Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivyo vishimo ni kero balaah, mwaka mzima vinakaa bila kuzibwaPM kumwajibisha mtendaji ni hatua nzuri. Lipo tatizo vishimo vidogo ambavyo hata kwa dharula vingezibwa kwa garama ndogo moram wakijipanga, vinakaa miezi, vinagarimu uharibifu magari, ajali na vifo. Tanroad waweke hotline ktk mabango yao tuwajuze.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni vyema wakawa creative na pia wafuate taratibu katika kufikisha mawazo yao. Tusiwe waoga kuja na mawazo mbadala, na pia tusisahau kufuata taratibu.Ukija na mawazo mbadala unakumbwa na figisu Kama alizokumbana nazo kamishna jenerali wa zimamoto aliyepita, afande Thobias Andengenye!
HAPO nilikwama kwenye basi ...nilifanya mawasiliano TANROADs kuomba waruhusu Mabasi kubadilishana Abiria (kufaulisha) yanayotokea Moro/Dar yachukue abiria waliotoka Mwanza/Dodoma..na kugeuka... Hawakuzingatia ushauri huu. Japo kuna njia watembea kwa muguu wanavuka. Mabasi mengi walitafutia abiria wao Usafiri ng'ambo kasoro baadhi walioendelea kuhold ikiwemo KIDIA ONE. hapo kuna watoto wadogo wapo tokea jumatatu...wanahitaji msaada.
Sory ni SUMATRAHebu tueleze; TANROADS wanahusikaje na mabasi kubadilishana abiria pande mbili za barabara?
Asante sana waziri Mkuu Majaliwa. Hivyo ndivyo inavyotakiwa ku react. Ukiendelea hivyo Ticket yako iko wazi ya wewe kumrithi Rais Magufuli 2025.WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD), mkoa wa Morogoro, Mhandisi Godwin Andalwisye arejeshwe wizarani na nafasi yake ijazwe na mtu mwingine mara moja baada ya kuzembea kutimiza wajibu wake.
Uamuzi huo umekuja baada ya kiongozi huyo kushindwa kufanya ukaguzi wa usalama wa madaraja yaliyoko kwenye mkoa wake na kubaini kama kuna daraja linamatatizo hali iliyosababisha daraja la Kiyegeya lililopo eneo la Gairo ambalo linaunganisha mkoa wa Morogoro na Dodoma kuvunjika.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo(Jumatano, Machi 4, 2020) baada ya kutembelea eneo hilo na kukagua ukarabati ili kurejesha mawasiliano ya barabara. Waziri Mkuu ameshuhudia mrundikano wa magari na abiria hali ambayo haikumfurahisha.
“Hivi unajua udhahifu wako ni kwa sababu hukufanya ukaguzi kuona kama daraja limejaa mchanga au uchafu ambao umesababisha kipenyo cha kupitisha maji kuwa kidogo na maji yakalazimika kupanda juu hali ambayo ilisababisha daraja hili kusombwa na maji.”
Amesema wakati njia hiyo inarekebishwa itengenezwe njia nyingine ya muda ili kuweza kupitisha magari na kisha Serikali itachukua hatua baada ya kubaini nini kimesababisha.
Ili kuharakisha kazi hiyo inakamilika kwa haraka, Waziri Mkuu ameagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwelwe, Katibu Mkuu wa wizara hiyo pamoja na wahandisi wote wa TANROAD mkoa wa Morogoro na Dodoma leo wakutane kwenye eneo la tukio na wahakikishe kuanzia kesho (Alhamisi, Machi 5, 2020) njia hiyo iwe imefunguka.
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema atawasiliana na Mkuu wa Majeshi, Generali Venance Mabeyo ili aweze kupata msaada wa wanajeshi ili waongeze nguvu katika kuhakikisha kwamba mawasialaino yanarejea kwa haraka.
Akiwapa pole madereva na watumiaji wengine wa barabara waliokwama katika eneo hilo, Waziri Mkuu amesema “Nimetumwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuja kuwapa pole na kuwahakikisha kwamba Serikali inafanya kila linalowezekana ili kuifungua barabara hii.”
Malkia alimwambia Nyerere (tunaemwabudu) kuwa "hamuwezi kujitawala" miubishi yake ona sasa!!Kikosi kazi yaani gang ikiiiongozwa na Myampala kama sikosei,eti watawala weusi wakafuta cheo na kikosi kazi sababu ya neno Mnyampala kwa sababu nyepesi tu.
Mkoloni ametuachia mambo mengi mazuri lakini sisi kazi yetu ni kuvuruga tu.Tumevuruga elimu,tumevuruga ushirika,tumevuruga kilimo ,tumevuruga siasa,hata kuvuruga East African Common Services.
Awamu ya tano mameneja wa TANROADS hawagusagwi kabisaaaa,hongera baba majaliwa kwa kudubutu kumngoa huyo wa morogoro.huku geita na kule serengeti ,kahama,mameneja wa TANROADS wamelala barabara ni mbovu mno mno,Ile inayotoka geita kwenda kahama ni mbovu haipitiki na imekaa maji.
LATRA Sasa HiviSory ni SUMATRA