Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi bila 'kutumwa'na rais kwenda huko kutoa hizo pole kwa madereva yeye kama yeye hawezi kwenda?WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD), mkoa wa Morogoro, Mhandisi Godwin Andalwisye arejeshwe wizarani na nafasi yake ijazwe na mtu mwingine mara moja baada ya kuzembea kutimiza wajibu wake.
Uamuzi huo umekuja baada ya kiongozi huyo kushindwa kufanya ukaguzi wa usalama wa madaraja yaliyoko kwenye mkoa wake na kubaini kama kuna daraja linamatatizo hali iliyosababisha daraja la Kiyegeya lililopo eneo la Gairo ambalo linaunganisha mkoa wa Morogoro na Dodoma kuvunjika.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo(Jumatano, Machi 4, 2020) baada ya kutembelea eneo hilo na kukagua ukarabati ili kurejesha mawasiliano ya barabara. Waziri Mkuu ameshuhudia mrundikano wa magari na abiria hali ambayo haikumfurahisha.
“Hivi unajua udhahifu wako ni kwa sababu hukufanya ukaguzi kuona kama daraja limejaa mchanga au uchafu ambao umesababisha kipenyo cha kupitisha maji kuwa kidogo na maji yakalazimika kupanda juu hali ambayo ilisababisha daraja hili kusombwa na maji.”
Amesema wakati njia hiyo inarekebishwa itengenezwe njia nyingine ya muda ili kuweza kupitisha magari na kisha Serikali itachukua hatua baada ya kubaini nini kimesababisha.
Ili kuharakisha kazi hiyo inakamilika kwa haraka, Waziri Mkuu ameagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwelwe, Katibu Mkuu wa wizara hiyo pamoja na wahandisi wote wa TANROAD mkoa wa Morogoro na Dodoma leo wakutane kwenye eneo la tukio na wahakikishe kuanzia kesho (Alhamisi, Machi 5, 2020) njia hiyo iwe imefunguka.
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema atawasiliana na Mkuu wa Majeshi, Generali Venance Mabeyo ili aweze kupata msaada wa wanajeshi ili waongeze nguvu katika kuhakikisha kwamba mawasialaino yanarejea kwa haraka.
Akiwapa pole madereva na watumiaji wengine wa barabara waliokwama katika eneo hilo, Waziri Mkuu amesema “Nimetumwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuja kuwapa pole na kuwahakikisha kwamba Serikali inafanya kila linalowezekana ili kuifungua barabara hii.”
Ni upumbavu.Hawa ndio waliokuwa wanajinasibu kwamba ukiharibu mahali Fulani ni 'kwaheri mwalimu' hakuna cha kuhamishwa,lakini ndio haya tunashuhudia leo,watu wakiharibu wanahamishwa,na pesa lazima walipwe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Unafikiri ukiacha Mfugale, nani mwingine wa kuanza nae?Kafukuzwa kwa kuwa hajui au hazingatii majukumu yake.
Lakini vile vile mfumo wa zamani wa mkoloni chini ya PWD yaani public works department ni mzuri sana kuliko sasa kwa kutenga kila kilometer 10 kuna kikosi kazi kinacho hudumia kipande cha barabara kila siku kwa mwaka mzima.Laiti wangekuwa na vikosi kazi hatua za mapema zingechukuliwa.
Kwa sasa kweli Magufuli anajenga barabara lakini hakuna Preventive Maintenance schedule, kwa mfano nimeona barabara za lami zikijengwa Dodoma makao makuu lakini barabara hazifagiliwi zimejaa michanga.Ni wazi lifespan ya barabara za mji wa Dodoma zitadumu kwa muda mfupi.
Nakumbuka miaka ya 70 kampuni ya waingereza MOWLEM ilyokuwa inajenga barabara za Dar ilikuwa ina magari ya kusafisha barabara.Kulipunguza kuziba mitaro ya maji wakati wa masika.
Magufuli aanze kuwachukulia hatua wasaidizi wake wanaoshindwa kusafisha barabara za miji ndio wahujumu uchumi.
Watendaji ni sehemu ya huo "mfumo". Watendaji "wabovu" ni sehemu ya ubovu wa huo mfumo. Kuwawajibisha ni sehemu ya kurekebisha huo ubovu. Kuna watu wengine ni kama gadgets. Kila kitu ilimradi kinaihusu serikali sharti kirushiwe mawe! Funny and annoying.Ni mfumo ndio tatizo
Kama serikali bado haijabaini kilichosababisha na hiyo hoja ya mchanga kujaa PM kaitoa wapi?
Kafukuzwa kwa kuwa hajui au hazingatii majukumu yake.
Lakini vile vile mfumo wa zamani wa mkoloni chini ya PWD yaani public works department ni mzuri sana kuliko sasa kwa kutenga kila kilometer 10 kuna kikosi kazi kinacho hudumia kipande cha barabara kila siku kwa mwaka mzima.Laiti wangekuwa na vikosi kazi hatua za mapema zingechukuliwa.
