Kubenea wa MWANAHALISI amenunuliwa na mafisadi?

Appreciated
u hv spoken ma mind
 
Wamejivua gamba. Nijuavyo mimi mdudu ajivuae gamba ni nyoka pekee, hakuna asiyefahamu kuwa nyoka ni mdudu mwenye sumu kali iletayo madhara kwa binadamu na viumbe wengine hai. Ajivuapo gamba inamaanisha kuwa hujiondoa uzee na kuwa nyoka mpya ambaye hata sumu yake huwa kali zaidi. Tutegemee nini baada ya chama chetu kujivua gamba?
 


Huyu ni mtu wa magamba ameandika hii.Ni aina nyingine ya Crap!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Homeboy

Jamaa anauza story hakuna kitu kama hicho! Ni vita wanapigana Magamba hao wanajaribu kumtumia Kubenea kama AK47. Kubenea is not that much cheap. Wanajua Magazeti yao ya Uhuru, Mzalendo, Habari leo hayauziki.

afadhali Rev umenishusha pumzi maana kuuza heshima uliyoijenga tangu unazaliwa kwa 20M ingekua kichekesho cha mwaka

Kubenea anatakiwa atambue kwamba utu haununuliki wala kuuzika, bali hudhalilishwa na kudhalilishwakutegemea na maanuzi ya mtendewa na si mtenda!!
 
Uongo mtupu huu! Kubenea bado na mwaminia..ni mmoja wa wanahabari makini walioko tanzania..mafisadi hawana nafasi.
 
Kubenea ni mtu aliyejijengea heshima sana katika tasnia ya uandishi wa habari na bila shaka gazeti lake linasomwa sana kwa sababu linaaminika na kuheshimiwa. Sitaki kupuuza yanayozungumzwa kwa sababu yeye ni binadamu na kila binadamu ana udhaifu wake. Lakini sitaki pia kuamini moja kwa moja kauli hii kwa sababu Kubenea anajua, pengine kuliko mtu yeyote, gharama alizolipa kwa kusimamia misimamo yake imara na kwa sasa hana la kupoteza kwa kuendelea kushikilia misimamo hiyo.

Lakini ni vizuri tukaelewa kwamba mapacha hawa watatu kwa sasa wamechanganyikiwa na wako tayari kuingia gharama yoyote ile katika kuhakikisha kwamba wanabaki salama na kujaribu kupigana kuifanikisha ndoto yao, ambayo hata hivyo HAITATIMIA. Jambo la kutilia maanani ni kwamba katika hali isiyo ya kawaida, msimamo mkali wa Mwanahalisi kuhusu mapacha hawa watatu toka baada ya maamuzi ya NEC mwezi uliopita umekuwa ni wa kutiliwa mashaka kwa sababu kwa kiasi kikubwa gazeti hili limejikita katika kukosoa na kuchambua maudhui ya maamuzi hayo, kiasi hata cha kuwaponda viongozi wakuu wa chama cha CCM, kuliko kuangalia the positive aspects of NEC deliberations. Hili lina hatari ya kutafsiriwa kama kupooza nguvu ya maamuzi yale na KWA KIASI FULANI INAWAPA NAFUU MAPACHA WATATU.

Kama hilo lina tafsiri ya kununuliwa au la sina hakika, labda matukio ya huko mbele yatatupa mwanga halisi. Hata hivyo milioni 20 kwa Kubenea ni dhihaka!
 
Taarifa za ndani kwenye duru za mwanahabari huyo zinasema kijembe kile cha kumnunulia Kubenea mtambo wa kuchapishia magazeti kimefanyiwa kazi na Kubenea yuko mbioni kupata mtambo mpya wa kisasa lakini kwa sharti la kuachana na habari hasi za Rostam na Lowassa kwenye gazeti lake na kuendesha kampeni kali dhidi ya msururu wa watu aliopewa katika miaka mitatu ijayo. Baadhi ya watu hao ni JK na familia yake, "Mtoto wa Mkulima", Magufuli, Chilligati, Nape, Sitta, Anne Kilango, Ole Sendeka, Lembeli, Mwandosya, Membe, Kinana, Mwakyembe, Mkuchika, Chatanda na Kigoda. Kubenea kakubali dili hilo ambalo tayari limemwingizia zaidi ya sh. milioni 20.

[/QUOTE]

Mwanzisha mada ni mbunifu na mtunzi mzuri wa hadithi za kusadikika. Milioni 20 kamwe hauwezi kununua mtambo wa kuchapia magazeti na wala haufikii robo ya advance payment; wala haitoshi kununua uhuru wa mtu makini. Kama ilivyo ada ni lazima tuulize; source ya information hiyo iko wapi?

Anyway "money changes every thing" and can buy even people but never will money be able to buy People Power!!!!.
 

Mwanzisha mada ni mbunifu na mtunzi mzuri wa hadithi za kusadikika. Milioni 20 kamwe hauwezi kununua mtambo wa kuchapia magazeti na wala haufikii robo ya advance payment; wala haitoshi kununua uhuru wa mtu makini. Kama ilivyo ada ni lazima tuulize; source ya information hiyo iko wapi?

Anyway "money changes every thing" and can buy even people but never will money be able to buy People Power!!!!.
 
