Mawakili wa Lissu waibuka kidedea, Gereza la Ukonga lapewa maagizo

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252

Mahakama Kuu ya Tanzania imeuagiza uongozi Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam kufuata taratibu za Kanuni za Uendeshaji wa Magereza kwa kutowanyima Mawakili na Washauri wa kisheria kuzungumza na mteja wao lakini pia maafisa magereza kusimamia maongezi hayo kwa kukaa umbali ambao wataweza kuona tu na sio kusikia mazungumzo.

Soma pia:

Maagizo hayo yametolewa leo Oktoba 16, 2026 katika kikao cha Mahakama hiyo Masjala Kuu ya Dodoa kilichoketi Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam katika shauri na 7300/2026 lililofunguliwa na Kulwa Maduhu na wenzake ambao ni Mawakili washauri wa Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu wakidai kuzuiwa kuonana na mteja wao na wakati mwingine walipoonana nae kukosa usiri wakati wa mazungumzo.

Akisoma uamuzi huo Jaji Amir Mruma ambaye ni kiongozi wa Jopo la Majaji watatu waliokuwa wakisikilzia kesi hiyo amesema"Mamlaka ya magereza ya Ukonga wafuate kanuni kuhakikisa maafisa Maafisa Magereza wanaangalia usalama lakini wawe umbali wa kutosikia."

Pamoja na maagizo mengine yaliyotolewa katika uamuzi huo mahakama hiyo imetamka kuwa kitendo cha Maafisa Magereza kusikiliza mazungumzo ya Lissu na Mawakili wake au washauri wake wa kisheria ambao ni Paul Kisabo na Nashon Nkungu ni uvunjifu wa Kanuni ya 13 ya Uendeshaji wa Magereza.

"Tunatamka Kanuni 13 ya Uendeshaji wa Magereza ya mwaka 1968 inataka mashauriano kati ya mfungwa na mshauri au wakili wake yafanyike mahali ambapo Magereza wanaweza kuona lakini hawawezi kusikia."

Pamoja na hayo hukumu hiyo imetamka kuwa kuzuiliwa kwa Wakili Maduhu Oktoba 28, 2025 kuingia gereza la ukonga licha ya kuonyesha vitambulisho vyake vya uwakili sababu ikitajwa kuwa hayupo kwenye orodha ya Lissu aliyowasilisha gerezani sio sahihi na sio sababu inayojitosheleza kwani kama Wakili na mshauri wa kisheria alikuwa ana sababu za kutosha kuonana na mteja wake.

Hata hivyo pamoja na uamuzi mwingine Mahakama hiyo Mahakama imeagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kamishna Jenerali wa Magereza na Mkuu wa Gereza la Ukonga kuhakikisha Mawakili wa Lissu watakapoenda gerezani hapo waweze kukutana na kufanya mazungumzo na mashauriano na mteja wao pasina kuingiliwa kwa vyovyote wala kusikilizwa.

Chanzo: Jambo TV
 
View attachment 3691793

well done mahakama huru za Tanzania kwa weledi wenu katika kuamua mashauri,

maelekezo yenu ya kisheria yatazingatiwa na kufanyiwa kazi kwa vitendo kwa kuzingatia mazingira na hali halisi ya kiusalama ya eneo husika. Hata hivyo, suala la usalama wa wafungwa na mahabusu ni muhimu zaidi ya maelekezo ya jumla jumla tu.

Lakini pia kama wananchi,,
tunashukuru sana mahakama huru ya Tanzania kwa namna mnavyofanya mambo yenu kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.

Taasisi husika chini ya serikali sikivu ya CCM, itapokea maelekezo yenu kwa mikono miwili na kuona namna bora zaidi ya kuyatekeleza 🐒
 
mashoga ya ccm tarehe 6/11 yatapata stroke pale mwamba atakaposimamisha jiji.
 
well done mahakama huru za Tanzania kwa weledi wenu katika kuamua mashauri,

maelekezo yenu ya kisheria yatazingatiwa na kufanyiwa kazi kwa vitendo kwa kuzingatia mazingira na hali halisi ya kiusalama ya eneo husika. Hata hivyo, suala la usalama wa wafungwa na mahabusu ni muhimu zaidi ya maelekezo ya jumla jumla tu.

