Kubomoka kwa daraja la Kiyegeya: Meneja Tanroads Morogoro arudishwa Wizarani

Hivi bila 'kutumwa'na rais kwenda huko kutoa hizo pole kwa madereva yeye kama yeye hawezi kwenda?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa ndio waliokuwa wanajinasibu kwamba ukiharibu mahali Fulani ni 'kwaheri mwalimu' hakuna cha kuhamishwa,lakini ndio haya tunashuhudia leo,watu wakiharibu wanahamishwa,na pesa lazima walipwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni upumbavu.

Ni sawa na ilivyokuwa shule fulani ukifanya makosa unapewa adhabu ya kulima.

Maana yake kilimo ilikubalika kuwa ni adhabu, si kazi ya maana.

Na hapa tumeoneshwa kufanya kazi wizarani ni adhabu baada ya kufanya makosa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafikiri ukiacha Mfugale, nani mwingine wa kuanza nae?
 
Ni mfumo ndio tatizo
Watendaji ni sehemu ya huo "mfumo". Watendaji "wabovu" ni sehemu ya ubovu wa huo mfumo. Kuwawajibisha ni sehemu ya kurekebisha huo ubovu. Kuna watu wengine ni kama gadgets. Kila kitu ilimradi kinaihusu serikali sharti kirushiwe mawe! Funny and annoying.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri kuna yale yanayoonekana ambayo kiongozi mzuri anapaswa kuwa na utashi wa kuyang'amua mara moja na kuchukua hatua za haraka. Kisha huwa ni vema kufanya uchunguzi wa kina ili kujua undani/upana/mwelekeo wa tatizo. Pia kuna hatua huwa haziwezi kuchukuliwa kwa kuzingatia observation ya jumla jumla.
Kama serikali bado haijabaini kilichosababisha na hiyo hoja ya mchanga kujaa PM kaitoa wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Very great thinking and presentation.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunamkumbuka mkoloni πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kuna taratibu ya kazi inasema "complain" or "comply". Bila shaka mhusika anaifahamu vema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Business as usual, tuachane na huu utamaduni.

Mtu anaweza kaa miaka 20 katika ajira bila kutoa wazo lolote jipya la kuboresha taasisi kwa mwajiri wake.
Ukija na mawazo mbadala unakumbwa na figisu Kama alizokumbana nazo kamishna jenerali wa zimamoto aliyepita, afande Thobias Andengenye!
 
Ulifanya jambo la muhimu sana, Kwa basi kukaa na abiria siku nne ni tatizo la serikali pia au wanasubiria Corona Virus hapo. Pamoja na kwamba kuna juhudi za kurekebisha Daraja pia kulikutakiwa kuwe na juhudi hasa abiria kuendelea na safari hasa wa magari ya usafirishaji watu
 
Inapaswa kutegemea "umeharibu" nini. Je ni fraud au incapacity. Pia kila mwajiri huwa na sera yake ambayo huelekeza adhabu/hatua za kuchukuliwa kwa kila situation. Mambo hayaendeshwi kwa mihemuko mzazi. Kwenye team playing kuna mwingine anaweza asifae kushambulia akafaa kwenye ulinzi! Unamkumbuka Patrice Evra? Hakufaa kwenye nafasi moja kapelekwa kwingine aka-deliver.
Hawa ndio waliokuwa wanajinasibu kwamba ukiharibu mahali Fulani ni 'kwaheri mwalimu' hakuna cha kuhamishwa,lakini ndio haya tunashuhudia leo,watu wakiharibu wanahamishwa,na pesa lazima walipwe.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunamkumbuka mkoloni πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Kikosi kazi yaani gang ikiiiongozwa na Myampala kama sikosei,eti watawala weusi wakafuta cheo na kikosi kazi sababu ya neno Mnyampala kwa sababu nyepesi tu.
Mkoloni ametuachia mambo mengi mazuri lakini sisi kazi yetu ni kuvuruga tu.Tumevuruga elimu,tumevuruga ushirika,tumevuruga kilimo ,tumevuruga siasa,hata kuvuruga East African Common Services.
 
Hujaelewa

Bus za kampuni moja ndio zinafaulisha ..mfano

Kisbo inatoka kahama ikifika hapo inafaulisha na kisbo inayotoka dsm

Ally's inabadilisha na Ally'

Frester vs Frester

kuliko kwenda huko Iringa wanatumia siku mbili njia wakat ni safari ya masaa tu

na kampuni zilikua tayari kufanya hivyo , wakafika hapo wakakatazwa wakaambiwa warudi , matokeo yake zile bus ndio zinaingia leo , siku tatu niian

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni sehemu ya demotion. Huko wizarani atapangiwa kazi ya chini kuliko hiyo aliyokuwa nayo. Kuna kitu kinaitwa "demotion" jitahidi ikifahamu vema.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa nini unafikiri mimi sijui demotion ni nini? That is so condescending.

Basi ingetajwa kwamba anapewa demotion.

Kurudishwa Wizarani tu hata Waziri anafanya kazi wizarani.

Sasa utajuaje anapewa demotion na si promotion kwa kauli ya kurudishwa wizarani tu?

Ni vizuri tuwe na clear communication.

Watoto wanaojifunza wanaweza kuona kwamba kumbe kufanya kazi wizarani ni sehemu ya adhabu.

Hapo ndipo mama anaweza kuulizwa na watoto, "Mama, wewe unafanya kazi wizarani, kwani ulifanya kosa gani?".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…