Kuchangia Ujenzi wa madarasa ni maendeleo ya Vitu au Watu?

Kuchangia Ujenzi wa madarasa ni maendeleo ya Vitu au Watu?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Nauliza tu maana hapa Kihesa Iringa kuna watu wanasuasua kuchangia ujenzi wa madarasa kwa madai kuwa hiyo siyo sera ya chama chao.

Binafsi nimeshachangia mifuko 10 ya cement.

Nawatakia ninyi nyote Dominica yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama
 
Tunarudishwa Enzi ya ukoloni, tukichangia mwisho wa siku ni CCM ili fanya tutaambiwa kwenye kampeni, vijijini ndo wanaipenda CCM ngoja wakamuliwe kwanza!!!
 
Nauliza tu maana hapa Kihesa Iringa kuna watu wanasuasua kuchangia ujenzi wa madarasa kwa madai kuwa hiyo siyo sera ya chama chao....
Post hii inaonyesha ni kwa namna gani hilo jambo lenu mnaliendesha kisiasa. Mtasumbuka sana kufikia malengo ikiwa mmetawaliwa na siasa kiasi hicho.

Mnapoamua kufanya jambo la maendeleo kumbukeni kuondoa ushabiki wa vyama vyenu ili watu wawe free kushiriki.

Kama mnalazimisha kuwa matokeo yake ionekani ni kwasababu ya uongozi wa chama fulani mtaendelea kubishana na huku muda unasonga mbele.
 
Nauliza tu maana hapa Kihesa Iringa kuna watu wanasuasua kuchangia ujenzi wa madarasa kwa madai kuwa hiyo siyo sera ya chama chao.

Binafsi nimeshachangia mifuko 10 ya cement.

Nawatakia ninyi nyote Dominica yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama
Yapi mawazo yako ni ya vitu au watu.
 
Elimu ya msingi ni bure, hivi unajua maana ya bure wewe?
Nani kakuambia elimu ya msingi ni bure?

Ni kwamba elimu ya msingi haina malipo.

Gharama zote za msingi zinalipiwa na serikali siyo wazazi.
 
Nani kakuambia elimu ya msingi ni bure?

Ni kwamba elimu ya msingi haina malipo.

Gharama zote za msingi zinalipiwa na serikali siyo wazazi.
Kwa hiyo sii bure kwa wadanganyika,kwani wanachangishwa siku hizi,au wear mchochezi?
 
Uzi tayari!Hivi wewe jamaa huwa huna break hata ukatoka out na familia na ukasahau kidogo mambo ya JF?Mmmmh,the world moves so fast,if u dont stop 4 a while and watch,u might miss it!
 
Uzi tayari!Hivi wewe jamaa huwa huna break hata ukatoka out na familia na ukasahau kidogo mambo ya JF?Mmmmh,the world moves so fast,if u dont stop 4 a while and watch,u might miss it!
Huku ni nyumbani kwa the paptist Joni unataka aende wapi.
 
Nani kakuambia elimu ya msingi ni bure?

Ni kwamba elimu ya msingi haina malipo.

Gharama zote za msingi zinalipiwa na serikali siyo wazazi.
Uko timamu kweli?
Bure na haina malipo tofauti yake ni nini?
 
Uzi tayari!Hivi wewe jamaa huwa huna break hata ukatoka out na familia na ukasahau kidogo mambo ya JF?Mmmmh,the world moves so fast,if u dont stop 4 a while and watch,u might miss it!
Hana kazi ya kufanya,anaishi kwa semeji/ kula kulala.
 
Siyo bure inalipiwa na serikali ya CCM!

Elimu bure msingi na sekondari, na bima ya afya kwa kila raia Ni sera ya chama tawala... sipo tayari kuchangia..

Nipo tayari kuchangia ununuzi wa ndege, ujenzi wa sgr, manunuzi ya magari kwa waheshimiwa.
 
Uzi tayari!Hivi wewe jamaa huwa huna break hata ukatoka out na familia na ukasahau kidogo mambo ya JF?Mmmmh,the world moves so fast,if u dont stop 4 a while and watch,u might miss it!
Mbona wewe unakesha kilabuni ukinywa mbege?

Hiyo ni furaha yako na unakunywa kwa pesa zako za kubrashi viatu hakuna tatizo.

So fanya yako kwa amani bwashee CCM imekupa maisha bora!
 
Back
Top Bottom