Lakini pia kama wananchi,,
tunashukuru sana mahakama huru ya Tanzania kwa namna mnavyofanya mambo yenu kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.

Taasisi husika chini ya serikali sikivu ya CCM, itapokea maelekezo yenu kwa mikono miwili na kuona namna bora zaidi ya kuyatekeleza 🐒
lipigwa miti la lumumba 2030 lazima likimbie nchi na mabasha yake.
 
wadau kwema, leo kesi ya kikatiba kuhusu bwana jera kuzuia mawakili wa Lissu imesomwa, ambapo serikali imebondwa kisawasawa sasa swali langu ni je haya ni maandalizi ya kisaikolojia kwa ccm na genge lao kuwa tarehe 06/11/2026 wajiandae kutoa mlio mkubwa zaidi? naomba majibu wakuu, only for unimbecile people and not idiots.
 
Call those imbecile and idiots to give you answers because,all already have answers fromr day one of the drama
 
wadau kwema, leo kesi ya kikatiba kuhusu bwana jera kuzuia mawakili wa Lissu imesomwa, ambapo serikali imebondwa kisawasawa sasa swali langu ni je haya ni maandalizi ya kisaikolojia kwa ccm na genge lao kuwa tarehe 06/11/2026 wajiandae kutoa mlio mkubwa zaidi? naomba majibu wakuu, only for unimbecile people and not idiots.
Kiboko cha Mazwazwa, habari za mchana.
Kwanza kabisa nikupongeze kwa kuleta mada hii hapa jukwaani. Kama mnavyojua, huko nyuma niliwahi kuandika kwa kirefu hapa hapa jukwaani kuhusu sheria za kimataifa zinazolinda haki ya mteja na wakili wake kuwasiliana kwa siri bila kuingiliwa na mtu yeyote. Hili si jambo la hisani, ni nguzo kuu ya haki inayofanya kazi duniani kote.
Sijajua ni kwanini kila siku serikali ya Tanzania na vyombo vyake kama Jeshi la Magereza huwa wanadhani nchi yetu ipo tofauti na mifumo hii ya kisheria ya kimataifa. Huwezi kumnyima mtuhumiwa haki ya msingi kabisa ya kujitetea kwa siri na mawakili wake kisha ukategemea utendaji wa haki mbele ya mahakama makini. Ni lazima ifahamike kitalamu kwamba mtuhumiwa anakuwa mtuhumiwa tu na siyo mfungwa mpaka hapo mahakama itakapomtia hatiani.
Kuna kauli mbiu na msingi mkuu wa kisheria duniani kote unaosema mtu hana hatia mpaka ithibitike vinginevyo (Innocent until proven guilty). Lakini ukiangalia mwenendo mzima, ulichokiona kikifanywa na hawa Magereza pamoja na amri zao kutoka juu ni kinyume chake kabisa; walikuwa wanaendesha mambo kwa msingi wa kwamba mtu ana hatia mpaka athibitishe hana hatia (Guilty until proven innocent).
Mimi nilijua tangu mwanzo kuwa kama Mahakama Kuu ingefanya kazi yake kwa weledi na bila upendeleo, haya ndiyo yaliyokuwa yanapaswa kuwa matokeo ya lazima. Askari magereza walikuwa wanavunja Kanuni zao wenyewe za Magereza za mwaka 1968 zinazowaruhusu kuangalia tu kwa macho lakini sio kusikiliza mambo ya ndani ya utetezi.
Kuhusu hilo swali lako kama huu ni mlio mkubwa unaokuja tarehe 06/11/2026, jibu langu kwako ni fupi tu: Mahakama ikisimamia weledi wake hivi hivi hadi mwisho kwenye kesi ya msingi, kila mtu atapata jibu lake na wenye mamlaka watajua kuwa nchi inaongozwa na Katiba na si matakwa ya mtu.
 
Ni hatua nzuri ,kwa nn maamuzi kama haya yanaamuliwa mda ukiwa umeisha ,,Najaribu kuaza, kuanzia mwanzo wa kesi Tundulisu alikuwa akilalamika juu ya jambo hili,hukumu trh 06 maamuzi yanatolewa Leo Tena kesi ikiwa crossed.hii ni hatali
 
Back
Top Bottom