Kucha za bandia ni hatari sana

Kucha za bandia ni hatari sana

Bulichekah

Member
Joined
Jan 12, 2014
Posts
68
Reaction score
186
Mazee, hizi kucha za bandia dada zetu wanazobandika juu ya kucha zao ni hatari sana.

Katika harakati za kupita pita mitaa ya town kusaka maisha, kuna mdada mmoja kajikwaa mguuni kwangu nikiwa nimevaa sendo ayani kanikwatua nyama na ule ukucha hadi nikaona kizunguzungu, halafu ananipa pole.

Nimemtazama kwa hasira kali yenye uchungu mwingi ikabidi tu nimuache lakini kiukweli haya makucha hata mkiwa mmelala ikatokea wakati anajigeuza akakugonga nao, asee ni zaidi ya kisu na maumivu yake ni hatare.

Na ninahisi yanaweza kuambuikiza tetanus haya makucha!
 
😀😀😁
Pole sana mkuu ila usidhani shida umepata mwenyewe hata sie wabandika kucha tabu tunaipata hasaa wakati wa kulala unaweza dhani umeng'atwa na nyoka 😊 kumbe ni likucha limekukwaruza.

Halafu hata raha za haya makorokocho sijui ni ipi arrggg😕 najaribugi kuacha ila nakuja kukumbuka nimeshatengeneza.
 
Sema kuna unacho amgalia c bure
.....[emoji28][emoji28][emoji28]
tapatalk_1574003001155.gif
 
Hata mie najua ni nene fulani hivi,huwa sio kali mara nyingi

Kucha natural huwa zinakwaruza zaidi ya hizi za kubandika

Ni muongo tu mtoa mada.

Hazijui hizi kucha.

Hazina nguvu yoyote....hata kukwangua vocha tu haziwezi iwe kumtoa mtu ngozi....atakuwa aliumizwa na kiatu
 
Sijui wanayapendea nini halafu huwa hayawapendezi. (Samahani huu ni mtazamo wangu)
Wengine tunawekaga ili tuinekane tuna vidole mana kama mimi nina vidole vifupi na kucha ni ndogo sana unaweza dhani ni tangawizi miguuni😂😂 so ili kuepusha kukanyagwa inabidi tuzibandike tu😨😥
 
Back
Top Bottom