Reactions: mja

Mkuu nimekuvulia kofia. Hawa jamaa walivyogandwa na uchafu, brashi za Kubenea haziwezi kufua dafu hata wangemnunua. Na pengine huu ndiyo uthibitisho wa jinsi jamaa hawa ambavyo hawana strategy na wale wanaowazunguka nadhani wako busy kuwapotosha na kuwaibia. Hata hii counter offensive ya ku-dramatize CCJ watu wameshaishtukia na sasa watu wameshajua source ni nini. Mimi nadhani dhambi ya kupora haki ya wananchi haiwezi kupoozwa na mipango ya watu kutaka kuondoka CCM hasa katka mazingira yaliyochochewa na baadhi ya watu (hasa hao mapacha watatu) ambao ni wachafu na hawastahili kuwemo katika utumishi wa umma. Afterall, imedhihirika kwamba ukiondoka CCM na kurudi unaweza pewa nafasi kubwa tu na mfano ni rafiki yao Wassira.
 

Mkuu nakugongea senksi. Wacha tuone, mengi yanakuja.
 
good point
 
Naomba Kubenea ajitokeze hapa atoe ufafanuzi nyie mnaomtolea mnakosea kuibuka tu nakutoa shutuma kwa huyu alieleta maada, mbona hamruhusu bongo zenu kujadili negative side?
Kubenea ni mtu makini sana na nina amini ni mmoja wa wana great thinkers jf pia naamini atachangia post hii.
Karibu KUBENEA......
 

Mkuu hii stori yako mbona ina harufu ya kuwatetea mafisadi? Porokwa aliulizwa maswali kadhaa siku ile akashindwa kuyajibu na kudhihirisha kwamba he was not himself. Lakini issue ya kutaka kuhama chama mbona inakuzwa? Kwani ni kuua mtu?
 

Mkuu sikuelewi, RA ni mwanachama wa CCM na rafiki mkubwa wa ******. Kifupi RACHEL ni CCM, sasa mbona unawaingiza CDM tena. Ndani ya CCM wote ni mafisadi tu, CDM kazi yao ni kupambana nao wote hata wakati wakiwa wananyosheana vidole.
 
Mbowe na slaa wote ni njaa tu, sasa wamepata mbulushi mwenye pesa, lazima watamsujudia.

Huyo mburushi kaamia lini CDM, taarifa nilizo nazo mpaka sasa ni kuwa yupo CCM, where he belongs.
 
Vuzuri sana bora yaishe,uhai ni bora kuliko sifa za kijinga we waache waseme tu we songa mbele,ulipomwagiwa tindikali waliishia kukupa pole je ungekufa si ungesahauliwa kama Katabalo nikukumbushe yule wa Loliondo Gate aliyefia DIA,wangapi wamekufa na wamesahauliwa wakati walijitoa muhanga watoto na ndugu zao wanateseka kwa manyanyaso ya moyo na shida za kila aina na waliofanya hayo wanapeta kwa sana,ufisadi ni kitu gani mbona hapa hakuna kiongozi wala mtumishi asiye fisadi wote mafisadi kwa kiwango chao mwenye kisu kikali ndiye anayefaidi zaidi,wewe ukiandika juu ya hayo wanapanga njama za kukuua na mateso mengine mengi kwani wewe uliumbiwa mateso? au kufurahisha watu fanya kazi yako uifaidi taaluma yako na uache umbea na wewe ufaidi uhuru wa kuishi siyo kila leo mara tindikali kakoswa kugongwa na gari n.k. ukishindwana nao ungana nao HONGERAAAAAAAA.:A S-rose:
 
Ni ukweli kabisa kuwa Kubenea amenunuliwa na mafisadi. Tatizo la Watanzania wengi ni wagumu kufikiri na kufanya uchambuzi wa mambo. Ukiangalia mwenendo wa habari zinatolewa na MWANAHALISI kwa zaidi ya mwezi sasa utaona gazeti hili limebadili mwelekeo kabisa.

Mei 18, 2011 niliweka post hii ifuatayo huku kwenye Jukwa la Siasa lakini moderators kwa "busara" yao waliona ni bora waitupilie mbali na kuificha kwenye folder ya Chit-Chat (porojo!):


Kubenea wa MWANAHALISI amenunuliwa na mafisadi?

Kuna tetesi kuwa Saed Kubenea, mhariri mkuu na mmiliki wa gazeti pendwa la MwanaHALISI naye ni miongoni mwa waandishi wa habari walionunuliwa na Rostam Aziz, Edward Lowassa na Andrew Chenge kwenye mkakati wa kuzuia mafisadi hawa wasifutwe uanachama wa CCM.

Tetesi ziliopo ni kuwa Kubenea kapewa pesa na mali kadhaa zenye thamani kubwa ili gazeti lake la MwanaHALISI liache kabisa kuwaandika habari yoyote mbaya (negative) kuhusu kina Rostam, Lowassa na Chenge tangu CCM ilipowataka wajitoe wenyewe kwenye uongozi.

Pamoja na kupigwa marufuku kuandika habari zozote mbaya kuhusu Rostam, Lowassa na Chenge, Kubenea pia amepewa kazi maalumu kuandika habari za kumchafua Rais Jakaya Kikwete, mtoto wake Ridhwani Kikwete, Samuel Sitta, Nape Nnauye, na viongozi wengine wa CCM.

Baada ya kuangalia mwenendo wa MwanaHALISI kwa wiki kadhaa na kuona ni kweli gazeti hili limekuwa na kigugumizi cha ghafla cha kuandika maovu ya Lowassa, Rostam na Chenge na badala yake linamshambulia Kikwete na Sitta kila kukicha, nimepata hofu kuwa huenda hizi tetesi si za kupuuza hata kidogo.

MUNGU IBARIKI TANZANIA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…