- Thread starter
-
- #121
Kanda2,mkuu unajichanganya umesema hapo juu kuwa huna uwezo wa kupata Laptop halafu leo umetuma ujumbe mwingine ukisema unao uwezo wa kupata hizo Laptop lakini sio priority kwako.
kingine unaposema wewe huwa hutoa ahadi jee hutakuwa na Manifesto kwenye kampeni zako?
Sijawahi kuona siasa ambazo hazina AHADI iwe America,ulaya au Africa. Kama ajira OBAMA aliahidi kuzalisha ajira,na JK naye aliahidi hivyo hivyo. Ameanza kwa kufungua chuo kikuu cha DODOMA na miradi mingine. Mtu hupimwa kwa ahadi zake. Huwezi kufanya siasa za kufikirika.
Gordon Brown na David Cameroun wanatoa ahadi kila siku ambazo zingine hazitekelezeki ingawa wako ulaya ndio siasa. Kwa mtindo wako huo sidhani kama ubunge ni mahala pako lazima ubadilike.
Niambie mbunge gani mkweli kuanzia vyama vya upinzani hadi tawala? Wewe utakuwa malaika? Mfano utaenda kwa waziri wa miundombinu atakwambia kuwa barabara ya kyela itajengwa kwenye bajeti ya 2010/2011 wewe kama mbunge ukitoka hapo utaenda kuwaeleza wananchi wako kuwa barabara hiyo itajengwa muda ujao. Halafu wizara ghafla inabadilisha ratiba hiyo, hayo yanatokea sana.
Naona unaenda mbali mno. Kusema nitatoa laptop kila shule na kusema hata mimi nina uwezo wa kupata laptop 40 lakini sio priority yangu kwasasa ni vitu viwili tofauti.
Kila mtu ana uwezo wa kwenda kula Kilimanjaro hotel akitaka lakini kwa walio wengi itakuwa kwa cost ya mambo mengine chungu nzima na ndio maana mtu anasema sina uwezo wa kufanya jambo fulani. Maisha ni priorities.
Manifesto yangu haijawa tayari na itakapokuwa tayari wana Kyela wataelezwa. Ila tu sina mpango wa kutoa ahadi ambazo najua kabisa siwezi kuzitimiza.
Muhimu ni kwamba watu wengi hapa JF waliamini mimi ndiye nimesema nitapeleka laptops kila shule wakati kumbe yalikuwa maneno yako. Huoni kwa kuingiza kitu kama hicho ulikuwa hunisaidii?