Kwa sasa kweli Magufuli anajenga barabara lakini hakuna Preventive Maintenance schedule, kwa mfano nimeona barabara za lami zikijengwa Dodoma makao makuu lakini barabara hazifagiliwi zimejaa michanga.Ni wazi lifespan ya barabara za mji wa Dodoma zitadumu kwa muda mfupi.
Nakumbuka miaka ya 70 kampuni ya waingereza MOWLEM ilyokuwa inajenga barabara za Dar ilikuwa ina magari ya kusafisha barabara.Kulipunguza kuziba mitaro ya maji wakati wa masika.
Magufuli aanze kuwachukulia hatua wasaidizi wake wanaoshindwa kusafisha barabara za miji ndio wahujumu uchumi.
Tunamkumbuka mkoloni 😀😀😀😀Kafukuzwa kwa kuwa hajui au hazingatii majukumu yake.

Wazee wa kusubiri hadi mambo yaharibike ndio wachukue hatua. Huo ni uzembe kazini.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna taratibu ya kazi inasema "complain" or "comply". Bila shaka mhusika anaifahamu vema.Most likely huyuni mbuzi wa kafara.Inanikumbusha issue ya Muhumbili MRI na Xraymbovu mkuu wa taasisi akawajibishwa facts zilipowekwa wazi tatizo lilikuwa wizarani. Sasa huyu wa Tanroda kwa jinsi bajeti zinavyoombwa na mwenendo wa zina vyotoka nina mashaka makubwa kama kweli 100%ni uzembe wake. Tusubiri.
Ukija na mawazo mbadala unakumbwa na figisu Kama alizokumbana nazo kamishna jenerali wa zimamoto aliyepita, afande Thobias Andengenye!Business as usual, tuachane na huu utamaduni.
Mtu anaweza kaa miaka 20 katika ajira bila kutoa wazo lolote jipya la kuboresha taasisi kwa mwajiri wake.
Ni sehemu ya demotion. Huko wizarani atapangiwa kazi ya chini kuliko hiyo aliyokuwa nayo. Kuna kitu kinaitwa "demotion" jitahidi ikifahamu vema.
Hivi bila 'kutumwa'na rais kwenda huko kutoa hizo pole kwa madereva yeye kama yeye hawezi kwenda?
Sent using Jamii Forums mobile app
Ulifanya jambo la muhimu sana, Kwa basi kukaa na abiria siku nne ni tatizo la serikali pia au wanasubiria Corona Virus hapo. Pamoja na kwamba kuna juhudi za kurekebisha Daraja pia kulikutakiwa kuwe na juhudi hasa abiria kuendelea na safari hasa wa magari ya usafirishaji watuHAPO nilikwama kwenye basi ...nilifanya mawasiliano TANROADs kuomba waruhusu Mabasi kubadilishana Abiria (kufaulisha)
yanayotokea Moro/Dar yachukue abiria waliotoka Mwanza/Dodoma..na kugeuka... Hawakuzingatia ushauri huu. Japo kuna njia watembea kwa muguu wanavuka. Mabasi mengi walitafutia abiria wao Usafiri ng'ambo kasoro baadhi walioendelea kuhold ikiwemo KIDIA ONE. hapo kuna watoto wadogo wapo tokea jumatatu...wanahitaji msaada.
Hawa ndio waliokuwa wanajinasibu kwamba ukiharibu mahali Fulani ni 'kwaheri mwalimu' hakuna cha kuhamishwa,lakini ndio haya tunashuhudia leo,watu wakiharibu wanahamishwa,na pesa lazima walipwe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mawazo yake mbadala yalikuwa yepi? Tujuze.Ukija na mawazo mbadala unakumbwa na figisu Kama alizokumbana nazo kamishna jenerali wa zimamoto aliyepita, afande Thobias Andengenye!
Kikosi kazi yaani gang ikiiiongozwa na Myampala kama sikosei,eti watawala weusi wakafuta cheo na kikosi kazi sababu ya neno Mnyampala kwa sababu nyepesi tu.Tunamkumbuka mkoloni 😀😀😀😀
HujaelewaSasa mkuu ulidhania hilo wazo lako, lingeweza kutekelezeka kweli? Kwa ghafla tu,? Huku ni makampuni tofauti tofauti?? Yaani nimepakiza abiria wangu naenda MWANZA, nafika hapo unaniambia niwashushe, hapo nipakize wanaotoka bukoba nirudi dar? Wale wa kwangu, wavuke daraja, wakatafutiwe la mwanza?? Wakati kuna njia mbadala, hili hilo lifanikiwe ni mlolongo mrefu sana, hizo sio daladala mkuu!!
Ni sehemu ya demotion. Huko wizarani atapangiwa kazi ya chini kuliko hiyo aliyokuwa nayo. Kuna kitu kinaitwa "demotion" jitahidi ikifahamu vema.
Sent using Jamii Forums mobile app