aka Gen Z. Imefika wakati hadi hawa vijana/watoto wanapoandika jambo au kuongea na wakafanya hivyo kwa usahihi ndio unashangaa. Sio unashangaa kwa kukosa bali unashangaa kwa kuwa sahihi. Mfano wa maneno haya ni kama;
1. aya - haya
2. hii nyimbo - huu wimbo
3. baazi - baadhi
4. naniliu - nahihii
5. una shangaa - unashangaa
6. lamani - ramani
7. dharula - dharura
8. mala - mara
9. mambo ambayo yaliyofanyika - mambo yaliyofanyika/mambo ambayo yalifanyika
10. mungu - Mungu
Yapo mengine mengi sana kiasi kwamba inaleta kichefuchefu. Tatizo hili linaanzia huko shuleni na hasa elimu ya msingi. Kwenye somo la kiswahili lipo somo la imla ambapo mwalimu husoma na mwanafunzi huandika kile kilichotamkwa na kwa usahihi.
Sasa yupo mtaalam mmoja kutokana na utafiti wake anasema ni kutokana na watu kutokuwa na tamaduni ya usomaji vitabu. Yaweza kuwa ni sababu kweli ila sio ya msingi. Msingi upo shuleni.
Sasa kutokana na hili tatizo kuwa ni la muda mrefu, hili baraza la kiswahili linaonekana lipolipo tu. Wao kazi ni kutohoa misamoiati mipya kuendana na mahitaji ya sasa na wamesahau kuwa kiswahili kinapaswa kutamkwa na kuandikwa kwa ufasaha kwanza.
BAKITA mna mchango kwenye uharibifu wa lugha adhimu ya kiswahili. Sasa mjiwekee malengo yafuatayo;
1. Kuainisha aina ya maneno ambayo yanakosewa sana na watumiaji.
2. Kuwakutanisha walimu wa shule za msingi Tanzania na kuwaeleza ukubwa wa tatizo.
3. Kuwapa walimu hao kozi ya ufasaha wa kiswahili.
4. Kuwakutanisha watu wenye ushawishi (influencers) hasa wa mitandaoni na kuhakikisha mnawapa elimu ya ufasaha wa lugha hii.
5. Kwenda kwenye vyombo vya habari na kutangaza mkakati wenu wa kuamsha ufasaha wa lugha ya kiswahili.
Mengine mnaweza kuongeza. Mkakati/malengo haya yawe ya mwaka mmoja, inatosha na baada ya miaka mitatu mnarudi kufanya tahmini. Tunahitaji kugongomea kiufasaha hii lugha kwenye akili na mioyo ya watanzania.
Duh hasa wachaga tuna shida kwenye Apana na hapana ,ninafikiri hizi lugha zetu za asili zina mchango mkubwa kwenye kukosea, mfano yeye ni mwalimu wangu , huyu ni mwalimu wangu.Mkuu,
Kwa jinsi ambavyo watu wanaichabanga lugha vibaya, nikiona maneno yenye ukakasi napita zangu mbio. Kifupi kuna kizazi kimekuja hapa kati kimeharibu sana lugha. Apa, apana, akuna, ujambo, dharula, kufuri, hii nyimbo...tena hii ndio kabisa unakuta wimbo mmoja jamaa wapo busy "hii nyimbo"...napata ukakasi napita zangu
Ukisoma story yenye mtirirko mzuri wa maneno, yakiwa yamepangiliwa vizuri huchoki mkuu.Kweli kabisa. Mtu unakuta ana hoja ila makosa ya kisarufi yanamwondolea thamani
Sahihi ni dharura#7 ipo sahihi, ila wewe mwalimu ndiye uliyekosea.
niliwahi kuelekezwa na mtaalam wa Lugha. mathalani, maneno yakujirudia mfano: mjingamjinga, huyohuyo, walewale..usiruke nafasi. andika kama unavyotamka. hua tunakosea kuachanisha nafasi.Ni kweli inabidi tupate mwongozo wa Bakita maana binafsi ni mswahili wa kawaida. Natumia ujuzi niliojifunza darasani. Kwa neno lako hilo ni huyo huyo
Wachaga mna matatizo mengi sana, hasa kule Rombo🤣🤣🤣🤣Duh hasa wachaga tuna shida kwenye Apana na hapana ,ninafikiri hizi lugha zetu za asili zina mchango mkubwa kwenye kukosea, mfano yeye ni mwalimu wangu , huyu ni mwalimu wangu.
acha ubishi Raia Fulani yupo sahihi #7.#7 ipo sahihi, ila wewe mwalimu ndiye uliyekosea.
Rombo ,mbusi=mbuzi😁Wachaga mna matatizo mengi sana, hasa kule Rombo🤣🤣🤣🤣