George Mwakalinga sio kijana kama unavyotaka kuonyesha, ana miaka 44 ambayo ni zaidi ya kuwa kijana.
Mwakalinga alimaliza shule mwaka 1997. Aliajiriwa na Lucent Technologies miezi michache kabla ya kumaliza shule yake. Baada ya kufanya kazi Lucent miaka minane, December 2005 alihamia Huawei Technologies ambako yuko mpaka sasa. Mwakalinga hajawahi kukosa kazi hata siku moja tokea alipomaliza masomo 1997. Sasa huo ni uanafunzi gani baada ya miaka 12? Lengo ni lile lile kudanganya watu waone Mwakalinga ni kijana tu! ni mwanafunzi tu.
George Mwakalinga hakufuatwa London na Mwakipesile au Mwang'onda. Sijui hata kama Mwakipesile amewahi kuwa London miaka ya karibuni. Mwakalinga aliamua kugombea ubunge tokea mwaka 2007 na March mwaka huo alituma watu kuonana na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kyela, bwana Mwakasumi na kumwambia dhamira ya Mwakalinga kugombea ubunge Kyela mwaka 2010. Picha na uthibitisho mwingine wa mkutano huo ambao ulifanyika pale Sativa Kyela vipo. Kumbuka hiyo ilikuwa mwaka mmoja kabla hata report ya Richmond kusomwa bungeni.
Mwakilishi wa Mwakalinga alikutana na Mwakipesile mwaka 2009, February kumwambia kuhusu dhamira ya Mwakalinga kugombea ubunge Kyela. Hiyo ni miaka miwili tokea Mwakalinga aanze harakati za kuwaambia baadhi ya wadau wa Kyela kwamba ana mpango wa kugombea. Team Mwakalinga iliamua kumwona Mwakipesile baada ya kupata uhakika wa kiasi kwamba Mwakipesile hana mpango wa kugombea. Kabla ya hapo hakukuwahi kuwa na mawasiliano yoyote kati ya Mwakalinga na Mwakipesile. Kuna watu wengine mbalimbali wa Kyeala, wanasiasa na wasio wanasiasa ambao team mwakalinga imekutana nao kuwaambia juu ya dhamira yake ya kugombea. Kama kukutana na mwana Kyela yeyote London au TZ ni makosa, si wataje wote niliowahi kukutana nao wakiwemo waliotumwa kunishawishi nisigombee? Watajeni akina Kifukwe, na wazito wengine huko jeshini.
Wana JF wanajua maana hiyo safari ilijadiliwa vikali hapa JF. Mwakalinga alikuwa Kyela kwa siku sita. Alifika yeye pamoja na familia yake siku ya Jumatatu (24/07/09) na kuondoka Kyela Jumamosi usiku (30/07/09). Kwahiyo, mwezi August Mwakalinga hakuwa Kyela wala hakukaa Kyela mwezi mzima.
Mwakalinga kila mara anaporudi nyumbani na familia yake yote hufanya sherehe ya pamoja kama njia ya familia yote kukutana pamoja maana kunakuwa hakuna muda wa kutembelea kila mtu katika siku hizo chache. Mwaka 2003 pia alipoenda na familia yake alifanya sherehe nyumbani na kuhudhuriwa na ndugu wote pamoja na majirani. Mwaka huu pia alienda nyumbani na familia ikiwa ni pamoja na mtoto wake wa mwisho ambaye alifika nyumbani kwa mara ya kwanza. Sherehe ya mwaka huu ikaongezewa nguvu na uamuzi wake wa kutangaza nia ya kugombea ubunge. Sherehe ilihudhuriwa na ndugu na wananchi wengine wa maeneo ya jirani. Hakukuwa na speeches wala maneno ya kwamba anaingia vitani.
Uongo! alitembelea kata 19 kati ya 21. Hakutoa msaada wowote wakati wa ziara nzima. Mwakalinga anatoa misaada mashuleni kwa muda wa zaidi ya miaka 15 sasa. Kuna kitabu cha misaada yote kiko pale Kyela Business Center (KBC) na anayetaka kuangalia anaweza kuhakiki na kuona lini alitoa msaada gani na wapi. Misaada yote hutolewa kiuwazi ila bila sherehe maana muda wote alikuwa hataki publicity.
I wish Mwakalinga angelikuwa na pesa zote hizo. Uwongo mkubwa sana! Hakuna hata mwananchi mmoja wa Kyela anayeweza kuthibitisha kwamba alipewa pesa kati ya shilingi 10,000 na 100,000. Kama yupo aende polisi kutoa taarifa. Tunamtafuta huyo Edson Matai ili kama kweli ni raia basi tumsaidie kumpeleka polisi ili akatoe ushahidi. Tumechoka Kyela kusingiziwa mambo ya ajabu. Inabidi tuanze kuwashughulikia wale wanaoona wanaweza wakasema au kuandika lolote bila ya chembe ya ukweli.
Hata ukimwuliza kichaa Kyela anajua kuna sehemu panaitwa KBC. Sasa mwandishi gani huyu na uchunguzi wa muda mrefu hata hajui kwamba hiyo kampuni inaitwa Kyela Business Center (KBC)? Hiyo KDC labda ni kampuni ya Kubenea ya kufikirika. Unajua habari za kupewa na watu wengine huwezi kuwa sahihi nazo.
Sasa huyo Mwakipesile, yeye mwenyewe anagombea ubunge na mara anaratibu shughuli za ubunge za Mwakalinga, mbona hayo maajabu?
Ni aibu kwa mtu kama Kubenea ambaye unajifanya mpiganaji, kuanza kutumia gazeti lako kuchafua watu wengine bila sababu zozote. Najua ni msomaji wa JF na kwa vyovyote unajua anayeongelewa kuhusu siasa za Kyela ni Mwakalinga mwana JF. Umeshindwa nini kuniuliza mimi Mwakalinga aka Mtanzania kujua ukweli? Mmezunguka kutafuta uchafu wowote na mmeshindwa sasa mnataka kumchafua mtu kwa kumhusisha kwa karibu na watu ambao mnawaona wachafu. Tatizo lenu ni kwamba hamuwezi hata sehemu moja kupata mahali ambapo Mwakalinga yuko karibu au hata anafahamiana na akina Lowassa, RA, Karamang au huyo Patel.
Mlianza na kusema Mwakalinga amepewa milioni 400. Mmeona wana Kyela wote wamewadharau baada ya kuona hizo milioni 400 hawazioni na hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza hata akasema amepewa laki moja na Mwakalinga. Sasa mnaanza majungu mengine ya kijinga, lakini na yenyewe yataishia patupu maana hamna data na uongo haudumu hata siku moja.
Acheni majungu na fitina; waache wana Kyela wachague kiongozi wanayemtaka kwa utashi wao. Kama mna ugomvi na Mwakipesile, pelekeni nguvu huko, kuanza kujaribu kumhusisha kila mtu haitawasaidia maana wana Kyela sasa wanajua nani anasema ukweli na nani anakimbilia magazetini kila saa kupaka wana Kyela wenzake.
Kumbe ndio maana watu wengine mnamwagiwa tindikali shauri ya kuandika majungu ambayo hayana ukweli hata mdogo. Ni taaluma gani hizo za kutumiwa na wanasiasa kuandika kila wanalotapika?
Shame on You Kubenea and your Newspaper!