Kubenea na siasa za Kyela

Status
Not open for further replies.
Unajua Mwakalinga mbona kile kikundi ambacho kilikuwa kina jinadi kuwa kimeahidiwa laptop mbona hukukanusha na wala hukuwakataa kama ndo wapiga debe wako sasa hawa ndo walio chafua hali ya hewa.
Fidel80,

Mbona nilikanusha hilo la laptop? Hakuna shule au mtu yeyote niliyemwahidi laptop, unajua JF watu wanakuza mambo mpaka unacheka.

Hata huko jimboni wakati mwingine inabidi uwe mkali. Unakuta mtu uliyeongozana naye amesema jambo ambalo mpaka unaona aibu. Inabidi ukitoka hapo umwambie, mambo kama hayo hutaki. Mtu anatangazia umma kwamba una uwezo wa kujenga mbingu, wakati hata uwezo wa kutengeneza baiskeli huna.

Siasa za TZ zinatakiwa mabadiliko makubwa sana hasa upande wa kusema ukweli. Wapambe wanaweza kufikiri wanamjengea mtu kumbe wanambomoa. Mimi kule Kyela baada ya siku ya kwanza, nikawatoa wapambe kwenye utangulizi maana walikuwa wanawaambia wananchi uwongo ambao nisingependa kusikia.

Ukiwaambia hapana tusifanye hivyo, wanakumabia mambo mengine utarekebisha baada ya kupata. Ukiwakataza tayari ni ugomvi, wanaanza kudai huwaamini, unaleta mambo ya Ulaya nk.

Ni kazi kweli kweli, muhimu ni kutokukubali kubadili maadili au misimamo yako kirahisi. Wakati mwingine ni bora ushindwe huku umebaki na maadili yako kuliko kutafuta ushindi kwa njia zozote zile.

Siasa za TZ ni ngumu mno kwa mtu anayeamini. Mwenyewe nimejiuliza mara nyingi, natafuta nini hapa? Lakini pia unaona opportunities za kuweza kusaidia zilizopo na kwa matatizo ya kule vijijini, hata ukiweza kuwasaidia watu 20 kubadili maisha yao huenda ni bora kujaribu.
 
tutashinda!....................
 

Ninakuunga mkono FMEs kwa 100%.Kubenea ajitokeze kujibu haya madudu aliyoandika.
 
.

Good fms!.ajitokeze.nafikiri sasa imefikia muda watu wajulikane kwa majina yao halisi.
 
Tatizo la Tanzania ni kwamba uandishi wa habari wanadhani ni seheme ya kujipatia utajieri hivyo wamekuwa ni mamluki kwa kuhongwa fedha kwa ajili ya kumchafua mtuu thats why wa tz tunadharauliwa sana katika taaluma zetu
 

Wana Kyela sio nyie peke yenu mnaomuunga mkono Mwakipesile wapo Wanakyela wengine ambao wako nyuma ya Mwakyembe vile vile.

Mie sioni lolote baya aliloandika KUBENEA zaidi ya kueleza kwa kina hali halisi ya kisiasa na jinsi ambavyo Mwakyembe anapigwa vita.
Watanzania tufike mahali tuelewe maana yademokrasia na kwamba kila mtu anao uhuru wa kusema lile analowaza, analojua, alilosikia n.k. bila kuonekana kwamba ana majungu dhidi ya watakaoguswa!

Je kubenea amevunja sheria gani kwa kueleza yale aliyoyasikia na yanayozungumzwa na wananchi kuhusu yanayotokea Mkoani Mbeya? Mwacheni Kubenea atuhabarishe tujue jinsi nchi inavyovurugwa na watu wenye uchu wa madaraka ambao kwao wao uongozi hununuliwa kwa fedha na kwa kuwachafua wenzao kwa kutumia fedha zao.
 
Ndugu yangu Mwakalinga mpaka sasa umejifunza nini katika mchakato mzima huu? Sijui kama unaelewa kuwa siasa za Bongo ni maji taka, kama unaelewa je nn lengo lako hasa la kutaka kugombea ubunge?
 
Kumbe ndio maana watu wengine mnamwagiwa tindikali shauri ya kuandika majungu ambayo hayana ukweli hata mdogo. Ni taaluma gani hizo za kutumiwa na wanasiasa kuandika kila wanalotapika?

