Kubananga: lugha ya Kiswahili, lawama ziende BAKITA

Ivi neno sahihi ni kurogwa ama kulogwa ephen_ ERoni njoeni apa tujifunze .
Mkuu,
Kwa jinsi ambavyo watu wanaichabanga lugha vibaya, nikiona maneno yenye ukakasi napita zangu mbio. Kifupi kuna kizazi kimekuja hapa kati kimeharibu sana lugha. Apa, apana, akuna, ujambo, dharula, kufuri, hii nyimbo...tena hii ndio kabisa unakuta wimbo mmoja jamaa wapo busy "hii nyimbo"...napata ukakasi napita zangu
 
Huwenda ni kweli mkuu, ila kumbuka lugha yetu adhimu ya kiswahili ni lugha pana kwa hiyo siwezi nikafahamu kila neno. Naomba kueleweshwa maana yake🙏
maneno hayo hayana ufanano. Kuyatimba ni lugha ya mtaani, japo neno "timba" ni neno sahihi
 
Huwenda ni kweli mkuu, ila kumbuka lugha yetu adhimu ya kiswahili ni lugha pana kwa hiyo siwezi nikafahamu kila neno. Naomba kueleweshwa maana yake🙏
Capitalise a language.
kiswahili ❌️
Kiswahili ✅️
 
Kweli kabisa. Mtu unakuta ana hoja ila makosa ya kisarufi yanamwondolea thamani
 
#7 ipo sahihi, ila wewe mwalimu ndiye uliyekosea.
 
Duh hasa wachaga tuna shida kwenye Apana na hapana ,ninafikiri hizi lugha zetu za asili zina mchango mkubwa kwenye kukosea, mfano yeye ni mwalimu wangu , huyu ni mwalimu wangu.
 
Kweli kabisa. Mtu unakuta ana hoja ila makosa ya kisarufi yanamwondolea thamani
Ukisoma story yenye mtirirko mzuri wa maneno, yakiwa yamepangiliwa vizuri huchoki mkuu.

Ninachoipendea jf pamoja na udhaifu wake, watu wanakuja na txt, xaxa nk then wanasoma mchezo na kubadilika ghafla😀
 
Ni kweli inabidi tupate mwongozo wa Bakita maana binafsi ni mswahili wa kawaida. Natumia ujuzi niliojifunza darasani. Kwa neno lako hilo ni huyo huyo
niliwahi kuelekezwa na mtaalam wa Lugha. mathalani, maneno yakujirudia mfano: mjingamjinga, huyohuyo, walewale..usiruke nafasi. andika kama unavyotamka. hua tunakosea kuachanisha nafasi.
 
Duh hasa wachaga tuna shida kwenye Apana na hapana ,ninafikiri hizi lugha zetu za asili zina mchango mkubwa kwenye kukosea, mfano yeye ni mwalimu wangu , huyu ni mwalimu wangu.
Wachaga mna matatizo mengi sana, hasa kule Rombo🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…