Jukumu la kuwaunganisha wanachama na kutibu majeraha sio la alieshindwa uchaguzi bali ni la aliyeshinda. Aliyeshinda ndie anayepaswa kumhakikishia aliyeshindwa kuwa bado ana nafasi katika chama. Kama aliyeshinda atakuwa anamuambia aliyemshinda anyamaze kwa sababu alishindwa kidonda kitabaki kibichi.
Mbowe kuamini kuwa angeshinda sio jambo la ajabu. Jambo la ajabu ni yeye kukubali kushindwa na kukaa pembeni na kuwaachia walioshinda waendeshe chama chao. Kwa kufanya hivyo ametoa darasa kubwa kwa watanzania kuliko kama angeshinda.
Kuna binti mmoja chawa wa Lissu anamshutumu Mbowe kwa kuwalipia wajumbe kuhudhuria Mkutano Mkuu na kuwagharamia walipokuwa Dar. Haoni kuwa alifanya hivyo ili mkutano ufanikiwe kwa kuwa na wajumbe wa kutosha. Kama alivyochangia milioni 250 ili Mkutano uweze kufanyika. Badala ya kumshukuru wanambagaza.
Mimi ninachoona kinaendelea ni kama walioshinda hawaamini kuwa walishinda. Ndio maana bado wako kwenye kampeni mode ya kumtukana, kumbagaza kila wanayeamini alikuwa upande wa Mbowe pamoja na Mbowe mwenyewe. Kosa kubwa alilolifanya Sagrida ni kumshukuru Mbowe kwenye mkutano ambacho mgeni wa heshima alikuwa Lissu. Akashughulikiwa haraka sana kwa mbinu zile zile za character assassination. Sasa hivi wamewageukia Mrema na wenzake. Inasikitisha sana.
Amandla...