Shame on You Kubenea and your Newspaper!

Kama unaweza kupongeza uhalifu wa namna hiyo ni dalili kwamba hujakomaa kisiasa.

Jifunze ustahimilivu vinginevyo watu watajiuliza mara mbilimbili!

Nikutakie mpambano mwema lakini jiandae kukabilia na changamoto kali zaidi ya hiyo.
 
Nimesoma George siasa za huko kwenye ni mbaya sana lakini umeamua kuingia kucheza ngoma za kikwenu kaza buti na kwa kuwa unagombea ama una mapenzi na chama kinacho tumaliza sis watanzania basi tuta kumulika maana labda ungali enda upinzani japokuw abado ni haki yako kuingia CCM tungaliona nia yako ya kutaka kukokomboa watanzania wa huko unakosema .Ila uko ndani ya CCM haya twende na karibuni mwaka 2010
 
huyu sio tu ni upande wa mwakalinga, ndiye mwakalinga haswaaaaa
soma hapa najua ni msomaji wa JF na kwa vyovyote unajua anayeongelewa kuhusu siasa za Kyela ni Mwakalinga mwana JF. Umeshindwa nini kuniuliza mimi Mwakalinga aka Mtanzania kujua ukweli?

Mwakalinga has taken out his veil and announced that he is our JF'S Mtanzania!! Mwakyembe inasemekana yeye anaingia humu JF kwa majina mengi tu lakini si la Mwakyembe; will he be courageous enough like his nemesis to announce his true identity hapa ukumbini? hiyo itatusaidia kujua kama ninani anaetoa hoja badala ya sasa ambapo wahusika ndio wanaoandika nasi tunadhani ni wapambe wao!! Mtu yeyote anaeandikaka kitu anachokiamini na si majungu hawezi kujificha kwa kutumia majina bandia; mbona sisi wengi tunatumia majina yetu humu janvini!!
 
Mtasikia mengi ukifika hasa huo mwaka 2010,huu ni mwanzo tu na hilo ni jimbo moja tu bado yale mambo ya wazee wa Singida wanaotaka kijana fulani toka USA arudi ili "Kukomboa" jimbo la singida mjini!!!
 
Nafikiri wengi mliotoa comment ni wepesi sana wakusahau hapa tulipo leo asingekuwa kubenea na Mwakyembe sijui kama tungefika maana hata JF sina uhakika kama tulikuwa huru kutamka mafisadi kama tunavyotamka sasa. Wao ndio wame-risk maisha yao kwaajili ya maslahi ya umma. Tanzania kuna mashujaa watatu walioweza kujitoa ktk kupambana na Mafisadi hao sio wengine ni Dr. Slaa, Dr. Mwakyembe na Kubenea....

Ninawaomba wana JF wenzangu tuwaheshimu hawa jamaa na tuachane na majungu ambayo hayana msingi na tupunguze hasira tutumie busara na hekima.
 
Wana JF toeni hoja acheni kutukanana kupitia thread. Kama mna visa vyenu pelekeni uswahilini. Pinganeni kwa hoja si kwa matusi! Mf."Shame on You Kubenea and your Newspaper!" by Mtanzania, na "3.Wapo maswahiba wake hapa(MWAFRIKA NA MASANILO) watatufafanulia zaidi kuhusu Ujinga wa mbunge huyu mwenye mdomo mkubwa.Kulia kwenye media ndiyo kutatua matatizo yake." by Samwel Let the JF be The Home of Great Thinkers and not rigmaroles.
 
Mengine uliyoandika ni safi......however this one

....................Kumbe ndio maana watu wengine mnamwagiwa tindikali shauri ya kuandika majungu ambayo hayana ukweli hata mdogo. Ni taaluma gani hizo za kutumiwa na wanasiasa kuandika kila wanalotapika?

Shame on You Kubenea and your Newspaper!

Yes wewe ni binadamu kama wengine lakini..........that one........speaks volume..........

Hebu msome Mangi hapa chini........


