Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,641
- 11,958
Habari wana jukwaa.
Kwanza namshukuru Mungu kunipa uzima na kuniwezesha kutimiza haki na wajibu wangu kikatiba wa kupiga Kura.
Pia nitoe pongezi kwa Tume kwa jinsi zoezi hili muhimu linavyoendeshwa hadi sasa, utulivu upo wa kutosha kwenye vituo vya kupigia Kura, pa si nashaka naweza kusema kuwa hali ni shwari kabisa na zoezi litakwisha vizuri bila ghasia zozote.
Changamoto kubwa inayo jitokeza ni hii ya kuchanganywa kwa majina ya wapiga kura kwenye vituo, yaani eneo ambalo mtu huyo alijiandikisha na Kisha kuhakiki jina lake baada ya kubandikwa na Tume siku chache kabla ya uchaguzi mtu anapokuja leo nakitambulisho chake akijua atapiga Kura kituo fulani alipo hakiki jina lake anakuta jina hilo limehamishiwa kituo na eneo tofauti kabisa.
Wengi wanahangaika kutafuta vituo vyao bila mafanikio mwisho wanakata tamaa na kughairi kupiga kura.
Pia kukosekana kwa weledi wa wasimamizi wa uchuguzi kwenye kutoa maelekezo sahihi kwa watu hao imekuwa changamoto nyingine inayo fanya zoezi kuwa gumu.
Jambo hili linaweza kusababisha wengi wakose haki yao ya msingi ya kupiga kura ikiwa hatua za haraka hazita chukuliwa hivi bado mapema.
Ila kiujumla zoezi linakwenda vizuri hadi sasa, mwitikio wa wapiga kura ni mkubwa japo si sawa na uchaguzi ulio pita.