Kijembe ambacho mmoja wa mapacha watatu wa ufisadi, Rostam Aziz Abdulrasul, alikirusha kwa Saed Kubenea kuwa anaweza kumnunulia mtambo wa kuchapishia gazeti lake la MwanaHalisi mapema mwaka huu, kimegeuka kuwa "azma iliyotimia" baada ya mwandishi huyo machachari aliyejizolea sifa kemkem kwa ujasiri kutiwa mfukoni na sasa ni sehemu ya majeshi ya Rostam ya kumlinda na kuwasambaratisha wabaya wake!
Kubenea ambaye mwaka juzi alishambuliwa na watu "wasiojulikana" na kumwagiwa tindikali machoni karibu apofuke, kasahau yote hayo na sasa ni silaha ya kuaminika ya Rostam katika kujihami dhidi ya kampeni kali ya CCM inayoongozwa na Katibu Mwenezi Taifa Nape Nnauye ili mkuu wake mpya Rostam abakie na gamba lake.
Taarifa za ndani kwenye duru za mwanahabari huyo zinasema kijembe kile cha kumnunulia Kubenea mtambo wa kuchapishia magazeti kimefanyiwa kazi na Kubenea yuko mbioni kupata mtambo mpya wa kisasa lakini kwa sharti la kuachana na habari hasi za Rostam na Lowassa kwenye gazeti lake na kuendesha kampeni kali dhidi ya msururu wa watu aliopewa katika miaka mitatu ijayo. Baadhi ya watu hao ni JK na familia yake, "Mtoto wa Mkulima", Magufuli, Chilligati, Nape, Sitta, Anne Kilango, Ole Sendeka, Lembeli, Mwandosya, Membe, Kinana, Mwakyembe, Mkuchika, Chatanda na Kigoda. Kubenea kakubali dili hilo ambalo tayari limemwingizia zaidi ya sh. milioni 20.
Gazeti la MwanaHalisi ambalo limekuwa kwa muda mrefu msumari wa moto kwa mapacha watatu wa ufisadi kutokana na Kubenea kuamini kwamba wawili kati ya mapacha hao watatu walihusika na mpango wa kumtoa roho au kumpa kilema cha maisha, halitabeba taarifa tena za Lowassa wala Rostam ila za wabaya wao hao.
Mathalan, toleo la kesho kutwa la MwanaHalisi tayari lina taarifa ndefu ya Daniel Porokwa akiwamwagia sumu "maadui" wa RA na EL bila kujali kuwa gazeti lake lilimwandika Porokwa mwaka jana kuwa kibaraka wa Lowassa baada ya kujitoa kugombea Ubunge jimbo la Monduli. Porokwa "alizawadiwa" kazi ya Katibu Msaidizi wa CCM wa Wilaya, gari mpya aina ya NOAH, shilingi milioni 2, na ng'ombe kadhaa baada ya kujisalimisha na kukubali Lowassa amkanyage kichwani kwa mila eti ya Kimasai kama siyo ya kishirikina.