.........notwithstanding the above.......Nakutakia kila la Kheri Mwakalinga aka Mtanzania wa JF
 
Mwakalinga has taken out his veil and announced that he is our JF'S Mtanzania!! Mwakyembe inasemekana yeye anaingia humu JF kwa majina mengi tu lakini si la Mwakyembe;

Inasemekana wapi, kwenye kijiwe cha gahawa au kwenye kilabu cha ulanzi pale kwa mama Gwakugole?

will he be courageous enough like his nemesis to announce his true identity hapa ukumbini? hiyo itatusaidia kujua kama ninani anaetoa hoja badala ya sasa ambapo wahusika ndio wanaoandika nasi tunadhani ni wapambe wao!!

Atumie jina lake ili iweje? na itakusadia wewe na nani?

Mtu yeyote anaeandikaka kitu anachokiamini na si majungu hawezi kujificha kwa kutumia majina bandia; mbona sisi wengi tunatumia majina yetu humu janvini!!

Bulesi, mbona wewe unatumia majina bandia? ni kwa vile unaandika majungu au kwa vile hauko courageous enough?
 

Bwa ha ha ha,

Mdomo huo ni mkubwa kama wa Haruna au kama wa Malima?
 

Mwakalinga kafulia big time kwenye hii kampeni yake. Yaani mambo anayoandika hapa (na wapambe wake) utadhani kama hakusomea shule ya IT kule Porrrrrrraaaandi.

Usijekucheza na pesa za kifisadi toka Monduli, zinageuza kila kitu.
 
.

1.Mwakyembe ka-divorce na Mengi na sasa ameoana na Kubenea.Huyu bwana ndiyo maana alimwagiwa tindikali usoni.Ata gazeti lake limeanza kukosa ubora tena.Limejaa majungu,unafiki na uongo.

Great,

Kama Mwakyembe ka-divorce na Mengi (big if...), je timu Mwakalinga itafunga rasmi ndoa na fisadi Rostam lini?


Ha ha ha,

inasemekana wapi? porrraaandi?

3.Wapo maswahiba wake hapa(MWAFRIKA NA MASANILO) watatufafanulia zaidi kuhusu Ujinga wa mbunge huyu mwenye mdomo mkubwa.Kulia kwenye media ndiyo kutatua matatizo yake.

Bwa ha ha ... huu mdomo ukubwa wake ni nusu au robo ya mdomo wa Samwel?
 

Ogah,

Ni rahisi sana ukiwa pembeni kuandika kama ulivyoandika. Lakini kwa mtu ambaye sasa miezi minne anatolewa kwenye magazeti ya nchi kwamba ni fisadi, kibaraka wa mtu, katuma vijana kuchoma mtu kisu, kamwagiwa mapesa na ujinga mwingine ambao hauna hata chembe ndogo ya ukweli. Hata watu ambao hawakujui wanaanza kuamini kwamba wewe ni mwizi. Inafika sehemu unasema enough is enough, siasa za jino kwa jino nazo zinafanywa na binadamu. Fuata sheria na maadili ya kazi yako, hakuna atakayekugusa. Ni maadili gani ya uandishi wa habari hao tunaowajadili hapa wanafuata?

Mkuu nimejifunza, Nipashe waliandika mambo ya hovyo hivyo hivyo. Msamalia mmoja wa JF hapa akaniunganisha na mhariri wao na nikaamua kuwa muungwana. Nikampigia simu kumwambia habari mliyoandika haina ukweli kabisa, chunguzeni. Kesho yake ndio akatoa makubwa zaidi kwamba kuna sms zimekutwa zikionyeshwa pesa zinavyosambazwa kutoka nje kupitia Arusha. Huku akijua ni uongo mkubwa wala hakuna kitu kama hicho. Unataka mtu kama huyo nimwambie nini tena zaidi ya lugha anayostahili? Kuna siku nitamwona uso kwa uso na nimwambie lugha anayostahili.

Nimetumia jina langu ili kila mtu awe una uhakika 100% kwamba alieandika ni Mwakalinga mwenyewe..

Uzuri wote wanaotumia magazeti yao kuchafua watu wengine wanajulikana. Na kila baya mtu analofanya kuna siku utawajibika nalo tu.

Hakuna anayekataza mwandishi kumchunguza mwanasiasa na huko kugundua scandals zilizojificha na kuzianika. Lakini sio sahihi kusema umemkuta Ogah anaiba kuku, huku unajua kabisa hujamwona Ogah popote hata akiiba kitumbua.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…